Marriage is an outdated concept

Hao watoto ni kwa faida ya nani kwanza tuanzie hapo
 
Tunarudi kule kule lazima mke akae nyumbani ili mambo yaende sababu hata yeye ukitengana nae ukamuacha na watoto, still akitoka atataka mwanamke mwenzake (house girl) abakie nyumbani kutazama watoto, why kwann asiweke mwanaume atazame watoto, sababu anajua ukweli kuwa mwanaume hakaagi nyumbani kutazama watoto.
 
1. Siwezi kusoma nikiwa ndani ya ndoa

2.Ndoa ni muhimu lakini sio lazima
Ukitaka kuamini sio lazima 'Twende makaburini ukanioneshe kaburi la mwanamke aliyekua hajaolewa'

3. Ndoa ni faida ya wote, kabla ya kuingia kuna maandalizi kwa mwanaume na mwanamke
Ndio maana unaweza kumuuliza mwanaume utaoa lini anakujibu 'nikijipanga' (Mimi sijajipanga bado!!!!)

4.Mwanaume unatakiwa uoe ukiwa unaweza kujimudu wewe mwenyewe kiuchumi na akili.
Ndoa ni ya wanaume na sio wavulana.

5.Sijui stress za wanawake wengine,
Najua stress zangu ambazo ni masomo.

6.Kitu cha lazima ni kile ukikosa utaumwa au kufa mfano; Uhai, Chakula, afya njema
Cha muhimu ni kile kinachoongeza faida lakini ukikosa hupati madhara mfano; kumiliki gari, kua na ndoa.

7. Kuingiliwa ni jambo la muhimu ila sio lazima, Nikiamua hakuna wa kunizuia.

8. Mipango yangu ina faida kwangu kwa 100% mafanikio yangu yatamnufaisha yeye baadae.... Ndoa inahitaji kupewa muda
Muda wangu hautoshi kumpikia, kumfulia, kuzaa na mtoto wa mtu kwasasa.
 
Tafuta ajira kwanza
 
1. Na hicho ndicho nilichokuwa nakisema kwamba wanaume hamjui mnachotaka, sasa mnapotaka wanawake wajitunze mlikuwa mnafikiri mtapata wapi wanawake wa kufanya nao ngono kabla ya ndoa, hiyo inamaanisha kwamba na ninyi mtatakiwa mjitunze ili mkutane kwenye ndoa mkiwa wote mmejitunza na kama mnaona ngumu hamuwezi basi msiwalaumu wanawake

2. Hapo nafikiri hujanielewa sijasema kwamba wanawake kukubali hovyo ndio hawana makosa bali nilichosema ni wote mna makosa, ila ninawashangaa wanaume kujitoa na kujiona mko innocent hamna makosa kwa kisingizio kwamba jinsia yenu inawabeba kwahiyo kwenu ni sahihi tu kuendelea kuwahadaa wanawake, ila wanawake ndio wajinga kukubali eti kisa wao ndio wanaodharaulika kwenye jamii what kind of cockamamie logic is this

3. Wakati mwingine wanawake huwa ni victims tu wa uongo wenu kwa sababu wenyewe huwa mnakiri kwamba, mara nyingi mnawaingia wanawake kwa gia ya kuwaoa sababu mnajua ni kitu ambacho wengi wanakitamani, na kweli mwanamke anakubali anajua anaenda kuolewa kumbe wewe lengo lako lilikuwa kula na kusepa tu sasa hapo kwanini umlaumu mwanamke mind you wanawake siyo malaika mkuu

4. Enzi za bibi zetu angalau babu zetu walipokuwa wakiwatongoza bibi zetu kisha wakaambiwa wakapose kwanza walikuwa wanakubali kama wamependa kweli lakini je hawa wanaume wa leo wanakubali, wewe mwenyewe shahidi sema tu ukweli leo hii mwanaume yeyote ukimuambia aende kujitambulisha tu achilia mbali kuposa kisha ndio ale mzigo anakuambia hawezi kuuziwa mbuzi kwenye gunia, yani dunia ya leo mwanamke kubania mzigo siyo tena ticket ya kuolewa kama zamani kwahiyo wanawake nao wanakata tamaa wanaamua kutoa tu na hapo sasa ndipo wanapokutana na mafisi waliojificha kwenye kivuli cha waoaji wazee wa kula na kusepa

5. Mkuu ni kweli kwamba siku hizi wanawake wengi wa umri huo wanatakaa kuolewa kwa sababu za kimasomo na kujiona hawako tayari kwa ajili ya ndoa, lakini kama mtu anajiona hayuko tayari kwa ajili ya ndoa kwanini umlazimishe huoni kama anakuwa amekusaidia kuliko kukudanganya kuwa anafaa kuwa mke halafu mkifika ndoani akionesha tabia zake halisi uanze kulalamika tena kwamba amefungua makucha yake, lakini pia jambo lingine nimegundua wanawake wa umri huo wanaokataa kuolewa na vijana wa rika lao sababu siyo kutokuwa na pesa au mali tu bali vijana wa umri huo pia wameshaonekana kuwa bado hawajatulia bado damu inachemka hawawezi kutulia na mwanamke mmoja wengi wanaoa lakini michepuko kama yote sasa sidhani kama kuna mwanamke atakuwa tayari kwa hilo labda awe desperate na mwenye low self esteem
 
U
Umeandika vizuri sana na ukweli mtupu .

Ndoa kwa sasa wanawake wote hata wa vijijini wanaingia kama ajira ili baadae kupitia udhaifu wa sheris na ujinga wa wanaume wavune mali ambazo hawakuzitolea jasho hata kama ni muajiriwa. Wanaume wengi wamekubali upumbavu wa kuruhusu mke asichangie gharama za uendeshaji fanilia wakati ana kipato, lakini baadae anadai tena mgawanyo wa mali ambayo kwanza hakuichuma lakini pia hata chakula tu alikuwa hachangii. Hoja inayotumiwa kuwa alikuwa anampikia chakula ni mufilisi sababu mume naye alikuwa ananunua hicho chakula lakini pia licha ya mume kununua chakula ni ukweli kuwa chakula hicho kinapikwa na housegirl kwa sababu mke anashinda kazini na kusafiri kikazi.

Starting point kwa mume anayejitambua ni kumbana na kumlazimisha mke kama anafanya kazi/biashara achangie gharama za chakula kwa uwiano wa kipato chake au pasu kwa pasu kama kipato chake ni sawa au kikubwa kuliko cha mume. Gharama za maendeleo kama ujenzi au gari kila mtu afanye kivyake bila kuchangishana ila mnaweza kutumia pamoja mfano nyumba mnaweza ishi ingawa ni mali ya mmoja wenu.

Kama hukumbana tangu mwanzo wa ndoa na ukakubali kuishi kwa kunyonywa basi kwa mke ni ushindi wa kwanza na huko mbeleni lazima atang'ang'ania mali zako tena waume wengine wanadhulumiwa mali zote sio tena 50 kwa 50..
 
@Jadda njoo usome hapa, mtu anataka kuoa anajibiwa "bado nipo nipo kwanza". Sasa kwann nisimtafutie ela ya simu mpya, saloon na kitimoto ili anipe hata nafasi ya kumkula tu kisha nitemane nae.
Si unaona sasa na hapo ndipo tatizo lilipo hapo ambapo wanaume hamtaki kukubali kwamba mna makosa kwahiyo wewe suala la kutaka kula na kusepa kisa kakataa kuolewa na wewe unajiona uko sawa, huwa nashindwa kuelewa kwanini wanaume you never take no for an answer when it comes to approaching women sijui kwanini huwa mnahisi mna haki ya kukubaliwa tu na mwanamke yeyote yule mnayetongoza na mkikataliwa basi inakuwa ni uadui na visasi where do you get this sense of entitlement from, kama mtu amekataa kuolewa na wewe kuna ulazima gani wa kuzini naye si umuache uendelee kutafuta yule ambaye atakuwa tayari kuolewa na wewe kisha umuoe na kama mnaona hilo ni gumu hamuwezi sasa hizi lawama na matusi kwa wanawake vinatoka wapi wakati ninyi ndio mnafanya kila namna ili muwashawishi wanawake wasiowapenda kwa kutumia udhaifu wao to fall into your trap..pathetic!!
 
Bora mtu usiolewe kuliko kukubali kuolewa na yeyote muhimu anapumua.
Kwenda kuishi ndoa ya mateso kwanini???

Wanaopapatikia kuolewa na yeyote umri ukienda wengi wao ni wale waliofail maisha!

Wanatafuta msaada ni wapi wataenda kuolewa ili wale chakula cha Bure!
 
Swadakta mkuu
 
Uko vizuri katika vita ya kisaikolojia! 😂😂

Masikini binti ambaye hajajengwa vizuri kisaikolojia akisoma hapa anatetereka anaenda kuolewa na “chochote” kinachokuja mbele yake 🤣

Kwa ndoa gani? Hizi tunazoziona mtaani au? Wana JF Yawezekana mna kamtaa chenu mnaishi ambapo mimi sijawahi kufika.

Wewe ungekuwa na binti wa miaka 20 sasa ungemshauri nini? Be practical please.
 
Yani ukisema hivi wanaume wanakuambia eti oo ngoja ukifika umri fulani bila ndoa au ukiwa single mother utatafuta mwanaume yeyote tu mradi anapumua, sijui wao wanaume wanawachukuliaje ila binafsi wanawake wa aina hiyo huwa nawachukulia kama walio desperate na wenye low self esteem tu mwanamke anayejitambua hawezi kukubali kuolewa na mwanaume yeyote ili mradi tu anapumua no matter the circumstances, wanaume nao wanatakiwa kujua kwamba siyo sifa wala raha mwanamke kufikia hatua hiyo bali inaonesha jinsi gani kwenye dunia ya leo wanawake wanawachukulia wanaume kwamba ni kimbilio pale tu wanapokuwa na matatizo na wameshachoka na si vinginevyo
 
Hili andiko lipo makini sana. Truth be told, wanaume hautupendi kukataliwa for sure. Tujifunze kukubaliana na hali if someone is not interested let them go. Matatizo ya ndoa mengi hanzia pale relationship inapokua mbich ukiona your partner is tolerating you, au it's like una invest nguvu nying kuliko yeye jua tayar ukuta una nyufa it's a matter of time ndoa itavunjika. Na hii concept ya ndoa is an outdated thing sio valid, tatizo sio ndoa tatizo ni wanandoa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…