Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi, Mhe. Martha Festo Mariki amewaasa Wanawake wa Mkoa wa Katavi kutumia vyema fursa ya utoaji mikopo ya Halmashauri ya Asilimia Kumi (10%) inayotolewa na Serikali ili kujikwamua kiuchumi
Mbunge Martha Mariki ameyasema hayo katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani 2025 yaliyofanyika tarehe 05 Machi, 2025 mkoani Katavi ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhe. Charles Makongoro ambaye amekaimu nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko (Ambaye yupo likizo)
"Tuitumie vyema mikopo ya asilimia 10 kwa kuzalisha sana kwenye miradi iliyopo katika maeneo yetu ikiwemo biashara, ufugaji, kilimo na miradi mingine ambayo tunaona inaendana na kiwango cha fedha zinazotolewa na Serikali yetu" Mbunge Martha Mariki
Aidha, Mbunge Martha Mariki ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuwekeza katika sekta ya afya kwa kujenga hospitali na kusambaza vifaa tiba; katika elimu, miundombinu ya usafirishaji, miradi ya maji na nishati safi ya kupikia
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani 2025 yaliyofanyika tarehe 05 Machi, 2025 mkoani Katavi yameacha ujumbe mzito kuhusu umuhimu wa uwezeshaji wa wanawake kwa maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.