Martha Mwaipaja atoboa siri sakata la Rose Muhando

Martha Mwaipaja atoboa siri sakata la Rose Muhando

Natamani siku moja ungeingia kwenye music industry ujue kilichoko huko.!
Kuna mengi sana ambayo hutakaa hata uelewe hata ukifundishwa mwaka mzima.

Siku ukikutana na muimbaji wa muziki wa injili muulize hili swali. "Kwanini unaimba"?
Akiwa anakujibu muangalie usoni kwa makini anachokujibu kisha oanisha na matendo yake.
Au ukikutana na Mhubiri wa Injili wa siku za leo... "Muulize hivi mpendwa kwanini umeamua kuwa mhubiri."?? Akiwa anakijibu muangalie usoni kwa makini kisha oanisha majibu yake na matendo yake

Kisha ukipata hayo majibu jifungie chumbani kwako Muombe sana Mungu.
Wafanya biashara. Naam, utasikia uzinduzi utafanywa na mh Lowassa. Au wengine utasikia maombi ya kufunga na kuomba mgeni rasmi mama Samia. Wengine tunabaki kushangaa tu
 
Sipendi sana unyanyasaji wa namna hii mbaya zaidi anamlazimisha na Penzi.... I wish ningekuwa naniliu watu kama hawa unawadetain kishumundu
 
Zamani ukipita mtaa wa pili ukasikia wimbo unajua tu kuna kanisa. Siku hizi mpaka uone viashiria ama usikie maneno. Kanisa lilikusudiwa kuibadili dunia, lakini kinyume chake dunia inalibadili kanisa. Mavazi ya kisasa, nyimbo za kisasa, maisha ya kisasa, mahubiri ya kisasa, etc. Bahati mbaya ni kuwa Mwenyezi Mungu habadiliki, ila sisi wanadamu tunapata definition mpya kila uchao. Tunajaribu kumfanha Mungu a-fit kwenye system ya maisha yetu badala ya sisi kujifitisha kwenye utaratibu wake. Haya ndio matokeo yake.
Kuna watu mnajua kuunda sentensi, una akili na hekima💪
 
Yes,hii ni vita halisi ya kiroho ila wengi hawajui!
Kuimba ni ibada kamili na ni anointing ,shetani anajua ndo maana anapambana kuwatoa kwny mstari!
Kumbe unawajua.! So gospel muziki huwa ni ngazi tu ya kupandia kuelekea matamanio yao. Ukisha fanya muziki kuwa ngazi ya kupandia lazima ukubali masharti yaliyo katika hiyo ngazi ili usiangukie pua.
Kuna mengi sana nyuma ya pazia la muziki.
Ambayo hayaelezeki kwa maandishi lakini kifupi lazima ujue muziki wa injili ni vita halisi katika ulimwengu wa roho.!
Nimeyashuhudia hayo kila mahali nilipoenda kuandaa matamasha haya ya muziki wa Injili. Na hadithi yake ni ndefu sana.!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom