Marriage is an outdated concept

Marriage is an outdated concept

Mkuu hapo kwenye point yako namba mbili nafikiri umesahau kitu kimoja tu, hiyo zamani wakati sifa za mwanamke kuolewa zilikuwa ni bikira na tabia njema zilikuwa ni enzi ambazo wanaume hawatongozi wanawake hovyo ili wapunguze tu upwiru, bali mwanaume alikuwa akimpenda mwanamke anaenda direct kwao kumchumbia na kumtolea mahari kisha anapewa mke wanaanza maisha ya ndoa

Lakini kwa hii dunia ya leo ambayo watu wamefanya ngono kama chakula mahusiano yanajengwa based on one night stand, friends with benefit, kufurahishana, kulana kimasihara, na upumbavu mwingine kama huo, watu wanajifanyia tu sex halafu mwisho wa siku mwanaume akitaka kuoa, aje aseme eti anataka bikira na tabia njema huyo atakuwa mzima kweli kichwani

Na mbaya zaidi ukisema jinsia zote zibadilike wanaume wanakuambia eti wanaotakiwa kubadilika ni wanawake ndio waache kukubali wakitongozwa, ila wao wanaume wanaona ni haki yao kutongoza wanawake hata wasio na malengo nao kwa gia ya kwamba watawaoa kumbe lengo lao ni kupunguza haja zao tu, yani eti wao kuwahadaa wanawake wanajiona wako sawa na wanafaa kuwa waume ila wanawake kuwakubalia wanaonekana wana matatizo na hawafai kuwa wake

Yani mtu urukeruke huku na huko ufanye umalaya uchezee na uharibu wanawake to your heart's content halafu ukitaka kuoa, ndio uje ujifanye unawalalamikia na kuwatukana wanawake kuwa hawajitunzi na hawajiheshimu kana kwamba siyo wewe uliyeshiriki kwenye kuwaharibu na kuwachezea, huku ukidhani kwamba jinsia yako itakubeba kwa kuwa unajua kwamba siku zote wanaodhalilishwa kuhusu suala la ngono ni wanawake kwa sana

Mimi ninachoweza kusema ni kwamba hao wanaume walioamua kushusha standards siyo kwamba ni wapumbavu ila wameamua kuacha kuwa delusional na kukubaliana na hali halisi, kwamba huwezi kuzini na wanawake halafu ukitaka kuoa uanze kutafuta mabikira katika hao hao wanawake ambao ulikuwa unazini nao sasa hao mabikira watoke wapi, huwezi kuyachafua mazingira halafu utegemee yakupe hewa safi lazima uchague moja ni either uyatunze mazingira ili yakupe hewa safi au uyachafue kisha uikubali hewa chafu yatakayokupa

Yani wanaume mnatakiwa muelewe kwamba kujitunza is not about nani anaonekana malaya na anadharaulika na jamii kati ya hizi jinsia mbili bali it's all about kupata mwenza bora wa maisha, maana hapa tulipofikia wanawake hawajali tena na wameshaanza kuzipuuzia hizo gender stereotypes na ndio kwanza wanazidisha maovu na huko tunakoelekea ndio kubaya zaidi, so it's up to you wanaume kuamua either mbadilike muache kuchezea na kuharibu wanawake au muendelee halafu mwisho wa siku mje kuoa hao hao maana ndio ambao wapo wala msidhani mtashushiwa hao mabikira mnaowataka

Ni kwa sababu imeshaonekana kwamba wenye shida na hizo bikira na tabia njema kutoka kwa wanawake ni ninyi na siyo wao wenyewe so ninyi kama ninyi mnafanya jitihada gani ili mfike nao wakiwa na hizo sifa hadi kwenye umri wa ndoa, kama bado mtaendelea kushindana nao kwamba wao ndio wajitunze kwa visingizio vya kipumbavu eti maumbile sijui nini basi msitegemee lolote na wala msiwalaumu pale ambapo mnataka kuoa bali mkubali tu kushusha vigezo vyenu na kuvuna mlichokipanda, tangu jamii imeanza kuwatukana wanawake matusi na kuwaita majina yote mabaya kama wanawake wangekuwa wanajali basi wangeshaanza kubadilika lakini matokeo yake ndio kwanza wanazidisha tabia za hovyo so my point is wanaume mkiona mnaumizwa na mnachukizwa na umalaya na ukahaba wa wanawake basi chagueni moja either anzeni ninyi kubadilika au la hamuwezi basi kubalianeni na hali halisi
Okay, nina maswali kwako?

1. Nini kitatokea kama wanawake watagomea wanaume kulala nao hadi tu pale watakapojicommit kwa familia zao kwa kuja na wazazi wao kutoa posa na kuoa kihalali, je wanaume wakikutana na huo utaratibu watapata vipi mwanamke wa kufanya nae mahusiano ya kingono nje ya ndoa?

2. So katika haya maelezo yako yote umefanya assumption kuwa mwanamke hana akili wala ufahamu wa kutambua umuhimu wa bikra yake mwenyewe katika kuanza maisha na mwanaume, why aiweke rehani akijua thamani yake, so wanawake hajui thamani ya bikra?

3. Kama una assume wanawake hawajui thamani ya Bikra then nikuulize je ni sahihi pia kwa mwanaume kutojua wajibu wa kujali na kumtunza mke wake atakae muoa? Kama umeweza kumpa mwanamke pass ya kutothamini kitu kinachompa thamani muhimu kama mke wa mtu then automatically unaopia uhalali wa kuassume ni sahihi kwa wanaume wote kupewa pass au kukaushiwa kama wanafeli majukumu yao kwa makusudi, si ndio?

4. Umezungumzia swala la wanaume kutongoza mabinti kama ndio sababu ya mabinti wa kisasa kutokuwa na bikra na kutozitunza, nikuulize mama zetu na bibi zetu unadhani walikuwa hawatongozwi miaka hiyo, haukusikia story zao wakihadithia namna waliwakwepa babu zetu kwa sharti kuwa wakapose kwanza makwao ndipo mengine yataendelea haujawahi sikia hizo story, je swali langu kwako, unahisi ni wanaume wameshusha standards zao kama wanaume au ni wanawake wameacha kusimamia misimamo itakayolinda utu wao kwa wanaume na kuwaandaa kuheshimiwa katika ndoa kama wanawake wanaolinda miili yao?

5. Unajua kwamba kwa wastani miaka hii binti wa kisasa kati ya umri wa miaka 16 hadi 25 huwa ndoa kwake ni kosa, yaani ukimwambia nataka nikuoe na ukiwa tayari kwa kufanya hilo jambo basi atakukataa kwasababu mbali mbali kama kujiona bado mtoto kwa ndoa, shinikizo la wazazi kuwa asome kwanza mahusiano ni baadae, ulimbukeni wa uhuru wa kujiachia umri wa usichana ili watumike kwanza sababu soko la ngono linawaita sana, wanaume wa rika lao wanakuwa bado hawana pesa na mali hivyo kuolewa nao ni kujifunga na maisha ya usichana na kupitwa na fursa nyingi za kujipatia mali.

Je, swali langu, ni nani huwa anamkataa mwenzake katika umri wa miaka 16 hadi 25 kati ya binti ambaye ndio anachanua au kijana ambae bado ndio anajitafuta anauwezo wa kumudu vitu vidogo sana ila maisha ya kuishi pamoja na mke anaweza kujikongoja ,tuongee ukweli, Mwanamke katika umri huo masharti yake ili umuoe uishi nae kama mke na tamaa yake ya kuolewa huwa inakuwa sawa sawa na akifika kuanzia miaka 28 hadi 30+ huko? [emoji848][emoji848][emoji848]
 
Kuna mkaka leo katoka kuniambia anataka kunioa[emoji1]
Unajua nikamjibu nini? 'Bado niponipo kwanza'
@Jadda njoo usome hapa, mtu anataka kuoa anajibiwa "bado nipo nipo kwanza". Sasa kwann nisimtafutie ela ya simu mpya, saloon na kitimoto ili anipe hata nafasi ya kumkula tu kisha nitemane nae.
 
Mwisho wa kua na soko ni miaka mingapi?
Ukifika kati ya 28 na 30 soko lako la kuolewa linashuka kwa kasi sana. Ila soko la ngono linapanda yaani utakuwa ni mdoli wa ngono. Hadi ukongoronyoke.

Si unaona Kajala na akina uwoya, mbona hawaolewi na ni wanawake, ukisikia ndoa ni ndoa tu ya mtu anataka uwe malaya wake wa kuweka ndani ila hautakuwa mke kama mke yule wa kuheshimiwa na kukubalika kama mke wa mtu.

Kwa ground game ni ngumu sana huwa nawaonea huruma sana mabinti wanaofarijiana eneo la ndoa bila kujua kuwa mambo huwa yanawabadilikia huku juu.
 
Ukifika kati ya 28 na 30 soko lako la kuolewa linashuka kwa kasi sana. Ila soko la ngono linapanda yaani utakuwa ni mdoli wa ngono. Hadi ukongoronyoke.

Si unaona Kajala na akina uwoya, mbona hawaolewi na ni wanawake, ukisikia ndoa ni ndoa tu ya mtu anataka uwe malaya wake wa kuweka ndani ila hautakuwa mke kama mke yule wa kuheshimiwa na kukubalika kama mke wa mtu.

Kwa ground game ni ngumu sana huwa nawaonea huruma sana mabinti wanaofarijiana eneo la ndoa bila kujua kuwa mambo huwa yanawabadilikia huku juu.
Nitachangamka nikifika 25, sasa hivi badobado
 
@Jadda njoo usome hapa, mtu anataka kuoa anajibiwa "bado nipo nipo kwanza". Sasa kwann nisimtafutie ela ya simu mpya, saloon na kitimoto ili anipe hata nafasi ya kumkula tu kisha nitemane nae.
Aisee! Mimi nina mipango yangu, na ndoa ni mpango wangu wa 3
Wa kwanza hata bado sijaumaliza nikarukie ndoa..kisa tu mtu anataka kunioa sasa hivi big No..

Yeye anataka kuoa sababu kakamilisha mipango yake.. Vipi kuhusu mipango yangu?? Siwezi kujisahau kisa ndoa
Nikamilishe yangu ili hata nikiingia kwenye ndoa naenda kuitumikia bila kua na stress ya mipango mingine.

Ndoa sio kitu cha lazima ila ni muhimu!!!!
 
Kama suala ni kuitunza nyumba na kunipikia chakula je yeye alikua haishi hapo? Alikua hali hapo? Kama mimi natakiwa kufidia muda na jitihada zake kunitunzia nyumba na kunipikiq chakula kupitia kugawana mali mbona mwanamke hawajibiki kunirudishia fidia ya gharama nilizoingia kumpa hifadhi na chakula na matunzo mengine(mavazi, matibabu n.k)?
Kubwa linaloangaliwa ni :-
1. Value ya muda wake aliopoteza akiwa na wewe.
2. Utulivu wa akili aliokupa mpk ukaweza kupata pesa na kupanga mipango ya kimaendeleo.
3. Utu aliokuonesha.

Thamani ya hivyo vitu 3 ni kubwa mno, hailipiki. Ndiyo maana mahakama huwa inaamua tu kwamba mgawane mlivyo navyo
 
Ningekuwa sijaoa haki ya nani nisingeoa kamwe.
Wanawake wa siku hizi hawana haiba za waifu materials wameharibiwa na mitandao ya kijamii CONTENT CREATORS wanawafundisha kulipa kisasi ,nyimbo za kizazi kipya zinawafundisha UKINICHIT NAKUCHIT ya nini tumiizane roho unakuta nyimbo inaimwa na mke wako eti SIKU HIZI HAKUNA MAHABA MAPENZI YA MKATABA bado ukienda Tik Tok mkeo analetewa video ambazo anapenda zaidi kuzisikiliza kama za kupambana na mwanaume ndo anazilike basi Artificial intelligence ya mitandao ya kijamii humsogezea mavideo yanayofanana na hizo akili zake.
Zamani nilijua ukioa una uhakika wa uchi kumbe tena kuna kunyimwa
 
Kama kuna watu sio waoaji hamaniishi ya kwamba ni sawa kwa waoaji wakandamizwe na sheria husika. Suala ni sheria kuwekwa katika mzani sawa iwe kwa muoaji na ambae sio muoaji ili ikitokea kutengana na mwenzake kuwe na fair playing ground.
Kenya tayari wamefanyia amendment sheria ya ndoa yao.
 
A

Aah wapi naijua hiyo.. Siwezi kukataa ndoa wakati sijatendwa vya kutendwa na wanawake hata watano.. Ndo kwanza nilianza na kamoja nilikavuta ndani kammakonde kale KAKANICHANGAMSHA FASTA ZA USO ila sijakataa tamaa bado nijaribu Kwanza pengine.. Nitafutie kabinti kamwalimu au nesi nataka nijaribu huko hawa wasio na mishe wanakupiga double yaani hata ya kusuka rasta Zake akutegemee wewe na bado analianzisha anytime... Bora niteseke Na Ka madam changu kamwalimu Nitafutie seriously Tena awe shule za vijijini ili nije kumvuta town uhamisho chap connections tamisemi Ninazo
Jaribu mwalimu ila kwa nesi usijaribu ni hatari sana kwako
 
Nadhani unayo hoja ya msingi kabisa. Ila kukufumbua macho zaidi ni vema ukafahamu kuwa ndoa haijawai wala haitawahi kuja kuwa outdated concept bali shida ni wahusika wanaoingia ndani ya ndoa kutokuwa na vigezo au uwezo wa kusimama ndani ya ndoa.

Kuna sababu ambazo kimsingi zinasababisha ndoa katika kizazi cha sasa kuwa kazi kubwa kuitumikia, na sababu zenyewe ni kama ifuatavyo:

1. Ndoa ni taasisi, na kila taasisi ndani yake ina watendaji wenye vigezo na uwezo wa kuitumikia. Huwezi kuajiri askari jeshi bila mafunzo ya jeshi. Huwezi ajiri muhasibu bila kufuzu mafunzo ya chuo na CPA, huwezi ajiri mkemia bila kuwa na cheti cha mkemia, je kwenye ndoa, hawa mabinti wa kisasa na vijana ni wapi hukaa kambi hata ya mwaka m'moja kupitia mafunzo makali ya ndoa?

2. Wanaume wameshusha sana standards zao kwa wanawake na wanawake wamepandisha sana standards zao kwa wanaume. Mwanamke zamani aliqualify kuwa mke kwa kuwa bikra kama sifa ya lazima, halafu tabia nzuri ikawekwa kama sifa inayofuata ya lazima.

Leo hii wanaume hii sifa hamuhangaiki nayo tena wanaume wengine wanatetea kabisa kwa kusema kwan kuna ubaya gani akiwa hana bikra, hawa ni wanaume wanaotetea si wanawake, sasa kwann wanawake wasikubaliane na huo uhalisia kuwa wanaume hawana shida na bikra watatuoa hata wakikuta tulishazaa na wanaume kwahiyo wacha tukachezewe kuna mabwege yatatulipia mahari na kutuoa.

3. Wanaume miaka hii wamekuwa wakwepa majukumu au wabeba majukumu yasiyowahusu. Mwanaume anazaa na binti ila hajui wajibu wake kama Mume na baba, hajui majukumu yake kwa kitu alichokianzisha mwenyewe anatoa toa macho kama ng'ombe na kusubiria wakwe, mashemeji, na familia yake wafanye jambo kumsaidia. Au anakutana na mwanamke ambaye sio wake ana watoto yeye huyo kabebelea, ni wa kwako? Kwann usitafute wa kwako? Hiyo roho nzuri si ungelea watoto wa dungu zako wenye hali ngumu, kwenda kulea mabao ya watu halafu ndio uitwe mwanaume wa shoka ni ujinga kutoka sayari gani huo? [emoji848] Kwa sampuli hii ya wanaume ndoa haiwezi kuwa imara.

4. Kudharau mafunzo ya kimaadili na Maagizo ya mwenyezi MUNGU ambayo kaagiza watu kuyafuata ili kuwa imara kiimani na kimwili ila viburi sasa vya wanadamu leo ndio matokeo yake tupo hapa ndoa zinaendeshwa kwa idea za movies za Hollywood, tamthiria za Telemundo, na hawa relationship coaches wa mitandaoni.

5. Wanawake wa sasa ni wavivu eneo la ndoa ila wanabidii kujihangaikia. Mwanamke unaweza mkuta alikuwa amepanga analipa Kodi kwa biashara ndogo ndogo au ameajiriwa lakini siku ukianza kaa nae ndani hatochangia hata 1000 endapo kutakuwa na dharula na mwanaume haupo karibu au haupo na vema kiuchumi kwa kukwambia wewe ni mwanaume as if yeye ndie huwa analipa 100% ya bills. Kwa kifupi ubinafsi.

So kimsingi Ndoa haijawai na haitakuja kuwa outdated concept shida ni wahusika kutokutambua na kusimamia vigezo vya ndoa na kuisimamia vilivyo kwa kila mojawapo kukaa eneo lake na si kuingiliana.
Safi sana umeongea vyema
 
Aisee! Mimi nina mipango yangu, na ndoa ni mpango wangu wa 3
Wa kwanza hata bado sijaumaliza nikarukie ndoa..kisa tu mtu anataka kunioa sasa hivi big No..

Yeye anataka kuoa sababu kakamilisha mipango yake.. Vipi kuhusu mipango yangu?? Siwezi kujisahau kisa ndoa
Nikamilishe yangu ili hata nikiingia kwenye ndoa naenda kuitumikia bila kua na stress ya mipango mingine.

Ndoa sio kitu cha lazima ila ni muhimu!!!!
Tatizo liko kwenye hiyo mipango. Wadada wengi unakuta anasema siolewi mpk nikamilishe mipango yangu lkn ukimchunguza utakuta hicho anachokiita mpango kiko centred kwenye kuitumikisha k.

Yaani unakuta ana biashara ndogo ama kazi ya kawaida ambayo haimpi nafasi ya yeye kujenga future yoyote. Ili apate kiwanja, gari, ama kuikuza biashara yake lazima ampate sponsor aitafune k.

Mwisho wa siku mdada kama huyu anakuwa anadanga na anachakaa kihisia, kiroho, kimwili na kijamii kuliko aliyeko kwenye ndoa.

Kwahiyo nasisitiza uwe na mipango inayokupa thamani kama mwanamke, siyo mipango inayokupa uhuru wa kudanga.
 
Back
Top Bottom