Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Muda mfupi uliopita Urusi imesema jiji la bandari na viwanda la Mariupol limeingia mikononi mwao kikamilifu baada ya kusafisha mabaki ya askari wa Ukraine waliokataa kujisalimisha waliokuwa wamejichimbia kwenye kiwanda kikubwa cha kufua chuma.
Askari hao pamoja na kuishiwa chakula na silaha walikuwa na uzalendo mkubwa na nchi yao na kwa kutiwa moyo na viongozi wao waliendelea kuleta upinzani mkali kwa jeshi la Urusi mpaka pale waliporushiwa makombora mazito mfululizo yaliyowafikia walipojificha na kukigeuza kiwanda hicho kuwa majivu kama ilivyothibitishwa na Reuters.
Mafanikio hayo makubwa ya Urusi yameitikisa Ukraine yote na kupelekea nchi hiyo kutoa tangazo la kusitisha kusafirisha kwenda nje ya nchi nafaka na vyakula vyote. Maelfu ya tani ya nafaka yalikuwa yamekwama kwenye bandari ya Mariupol hivyo kauifanya Ukraine kujaribu kusafirisha nafaka kibiashara kupitia kaskazini ya nchi hiyo kabla ya kutolewa tangazo la katazo hilo.
Jiji zuri la Kyiv nalo linaendelea kuwaka moto.