Marination nzuri kwa nyama choma mbuzi, ng'ombe au kuku

Marination nzuri kwa nyama choma mbuzi, ng'ombe au kuku

emmarki

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2012
Posts
1,001
Reaction score
1,430
Kwenu wataalamu wa kuchoma nyama za aina zote.

Naomba tips za kibabe kuhusu namna ya kumarinate nyama kabla ya kuichoma na baada. Viungo gani vitumike, kiasi gani, balancing ya moto haswa kwenye jiko la mkaa iweje.
 
Naomba kueleza nachojua,tumia Tangawizi,kitunguu swaumu,limau,ajina moto,soy sauce,majani ya giligiliani na pilipili manga ya unga......baadae njoo unishukuru.
ajina moto ni kiungo au typing error, hivyo vingine nipe namna ya kuvitumia
 
Naomba kueleza nachojua,tumia Tangawizi,kitunguu swaumu,limau,ajina moto,soy sauce,majani ya giligiliani na pilipili manga ya unga......baadae njoo unishukuru.
Unaweka kwa kiasi gani kwa nyama ya wingi kiasi kipi?
 
Unaweka kwa kiasi gani kwa nyama ya wingi kiasi kipi?
kwa kuanzia tu,limao weka nusu,tangawizi saga na swaunu upate kijiko kimoja cha chakula inatosha,ajina moto weka nusu kijiko cha chai,pilipili manga weka kiduchu sana,nyunyuzia tu kwa vidole juu juu,unga wa giligiliani hivyo hivyo,soy sauce weka vijiko viwili vya chakula......hio inatosha kwa nyama kilo moja,changanya alafu acha mpaka nusu saa...chumvi kadiria upendavyo.
 
ndo ile unakuta muuza supu mahali fulani wateja wanajaa unajiuliza anatumia ndumba kumbe viungo
Chimvi chumvi ya mwarabu hiyo!!ni balaa ikiwekwa kwenye supu ladha yake sio mchezo!!!mimi supu bila hiyo kitu siwezi kabisa kuita nimekunywa supu!
 
Chimvi chumvi ya mwarabu hiyo!!ni balaa ikiwekwa kwenye supu ladha yake sio mchezo!!!mimi supu bila hiyo kitu siwezi kabisa kuita nimekunywa supu!!
supu yako huwa unaandaa mwenyewe au kwa wauza supu. kama unaandaa mwenyewe kuna siri gani unayotumia mpk uufurahie ubora wa pishi la supu yako
 
supu yako huwa unaandaa mwenyewe au kwa wauza supu. kama unaandaa mwenyewe kuna siri gani unayotumia mpk uufurahie ubora wa pishi la supu yako
Mala nyingi huwa nakunywa supu kwenye migahawa,/bar ambayo wanajua kuandaa, na kuitia ajina moto!! Hata kama labda nimeandaa mwenyewe, nikitia, hoho, karoti na kumalizia hiyo ajina moto, tayari ile ladha ninayoihitaji naipata!!kama ukiiweka huna ulazima wa kuweka maviungo mengi...
 
Nahitaji...
Red wine 1/2 glass
Kuku mzima 1 wa kienyeji
Kitunguu saumu kimoja
Tangawizi 1
Ajina Moto
Pili pili manga.
Binzari nyembamba


Blend kitunguu saumu na tangawizi binzari nyembamba...

NB...Mkiwa masela watupu mnaojiweza kwenye nyama ya ng'ombe tunatumia Whiskey Kama grants inapendeza sana....

Osha vizuri kuku yako Weka kwenye huo mchanganyiko Weka chumvi kiasi usiweke nyingi Sababu utaweka ajina Mot😵ngeza red wine Kama vile Altar au Dompo nusu glass...Weka kwenye fridge kwa nusu saa...
Ukitoka Weka jikoni nyunyuzia unga wa pilipili manga kiasi.

Kata ndimu ya Tunda pembeni...save kuku yako na marshed potatoes,chipsi au ndizi mzuzu.
 
Back
Top Bottom