Maridhiano ya Taifa yapata mwelekeo mpya, muswada maalum waandaliwa

Maridhiano ya Taifa yapata mwelekeo mpya, muswada maalum waandaliwa

Taarifa kwa UMMA Kuhusu Uandaaji wa Muswada wa Mfano (Model Bill) wa Kuongoza Mchakato wa Mazungumzo ya Maridhiano na Muafaka wa Kitaifa*

Kamati ya Kusukuma Maridhiano ya Kitaifa (KKMK) inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania, taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa, wadau wa maendeleo, vyama vya siasa, asasi za kiraia, viongozi wa dini pamoja na makundi yote ya kijamii kuwa imeanza rasmi maandalizi ya Muswada wa Mfano (Model Bill) utakaoweka mfumo wa kisheria na kiutawala wa kuendesha Mchakato wa Mazungumzo ya Maridhiano na Muafaka wa Taifa.

Hatua hii inafuatia mapendekezo yaliyotolewa na Jaji Chande kuhusu umuhimu Mazungumzo ya Maridhiano ya kitaifa na Muafaka wa Kitaifa kuponya na kuandaa Taifa kwenda kwenye mchakato wa uandikaji wa Katiba mpya.

KKMK inaamini kuwa Tanzania ina wajibu wa kuimarisha mshikamano wa kitaifa, kuendeleza misingi ya haki, usawa, maridhiano na demokrasia jumuishi kupitia mazungumzo yenye kujenga uelewano wa kitaifa na kuimarisha amani ya kudumu.

Muswada huo wa Mfano unatarajiwa:

1) Kuweka mfumo rasmi wa uendeshaji wa Mazungumzo ya Maridhiano na Muafaka wa Taifa ikiwemo Uteuzi wa Wajumbe,Ajenda za Mazungumzo, Muundo wa Tume nk

2) Kufafanua wajibu wa wadau mbalimbali katika mchakato wa maridhiano;

3) Kuweka misingi ya ushirikishwaji wa wananchi na taasisi mbalimbali;

4) Kuweka taratibu za utekelezaji wa makubaliano yatakayofikiwa;

5) Kulinda misingi ya haki, uwazi, uwajibikaji na umoja wa kitaifa.

6) Fidia kwa Waathirika

Katika kuandaa Muswada wa Mfano huo, KKMK itafanya mashauriano mapana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha kuwa maoni ya wananchi na makundi yote yanazingatiwa kikamilifu.

KKMK inatoa wito kwa Watanzania wote kushiriki kwa amani, uwazi na uzalendo katika kutoa maoni na mapendekezo yatakayosaidia kujenga Taifa lenye mshikamano, haki na maridhiano ya kudumu.

Kamati pia inapenda kusisitiza kuwa mchakato huu si wa kisiasa pekee, bali ni agenda ya kitaifa inayolenga kuimarisha umoja wa taifa, kulinda amani na kuweka msingi imara wa maendeleo endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Ratiba ya mashauriano na namna ya kuwasilisha maoni itatangazwa rasmi kupitia vyombo mbalimbali vya habari na majukwaa ya umma.

Imetolewa na:

Odero Charles Odero

Mwenyekiti Kamati Kusukuma Maridhiano ya Kitaifa (KKMK)
Hela mnapata wapi kuendesha huo mchakato wa maridhiano? Isije ikawa unatumiwa na wauaji kutaka kuja kuwasafisha. Maridhiano ni utapeli unaotumika kupumbaza watu ili viongozi waendelee kukaa madarakani kwa amani bila ridhaa ya wananchi. Kisha ukija uchaguzi mwingine uchaguzi unaporwa na kufanyika mauaji, halafu nyie madalali mnatumika tena kuitisha maridhiano.
 
watu wote wanao tea katiba ya Sasa ujue ni wanufaika wa utawala uliopo sasa
 
MARIDHIANO YA TAIFA YAPATA MWELEKEO MPYA, MUSWADA MAALUM WAANDALIWA

DAR ES SALAAM – Mchakato wa kuelekea maridhiano na muafaka wa kitaifa umeingia hatua mpya baada ya Kamati ya Kusukuma Maridhiano ya Kitaifa (KKMK) kutangaza kuanza rasmi maandalizi ya Muswada wa Mfano (Model Bill) utakaoweka mfumo wa kisheria na kiutawala wa kuendesha mazungumzo ya maridhiano nchini.

Hatua hiyo inalenga kuweka msingi wa mazungumzo yatakayosaidia kuimarisha umoja wa taifa, kurejesha uelewano miongoni mwa wadau mbalimbali na kuweka mazingira yanayodaiwa kuwa muhimu kabla ya kuanza mchakato wa uandishi wa Katiba mpya.

Katika taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa KKMK, Odero Charles Odero, kamati hiyo imesema maandalizi ya muswada huo yamechochewa na mapendekezo yaliyowahi kutolewa na Jaji Chande kuhusu umuhimu wa mazungumzo ya maridhiano kama njia ya kuponya taifa na kujenga mwafaka wa kitaifa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, muswada huo unakusudiwa kuweka mfumo rasmi wa uendeshaji wa mazungumzo, ikiwemo utaratibu wa uteuzi wa wajumbe, ajenda za mazungumzo, muundo wa tume itakayosimamia mchakato huo pamoja na majukumu ya wadau wote watakaoshiriki.

Aidha, muswada huo utaweka misingi ya ushirikishwaji wa wananchi, taasisi za umma na binafsi, vyama vya siasa, viongozi wa dini na makundi mbalimbali ya kijamii ili kuhakikisha mchakato unakuwa shirikishi na wenye uwazi.

KKMK pia imeeleza kuwa muswada huo utaweka utaratibu wa utekelezaji wa makubaliano yatakayofikiwa, kulinda misingi ya haki, uwazi, uwajibikaji na umoja wa kitaifa, pamoja na kuainisha mfumo wa fidia kwa waathirika wa migogoro au matukio yatakayohusishwa na mchakato wa maridhiano.

Kamati hiyo imesema kabla ya kukamilisha muswada huo, itafanya mashauriano mapana na wadau wa kitaifa na kimataifa ili kuhakikisha maoni ya wananchi yanajumuishwa kikamilifu.

"Tunatoa wito kwa Watanzania wote kushiriki kwa amani, uwazi na uzalendo katika kutoa maoni na mapendekezo yatakayosaidia kujenga taifa lenye mshikamano, haki na maridhiano ya kudumu," imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

KKMK imeongeza kuwa mchakato huo haupaswi kutazamwa kama ajenda ya kisiasa pekee, bali ni jukumu la kitaifa lenye lengo la kuimarisha amani, umoja na kuweka msingi imara wa maendeleo endelevu kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Kamati hiyo imesema ratiba ya mashauriano pamoja na utaratibu wa kuwasilisha maoni ya wananchi itatangazwa rasmi kupitia vyombo vya habari na majukwaa mbalimbali ya umma katika siku zijazo.
Hayo maridhianao ni kati ya nani na nani. Na wanaridhiana kuhusu nini?
 
4. MASHARTI NA MUDA MAALUMU KUTOKA COMMONWEALTH CMAG(The Ultimatum)

Kutokana na mapendekezo ya Mjumbe Maalum, CMAG imetoa maelekezo yenye ukomo wa muda (Time-bound actions) kwa Tanzania:

Ndani ya Siku 30: Kutatua suala la kushikiliwa kwa Tundu Lissu kupitia njia za kisiasa au kisheria, na kuwaachia wengine wote wanaoshikiliwa kwa kutumia haki zao kwa amani.

Ndani ya Siku 60: Kurejesha upatikanaji kamili wa mitandao ya kijamii na kuacha vitisho dhidi ya vyombo vya habari na watetezi wa uhuru wa kujieleza.

Ndani ya Siku 90: Kuitisha jukwaa shirikishi na la kuaminika la vyama vya siasa (likiongozwa na mwezeshaji huru) kujadili mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi, ushindani wa kisiasa, wafungwa, na uwajibikaji.

Bila Kuchelewa: Kuanza uchunguzi huru wa makosa ya jinai uliopendekezwa na Tume ya Uchunguzi, pamoja na fidia kwa wahanga.

MWISHO WA UBAYA NI AIBU
 
Taarifa kwa UMMA Kuhusu Uandaaji wa Muswada wa Mfano (Model Bill) wa Kuongoza Mchakato wa Mazungumzo ya Maridhiano na Muafaka wa Kitaifa*

Kamati ya Kusukuma Maridhiano ya Kitaifa (KKMK) inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania, taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa, wadau wa maendeleo, vyama vya siasa, asasi za kiraia, viongozi wa dini pamoja na makundi yote ya kijamii kuwa imeanza rasmi maandalizi ya Muswada wa Mfano (Model Bill) utakaoweka mfumo wa kisheria na kiutawala wa kuendesha Mchakato wa Mazungumzo ya Maridhiano na Muafaka wa Taifa.

Hatua hii inafuatia mapendekezo yaliyotolewa na Jaji Chande kuhusu umuhimu Mazungumzo ya Maridhiano ya kitaifa na Muafaka wa Kitaifa kuponya na kuandaa Taifa kwenda kwenye mchakato wa uandikaji wa Katiba mpya.

KKMK inaamini kuwa Tanzania ina wajibu wa kuimarisha mshikamano wa kitaifa, kuendeleza misingi ya haki, usawa, maridhiano na demokrasia jumuishi kupitia mazungumzo yenye kujenga uelewano wa kitaifa na kuimarisha amani ya kudumu.

Muswada huo wa Mfano unatarajiwa:

1) Kuweka mfumo rasmi wa uendeshaji wa Mazungumzo ya Maridhiano na Muafaka wa Taifa ikiwemo Uteuzi wa Wajumbe,Ajenda za Mazungumzo, Muundo wa Tume nk

2) Kufafanua wajibu wa wadau mbalimbali katika mchakato wa maridhiano;

3) Kuweka misingi ya ushirikishwaji wa wananchi na taasisi mbalimbali;

4) Kuweka taratibu za utekelezaji wa makubaliano yatakayofikiwa;

5) Kulinda misingi ya haki, uwazi, uwajibikaji na umoja wa kitaifa.

6) Fidia kwa Waathirika

Katika kuandaa Muswada wa Mfano huo, KKMK itafanya mashauriano mapana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha kuwa maoni ya wananchi na makundi yote yanazingatiwa kikamilifu.

KKMK inatoa wito kwa Watanzania wote kushiriki kwa amani, uwazi na uzalendo katika kutoa maoni na mapendekezo yatakayosaidia kujenga Taifa lenye mshikamano, haki na maridhiano ya kudumu.

Kamati pia inapenda kusisitiza kuwa mchakato huu si wa kisiasa pekee, bali ni agenda ya kitaifa inayolenga kuimarisha umoja wa taifa, kulinda amani na kuweka msingi imara wa maendeleo endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Ratiba ya mashauriano na namna ya kuwasilisha maoni itatangazwa rasmi kupitia vyombo mbalimbali vya habari na majukwaa ya umma.

Imetolewa na:

Odero Charles Odero

Mwenyekiti Kamati Kusukuma Maridhiano ya Kitaifa (KKMK)

Hamtafanikiwa kwa haya . Bila kuweka mpatanishi wa kimataifa hamtafanikiwa. Lakini hamtafanikiwa kwasababu Mama Samia anahadaa hataki maridhiano tumeshaona Chadema
 
Back
Top Bottom