Maridhiano ya Taifa yapata mwelekeo mpya, muswada maalum waandaliwa

Maridhiano ya Taifa yapata mwelekeo mpya, muswada maalum waandaliwa

Taarifa kwa UMMA Kuhusu Uandaaji wa Muswada wa Mfano (Model Bill) wa Kuongoza Mchakato wa Mazungumzo ya Maridhiano na Muafaka wa Kitaifa*

Kamati ya Kusukuma Maridhiano ya Kitaifa (KKMK) inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania, taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa, wadau wa maendeleo, vyama vya siasa, asasi za kiraia, viongozi wa dini pamoja na makundi yote ya kijamii kuwa imeanza rasmi maandalizi ya Muswada wa Mfano (Model Bill) utakaoweka mfumo wa kisheria na kiutawala wa kuendesha Mchakato wa Mazungumzo ya Maridhiano na Muafaka wa Taifa.

Hatua hii inafuatia mapendekezo yaliyotolewa na Jaji Chande kuhusu umuhimu Mazungumzo ya Maridhiano ya kitaifa na Muafaka wa Kitaifa kuponya na kuandaa Taifa kwenda kwenye mchakato wa uandikaji wa Katiba mpya.

KKMK inaamini kuwa Tanzania ina wajibu wa kuimarisha mshikamano wa kitaifa, kuendeleza misingi ya haki, usawa, maridhiano na demokrasia jumuishi kupitia mazungumzo yenye kujenga uelewano wa kitaifa na kuimarisha amani ya kudumu.

Muswada huo wa Mfano unatarajiwa:

1) Kuweka mfumo rasmi wa uendeshaji wa Mazungumzo ya Maridhiano na Muafaka wa Taifa ikiwemo Uteuzi wa Wajumbe,Ajenda za Mazungumzo, Muundo wa Tume nk

2) Kufafanua wajibu wa wadau mbalimbali katika mchakato wa maridhiano;

3) Kuweka misingi ya ushirikishwaji wa wananchi na taasisi mbalimbali;

4) Kuweka taratibu za utekelezaji wa makubaliano yatakayofikiwa;

5) Kulinda misingi ya haki, uwazi, uwajibikaji na umoja wa kitaifa.

6) Fidia kwa Waathirika

Katika kuandaa Muswada wa Mfano huo, KKMK itafanya mashauriano mapana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha kuwa maoni ya wananchi na makundi yote yanazingatiwa kikamilifu.

KKMK inatoa wito kwa Watanzania wote kushiriki kwa amani, uwazi na uzalendo katika kutoa maoni na mapendekezo yatakayosaidia kujenga Taifa lenye mshikamano, haki na maridhiano ya kudumu.

Kamati pia inapenda kusisitiza kuwa mchakato huu si wa kisiasa pekee, bali ni agenda ya kitaifa inayolenga kuimarisha umoja wa taifa, kulinda amani na kuweka msingi imara wa maendeleo endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Ratiba ya mashauriano na namna ya kuwasilisha maoni itatangazwa rasmi kupitia vyombo mbalimbali vya habari na majukwaa ya umma.

Imetolewa na:

Odero Charles Odero

Mwenyekiti Kamati Kusukuma Maridhiano ya Kitaifa (KKMK)

Mnashangaza sana, hamueleweki kabisa.

Mnaimba nyimbo zinazopingana kwa wakati mmoja, yaani mnaimba maridhiano wakati huo huo mnaimba ugaidi kwa kuwakamata, kuweteka, kuwatesa na kuwauwa wananchi.

Chagueni moja tu ili mueleweke mnachotaka. Kama ni kuteka na kuuwa wananchi na kuwabambikia wengine kesi za ugaidi muendelee tu kuliko kuleta hadaa.

Mnaichezea nchi yetu mnavyotaka kwa kujiundia vikundi vya upigaji wa rasilimali zetu kwa kuleta hadaa ya maridhiano wakati bado mnawaumiza watu kwa utekaji na kubambikiza kesi za ugaidi.

Endeleeni kututesa na kutukejeli lakini mkumbuke kuna muda utafika ambapo ukweli na haki vitasimama na kutamalaki kwenye taifa letu, na hii ni hakika.

Acheni uonevu na hadaa, muwe wakweli kwa nafsi zenu, msifanye au msiongee tu kwa sababu mmejilipa na kushiba kodi zetu.
 
Hiyo kamati ya waganga haina mamlaka ya kutunga muswada wowote, kafanyeni maridhiano na waliouwawa oktoba 29
 
Ayo maridhiano yatarudisha Mzee ally Kibao na Baloz Polepole? Kama yakifanyka hao wakarudi kabla ya October 29 waliouwa sina tatizo na ayo maridhiano.
 
Back
Top Bottom