Maridhiano ya kweli kati ya chama tawala na vyama vya upinzani yanawezekana kama haya yatazingatiwa

DaudiAiko

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2012
Posts
372
Reaction score
310
Kwa muda mrefu Sasa, Chama cha Mapinduzi kimeongoza kwenye dira ya siasa kwa kuwa na Sera zinazo kubalika kwa wananchi na kwa ujumla kufanya vizuri katika kipindi ambacho wawakilishi wake wamekuwa madarakani. Matokeo ya kuwa na rekodi nzuri kama hii ni nzuri kwa wananchi na Chama tawala lakini ni mbaya kwa vyama vya upinzani. Mbaya kwasababu katika kipindi cha miaka kumi iliyopita ushawishi wa vyama hivi kisiasa na nafasi yao kwenye demokrasia vimepungua kwa kiasi kikubwa sana.

Elewa kwamba mifumo iliyopo imechangia kuwa na amani na utulivu hata katika kipindi ambacho vyama vya siasa vingine vinaweza kupotea kabisa. Hata kama siasa za Tanzania ni za vyama vingi, kupotea kwa vyama vya upinzani kuta halalisha siasa za chama kimoja kwa njia ambayo sio ya moja kwa moja. Vyama vya upinzani haswa CHADEMA vimezungumza sana kuhusu maridhiano, lakini je maridhiano yenye tija kwa wananchi ni maridhiano ya aina gani?

Nitatoa mfano mmoja ambao unaohusu vyama vya siasa kuruhusiwa kufanya mikutano ya hadhara. Utagundua kwamba jambo ambalo lingetakiwa kuwa zuri limetumiwa vibaya na wanasiasa haswa wa CHADEMA na ni tishio kwa amani ya taifa. Upinzani bora kwenye nchi zilizokomaa kisiasa haziko hivyo. Natoa mapendekezo yangu ya maridhiano nikiwa na imani kwamba vyama vya upinzani vitabadilika na kwamba siku moja tutakuwa na afya kwenye demokrasia yetu kwa kuwa na vyama vya siasa vinavyofanya shughuli za siasa kwenye mipaka mizuri. Vilevile vyama vya upinzani vinatakiwa kuwa na mchango chanya kwenye masuala ya nchi

Kwanza kabisa, vyama vya upinzani vinatakiwa kuwa na angalau asilimia fulani ya wawakilishi bungeni hata kama vikishindwa uchaguzi kwa asilimia kubwa. Idadi ya wawakilishi ambayo ni ndogo lakini yenye mchango mkubwa na sio kukosoa kila kitu bila kuwa na sababu za msingi ni mwanga kwenye bunge letu. Vyama vya upinzani vingetakiwa kuwa na wawakilishi Ikulu ukizingatia kwamba Ikulu ni taasisi ambayo inatakiwa iweze kupokea mabadiliko ya uongozi yoyote. Vilevile taasisi ya ushirikiano ya siasa inaweza kuundwa kama njia ya kuvishirikisha vyama vya upinzani kwenye maamuzi ya serikali. Uwakilishi kwenye kila wizara pia ni muhimu. Hivi vitakuwa na manufaa kama majukumu haya yatatumiwa vizuri

Mwisho kabisa, naomba tufikirie kuhusu vizazi vijavyo, kuhusu mabadiliko yanayoweza kutatua changamoto kabla hazijatokea. Tuelewe kwamba maridhiano ya kweli yanahusu pande zote mbili. Chama tawala kukubali umuhimu wa mchango wa upinzani kwenye demokrasia yenye afya na vyama vya upinzani kuwa na mchango muhimu na kutekeleza majukumu yao professionally serikalini

Haya ndiyo maridhiano ya kweli na yenye tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla
 
..vyama vimekoseana mini?

..vimekoseana ktk jambo au mambo gani?

..Chadema wameikosea nini Ccm?

..Na Ccm wameikosea nini Chadema?
 
..vyama vimekoseana mini?

..vimekoseana ktk jambo au mambo gani?

..Chadema wameikosea nini Ccm?

..Na Ccm wameikosea nini Chadema?
Serikali ya CCM imeonekana kuwa gandamizi Kwa vyama vingine vya upinzani Kwa muda sasa. Ila ugandamizi huo unaodhaniwa unaweza ukawa unasababishwa na wawakilishi wa vyama vya upinzani kushindwa kufuata sheria au kufanya shughuli zao za siasa Kwa njia ambazo sizo. Ingawa matukio yaliyo chochewa na siasa kama shambulizi la Tundu Lissu au kukamatwa au kupotea Kwa wanaharakati wa CHADEMA yanadhihirisha kwamba ugandamizi upo Kwa kiasi fulani. Ila kama Wana CHADEMA wanaweza kuendesha shughuli zao za siasa kwa kufuata Sheria wakati wote basi mchango wao utakuwa wa muhimu na uwezekano wa matukio haya kutokea yata pungua
 
..mawazo yako ni mazuri, tatizo ni kwamba hayaendani na uhalisia wa kinachoendelea ktk siasa za Tanzania.

..Labda ungenitajia mwanachadema ambaye amefikishwa mahakamani na kupatikana na hatia kutokana na aliyoyafanya ktk uwanja wa siasa.

..Ccm inatumia Polisi, usalama wa taifa, watumishi wa umma, na mahakama, kusumbua, na kuhujumu, shughuli halali za vyama vya siasa.

..Tulifika mahali mamlaka zikatengeneza kesi ya ugaidi dhidi ya Mwenyekiti wa Chadema. Mashtaka yale hukumu yake ni kifo, na Ccm walikuwa radhi kucheza michezo michafu kiasi kile. Kabla ya hapo mamlaka ziliwahi kumtengenezea Juma Duni Haji na wenzake kesi ya uhaini
 
Ugandamizi wa vyama vya upinzani upo lakini je kuna njia ambayo pande zote mbili zinaweza kufikia muafaka?.
 
..ugandamizaji wa vyama vya upinzani unaouzungumzia ni kinyume na katiba na sheria.

..wanaohusika na jinai dhidi ya vyama vya upinzani wachukuliwe hatua za kisheria.

..hivi kwa mfano Mkurugenzi anahujumu uchaguzi, na kutoa matokeo ya uongo, sio mhaini na msaliti wa nchi?

..vyombo vya dola vikianza kuwachukulia hatua watendaji wanaoharibu chaguzi zetu HAKI nitarudi nchini.
 
Kwa muda mrefu Sasa, Chama cha Mapinduzi kimeongoza kwenye dira ya siasa kwa kuwa na Sera zinazo kubalika kwa wananchi na kwa ujumla kufanya vizuri katika kipindi ambacho wawakilishi wake wamekuwa madarakani. Matokeo ya kuwa na rekodi nzuri kama hii ni nzuri kwa wananchi na Chama tawala lakini ni mbaya kwa vyama vya upinzani. Mbaya kwasababu katika kipindi cha miaka kumi iliyopita ushawishi wa vyama hivi kisiasa na nafasi yao kwenye demokrasia vimepungua kwa kiasi kikubwa sana.

Elewa kwamba mifumo iliyopo imechangia kuwa na amani na utulivu hata katika kipindi ambacho vyama vya siasa vingine vinaweza kupotea kabisa. Hata kama siasa za Tanzania ni za vyama vingi, kupotea kwa vyama vya upinzani kuta halalisha siasa za chama kimoja kwa njia ambayo sio ya moja kwa moja. Vyama vya upinzani haswa CHADEMA vimezungumza sana kuhusu maridhiano, lakini je maridhiano yenye tija kwa wananchi ni maridhiano ya aina gani?

Nitatoa mfano mmoja ambao unaohusu vyama vya siasa kuruhusiwa kufanya mikutano ya hadhara. Utagundua kwamba jambo ambalo lingetakiwa kuwa zuri limetumiwa vibaya na wanasiasa haswa wa CHADEMA na ni tishio kwa amani ya taifa. Upinzani bora kwenye nchi zilizokomaa kisiasa haziko hivyo. Natoa mapendekezo yangu ya maridhiano nikiwa na imani kwamba vyama vya upinzani vitabadilika na kwamba siku moja tutakuwa na afya kwenye demokrasia yetu kwa kuwa na vyama vya siasa vinavyofanya shughuli za siasa kwenye mipaka mizuri. Vilevile vyama vya upinzani vinatakiwa kuwa na mchango chanya kwenye masuala ya nchi

Kwanza kabisa, vyama vya upinzani vinatakiwa kuwa na angalau asilimia fulani ya wawakilishi bungeni hata kama vikishindwa uchaguzi kwa asilimia kubwa. Idadi ya wawakilishi ambayo ni ndogo lakini yenye mchango mkubwa na sio kukosoa kila kitu bila kuwa na sababu za msingi ni mwanga kwenye bunge letu. Vyama vya upinzani vingetakiwa kuwa na wawakilishi Ikulu ukizingatia kwamba Ikulu ni taasisi ambayo inatakiwa iweze kupokea mabadiliko ya uongozi yoyote. Vilevile taasisi ya ushirikiano ya siasa inaweza kuundwa kama njia ya kuvishirikisha vyama vya upinzani kwenye maamuzi ya serikali. Uwakilishi kwenye kila wizara pia ni muhimu. Hivi vitakuwa na manufaa kama majukumu haya yatatumiwa vizuri

Mwisho kabisa, naomba tufikirie kuhusu vizazi vijavyo, kuhusu mabadiliko yanayoweza kutatua changamoto kabla hazijatokea. Tuelewe kwamba maridhiano ya kweli yanahusu pande zote mbili. Chama tawala kukubali umuhimu wa mchango wa upinzani kwenye demokrasia yenye afya na vyama vya upinzani kuwa na mchango muhimu na kutekeleza majukumu yao professionally serikalini

Haya ndiyo maridhiano ya kweli na yenye tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla
"Vyama vya siasa kuruhusiwa kufanya Siasa"

Kwenye Moja ya paragraph Yako, kwangu ni KAULI YA UPUUZI WA HALI YA JUU, vyama vya siasa vipo kwa mujibu wa sheria, kufanya mikutano kumeruhusiwa kisheria, aliyejifanya kuweka zuio alikuwa "MSHAMBA"

Alikuwa anavunja katiba mchana kweupe.

Mstari huo kwenye paragraph hiyo umetosha kuona andiko lako limebeba UCHAFU wa kutosha.
🤔🤔🤔
 
Kwa muda mrefu Sasa, Chama cha Mapinduzi kimeongoza kwenye dira ya siasa kwa kuwa na Sera zinazo kubalika kwa wananchi na kwa ujumla kufanya vizuri katika kipindi ambacho wawakilishi wake wamekuwa madarakani. Matokeo ya kuwa na rekodi nzuri kama hii ni nzuri kwa wananchi na Chama tawala lakini ni mbaya kwa vyama vya upinzani. Mbaya kwasababu katika kipindi cha miaka kumi iliyopita ushawishi wa vyama hivi kisiasa na nafasi yao kwenye demokrasia vimepungua kwa kiasi kikubwa sana.

Elewa kwamba mifumo iliyopo imechangia kuwa na amani na utulivu hata katika kipindi ambacho vyama vya siasa vingine vinaweza kupotea kabisa. Hata kama siasa za Tanzania ni za vyama vingi, kupotea kwa vyama vya upinzani kuta halalisha siasa za chama kimoja kwa njia ambayo sio ya moja kwa moja. Vyama vya upinzani haswa CHADEMA vimezungumza sana kuhusu maridhiano, lakini je maridhiano yenye tija kwa wananchi ni maridhiano ya aina gani?

Nitatoa mfano mmoja ambao unaohusu vyama vya siasa kuruhusiwa kufanya mikutano ya hadhara. Utagundua kwamba jambo ambalo lingetakiwa kuwa zuri limetumiwa vibaya na wanasiasa haswa wa CHADEMA na ni tishio kwa amani ya taifa. Upinzani bora kwenye nchi zilizokomaa kisiasa haziko hivyo. Natoa mapendekezo yangu ya maridhiano nikiwa na imani kwamba vyama vya upinzani vitabadilika na kwamba siku moja tutakuwa na afya kwenye demokrasia yetu kwa kuwa na vyama vya siasa vinavyofanya shughuli za siasa kwenye mipaka mizuri. Vilevile vyama vya upinzani vinatakiwa kuwa na mchango chanya kwenye masuala ya nchi

Kwanza kabisa, vyama vya upinzani vinatakiwa kuwa na angalau asilimia fulani ya wawakilishi bungeni hata kama vikishindwa uchaguzi kwa asilimia kubwa. Idadi ya wawakilishi ambayo ni ndogo lakini yenye mchango mkubwa na sio kukosoa kila kitu bila kuwa na sababu za msingi ni mwanga kwenye bunge letu. Vyama vya upinzani vingetakiwa kuwa na wawakilishi Ikulu ukizingatia kwamba Ikulu ni taasisi ambayo inatakiwa iweze kupokea mabadiliko ya uongozi yoyote. Vilevile taasisi ya ushirikiano ya siasa inaweza kuundwa kama njia ya kuvishirikisha vyama vya upinzani kwenye maamuzi ya serikali. Uwakilishi kwenye kila wizara pia ni muhimu. Hivi vitakuwa na manufaa kama majukumu haya yatatumiwa vizuri

Mwisho kabisa, naomba tufikirie kuhusu vizazi vijavyo, kuhusu mabadiliko yanayoweza kutatua changamoto kabla hazijatokea. Tuelewe kwamba maridhiano ya kweli yanahusu pande zote mbili. Chama tawala kukubali umuhimu wa mchango wa upinzani kwenye demokrasia yenye afya na vyama vya upinzani kuwa na mchango muhimu na kutekeleza majukumu yao professionally serikalini

Haya ndiyo maridhiano ya kweli na yenye tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla
Marithiano ni baada ya matokeo ya uchaguzi ambao haujafanyiwa uchafuzi. Si kujifanya unatoa hisani.
 
Back
Top Bottom