Marriage is an outdated concept

Marriage is an outdated concept

Una uhakika kuwa hajawaambia??

Hili ni suala la kijamii,halihusu baba,mama wala dada,linawahusu wanajamii wote,hao dada zake na shangazi zake yeye hawezi kuwaoa.

Hivyo ana haki ya kuwasilisha jambo hili kwenye jamii ili jamii ijifunze.
Achana nao hao hawana hoja. Wanajaribu kufanya bullying kwenye weak spot. Wakijua wakileta ndugu zangu kwenye mjadala itanichoma moyo
 
Hata kama ni makubaliano kama hayupo fair basi yanatakiwa kupitiwa na yawekewe utaratibu ambao haumkandamizi yoyote kumbuka kuna wengine wagumu kuelewa au ni mpaka wapigwe na kitu kizito ndio wanashtuka. moyo wa mtu ni kichaka anaweza kuwa mwema kwako kumbe lengo lake ni mali baada ya kupata cheti cha ndoa hapo ndio heka heka zitaanza kwaiyo suala sio makubaliano tu suala ni kwamba hayo makubaliano yapo fair? hayo makubaliano yakivunjika kila upande utakua satified?

Kama mwanaume alikushinikiza kuacha kazi/ biashara au una msaada wa kiuchumi katika mali zilizozalishwa kwenye ndoa (mfano umechangia mtaji au ujuzi wako wankitaaluma) hapo una haki ya kupata percent yako lakini kama mwanamke alikukuta tayari ushajipata na hana mchango wa moja moja kwenye mishe za mwanaume basi uyo hana haki ya kupata mgao.
Mbona ndio ilivyo? Kuwa ukioa na mali zako unazo basi hazimuhusu muolewa katika mgao.

Ondoa neno shinikiza weka kubaliana, Ukisema kila kitu kiwekewe sheria unajua ni wapi unaelekea?

Ndoa ni kwaajili ya watu watu wazima wawili waliokubalina kuoana. Tupewe sheria na ya kunanilii basi! 😂
 
Mdogo wangu hiki kitu kinakuzwa kuliko uhalisia, hizi ndoa tunazoziona mtaani ziko na diversity kwa kiasi kikubwa, Hivi mfano mwanaume kutoa hela kwaajili ya chakula cha familia ni kumuhudumia mwanamke??

Hivi we unaamini kuwa kuna wanawake wanafanya kazi wana familia na watoto na wana waume zao na hela zao hazihusiki kwenye kutunza familia? Ingekuwa hivyo wanawake tungetajirika basi.

Mimi ntakuwa mtu wa mwisho kuamini hili.
Mbona karibia wote ni hivyo. Ukitafiti utajua. Mwanamke anapata pesa akitumia mwanaume atajulishwa na itabidi amrejeshee kama deni au mkopo.

Ila pia wanawake huwa wana matumizi yao ambayo ndio pesa yao wanayofuta huwa inakwenda huko.
 
Nadhani unayo hoja ya msingi kabisa. Ila kukufumbua macho zaidi ni vema ukafahamu kuwa ndoa haijawai wala haitawahi kuja kuwa outdated concept bali shida ni wahusika wanaoingia ndani ya ndoa kutokuwa na vigezo au uwezo wa kusimama ndani ya ndoa.

Kuna sababu ambazo kimsingi zinasababisha ndoa katika kizazi cha sasa kuwa kazi kubwa kuitumikia, na sababu zenyewe ni kama ifuatavyo:

1. Ndoa ni taasisi, na kila taasisi ndani yake ina watendaji wenye vigezo na uwezo wa kuitumikia. Huwezi kuajiri askari jeshi bila mafunzo ya jeshi. Huwezi ajiri muhasibu bila kufuzu mafunzo ya chuo na CPA, huwezi ajiri mkemia bila kuwa na cheti cha mkemia, je kwenye ndoa, hawa mabinti wa kisasa na vijana ni wapi hukaa kambi hata ya mwaka m'moja kupitia mafunzo makali ya ndoa?

2. Wanaume wameshusha sana standards zao kwa wanawake na wanawake wamepandisha sana standards zao kwa wanaume. Mwanamke zamani aliqualify kuwa mke kwa kuwa bikra kama sifa ya lazima, halafu tabia nzuri ikawekwa kama sifa inayofuata ya lazima.

Leo hii wanaume hii sifa hamuhangaiki nayo tena wanaume wengine wanatetea kabisa kwa kusema kwan kuna ubaya gani akiwa hana bikra, hawa ni wanaume wanaotetea si wanawake, sasa kwann wanawake wasikubaliane na huo uhalisia kuwa wanaume hawana shida na bikra watatuoa hata wakikuta tulishazaa na wanaume kwahiyo wacha tukachezewe kuna mabwege yatatulipia mahari na kutuoa.

3. Wanaume miaka hii wamekuwa wakwepa majukumu au wabeba majukumu yasiyowahusu. Mwanaume anazaa na binti ila hajui wajibu wake kama Mume na baba, hajui majukumu yake kwa kitu alichokianzisha mwenyewe anatoa toa macho kama ng'ombe na kusubiria wakwe, mashemeji, na familia yake wafanye jambo kumsaidia. Au anakutana na mwanamke ambaye sio wake ana watoto yeye huyo kabebelea, ni wa kwako? Kwann usitafute wa kwako? Hiyo roho nzuri si ungelea watoto wa dungu zako wenye hali ngumu, kwenda kulea mabao ya watu halafu ndio uitwe mwanaume wa shoka ni ujinga kutoka sayari gani huo? [emoji848] Kwa sampuli hii ya wanaume ndoa haiwezi kuwa imara.

4. Kudharau mafunzo ya kimaadili na Maagizo ya mwenyezi MUNGU ambayo kaagiza watu kuyafuata ili kuwa imara kiimani na kimwili ila viburi sasa vya wanadamu leo ndio matokeo yake tupo hapa ndoa zinaendeshwa kwa idea za movies za Hollywood, tamthiria za Telemundo, na hawa relationship coaches wa mitandaoni.

5. Wanawake wa sasa ni wavivu eneo la ndoa ila wanabidii kujihangaikia. Mwanamke unaweza mkuta alikuwa amepanga analipa Kodi kwa biashara ndogo ndogo au ameajiriwa lakini siku ukianza kaa nae ndani hatochangia hata 1000 endapo kutakuwa na dharula na mwanaume haupo karibu au haupo na vema kiuchumi kwa kukwambia wewe ni mwanaume as if yeye ndie huwa analipa 100% ya bills. Kwa kifupi ubinafsi.

So kimsingi Ndoa haijawai na haitakuja kuwa outdated concept shida ni wahusika kutokutambua na kusimamia vigezo vya ndoa na kuisimamia vilivyo kwa kila mojawapo kukaa eneo lake na si kuingiliana.
Mkuu matatizo binafsi yapo kila upande na pale mnaposhindwana basi mnaachana tu tatizo linakuja utaratibu upoje baada ya kuachana? Hapo ndipo unaona sheria ya ndoa ipo outdate kumbuka hapa sipingi mahusiano ya kimapenzi baina ya mwanamke na mwanaume ambacho sikubaliano nacho ni ule mkataba wa ndoa mnaotakiwa kuusaini. Mnapoingia kwenye ndoa mara zote thamani ya mwanaume kiuchumi inakua juu kuzidi thamani ya mwanamke kwaiyo automaticaly mwanaume atakua na mchango mkubwa kiuchumi sasa kwann mali zigawanywe. Wewe uza range rover yako mimi nauza bajaji yangu halafu tuchanganye hela za mauzo tugawane pasukl kwa pasu je utakubali?
 
Mbona karibia wote ni hivyo. Ukitafiti utajua. Mwanamke anapata pesa akitumia mwanaume atajulishwa na itabidi amrejeshee kama deni au mkopo.

Ila pia wanawake huwa wana matumizi yao ambayo ndio pesa yao wanayofuta huwa inakwenda huko.
Na ninyi waume zao mnafurahia hilo suala?

Kwahiyo umeona tatizo lilipo?
 
Mbona ndio ilivyo? Kuwa ukioa na mali zako unazo basi hazimuhusu muolewa katika mgao.

Ondoa neno shinikiza weka kubaliana, Ukisema kila kitu kiwekewe sheria unajua ni wapi unaelekea?

Ndoa ni kwaajili ya watu watu wazima wawili waliokubalina kuoana. Tupewe sheria na ya kunanilii basi! 😂
Suala sio makubaliano suala ni usawa katika hayo makubaliano. Baada ya ndoa kuvunjika kila mmoja achukue mali ambayo ina jina lake kama mmiliki yaani umemkuta mtu tayari ashajiwekea misingi ya kukua kiuchumi halafu uko mbeleni mali zigawanywe sio sawa.
 
Ndoa
_____

Sio kila mwanaume anaweza kuoa na sio kila mwanamke anaweza kuolewa"....marriage is not for everyone" kwani si kila anayeonekana mwanaume ni mwanaume & mwanamke ni mwanamke .. nisiingie in details.



..kuoa/kuolewa na kuishi kwenye ndoa yenye amani ni ndoto ya kila mwanaume na mwanamke anayejitambua na anayejua anataka nini hapa duniani.

Wanaume tunapoowa hatutakiwi kufikiria kuachana na vijimali vyetu vya hapa na pale ......hiyo ni ajali km ajali nyingine, haina kinga...ni km unaponunua gari hautakiwi kufikiri kuhusu ajali na kusema "kataa kumiliki gari".
 
Back
Top Bottom