Okay, nina maswali kwako?
1. Nini kitatokea kama wanawake watagomea wanaume kulala nao hadi tu pale watakapojicommit kwa familia zao kwa kuja na wazazi wao kutoa posa na kuoa kihalali, je wanaume wakikutana na huo utaratibu watapata vipi mwanamke wa kufanya nae mahusiano ya kingono nje ya ndoa?
2. So katika haya maelezo yako yote umefanya assumption kuwa mwanamke hana akili wala ufahamu wa kutambua umuhimu wa bikra yake mwenyewe katika kuanza maisha na mwanaume, why aiweke rehani akijua thamani yake, so wanawake hajui thamani ya bikra?
3. Kama una assume wanawake hawajui thamani ya Bikra then nikuulize je ni sahihi pia kwa mwanaume kutojua wajibu wa kujali na kumtunza mke wake atakae muoa? Kama umeweza kumpa mwanamke pass ya kutothamini kitu kinachompa thamani muhimu kama mke wa mtu then automatically unaopia uhalali wa kuassume ni sahihi kwa wanaume wote kupewa pass au kukaushiwa kama wanafeli majukumu yao kwa makusudi, si ndio?
4. Umezungumzia swala la wanaume kutongoza mabinti kama ndio sababu ya mabinti wa kisasa kutokuwa na bikra na kutozitunza, nikuulize mama zetu na bibi zetu unadhani walikuwa hawatongozwi miaka hiyo, haukusikia story zao wakihadithia namna waliwakwepa babu zetu kwa sharti kuwa wakapose kwanza makwao ndipo mengine yataendelea haujawahi sikia hizo story, je swali langu kwako, unahisi ni wanaume wameshusha standards zao kama wanaume au ni wanawake wameacha kusimamia misimamo itakayolinda utu wao kwa wanaume na kuwaandaa kuheshimiwa katika ndoa kama wanawake wanaolinda miili yao?
5. Unajua kwamba kwa wastani miaka hii binti wa kisasa kati ya umri wa miaka 16 hadi 25 huwa ndoa kwake ni kosa, yaani ukimwambia nataka nikuoe na ukiwa tayari kwa kufanya hilo jambo basi atakukataa kwasababu mbali mbali kama kujiona bado mtoto kwa ndoa, shinikizo la wazazi kuwa asome kwanza mahusiano ni baadae, ulimbukeni wa uhuru wa kujiachia umri wa usichana ili watumike kwanza sababu soko la ngono linawaita sana, wanaume wa rika lao wanakuwa bado hawana pesa na mali hivyo kuolewa nao ni kujifunga na maisha ya usichana na kupitwa na fursa nyingi za kujipatia mali.
Je, swali langu, ni nani huwa anamkataa mwenzake katika umri wa miaka 16 hadi 25 kati ya binti ambaye ndio anachanua au kijana ambae bado ndio anajitafuta anauwezo wa kumudu vitu vidogo sana ila maisha ya kuishi pamoja na mke anaweza kujikongoja ,tuongee ukweli, Mwanamke katika umri huo masharti yake ili umuoe uishi nae kama mke na tamaa yake ya kuolewa huwa inakuwa sawa sawa na akifika kuanzia miaka 28 hadi 30+ huko? [emoji848][emoji848][emoji848]