OFISI ya Rais (Ikulu), imesema imeshtushwa na kushangazwa na katuni iliyochorwa katika gazeti la Kenya la Sunday Nation la Jumapili iliyopita inayomuonyesha Rais Jakaya Kikwete akilambwa viatu na waandishi wa vyombo vya habari hapa nchini.
Akizungumza na Tanzania Daima kwa simu jana, Mwandishi Msaidizi wa Habari wa Rais, Maura Mwingira alisema Ikulu imeiona picha hiyo na kuichukulia kuwa ni dhihaka mbaya kwa Rais Kikwete na kwa vyombo vya habari hapa nchini.
...
Alisema pamoja na wao (Ikulu) kukaa kimya, ana imani kwamba, vyombo vya habari hapa nchini, vina wajibu wa kutokaa kimya katika hili kwani, katuni hiyo nayo inaonyesha kwamba waandishi wa habari wanamlamba Rais Kikwete viatu, jambo alilolielezea kuwa ni udhalilishaji wa taaluma ya uandishi.