Zamani ukipita mtaa wa pili ukasikia wimbo unajua tu kuna kanisa. Siku hizi mpaka uone viashiria ama usikie maneno. Kanisa lilikusudiwa kuibadili dunia, lakini kinyume chake dunia inalibadili kanisa. Mavazi ya kisasa, nyimbo za kisasa, maisha ya kisasa, mahubiri ya kisasa, etc. Bahati mbaya ni kuwa Mwenyezi Mungu habadiliki, ila sisi wanadamu tunapata definition mpya kila uchao. Tunajaribu kumfanha Mungu a-fit kwenye system ya maisha yetu badala ya sisi kujifitisha kwenye utaratibu wake. Haya ndio matokeo yake.