Martha Mwaipaja atoboa siri sakata la Rose Muhando

Martha Mwaipaja atoboa siri sakata la Rose Muhando

MARTHA MWAIPAJA ATOBOA SIRI KUHUSU MATESO YA ROSE MUHANDO
[emoji737]
[emoji737]
Msanii wa nyimbo za injili Martha Mwaipaja ambaye ni miongoni mwa wasanii walio karibu sana muimbaji Rose Muhando ameeleza kilichotokea kwa Rose Muhando .

Martha ameeleza jinsi Rose alivyojiingiza kwenye madawa ya kulevya na jinsi alivyolazimika kujihusisha kimapenzi na meneja wake aitwaye Nathani.

Martha anaeleza kuwa vita ya kiroho ilimuelemea Rose Muhando. Rose Muhando ana meneja wake aitwaye Nathan ambaye ndiye aliyemtoa kimuziki mpaka akafahamika. Kiufupi huyo meneja wake ndiye aliyegharamia gharama zote za kurekodi albamu ya kwanza ya Rose Muhando baada ya kuachana na kitimtimu kwaya. Rose Muhando aliingia mkataba na Nathan ambao kwa mujibu wa Martha Mwaipaja ulikuwa ukimkandamiza Rose Muhando na kumnufaisha meneja.

Martha Mwaipaja anayedai amekuwa karibu na Rose Muhando kiasi cha kumueleza kila lililomsibu anatolewa mfano kwamba ili umualike Rose Muhando kwenye show ni lazima uingize milioni mbili kwenye akaunti ya Nathan, halafu laki tano utampatia Rose Muhando atakapokuja kupafomu. Hivyo Rose Muhando akitoka kwenye show anapewa laki tatu kwenye hiyo milioni mbili na inayobaki yote anachukua meneja. Ilifika hatua ikawa meneja akila pesa za watu mbalimbali na kumlazimisha Rose ajaperform na mara nyingine Rose aligoma kwenda na matokeo yake alikuwa akipata lawama za utapeli mara kwa mara.

Martha Mwaipaja anaendelea kueleza kwamba Nathan alitumia nafasi yake ya umeneja kumtumia Rose Muhando kimapenzi pamoja na kuwa alikuwa mume wa mtu. Rose Muhando alijaribu kupambana na hali hiyo lakini mwisho wa siku akajikuta akijihusisha kimahusiano na meneja wake huyo.

Meneja alimtumia Rose Muhando kimapenzi na kiuchumi, kuna kipindi Rose Muhando alipata mchumba mwingine ambaye alitaka kumuoa lakini alikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Nathan. Martha Mwaipaja anasema mchumba huyu aliyekuwa rafiki wa karibu wa Masanja mkandamizaji alipata vitisho vikali kutoka kwa Nathan. Yeye Martha na Masanja ndiyo waligeuka wasuluhishi wa kutafuta utatuzi wa hali hiyo. Martha anasisitiza kuwa Nathan hakupenda Rose Muhando aolewe na mtu mwingine, wakati Rose Muhando akiwa amechoka kuzini na Nathan akijitakia ndoa yake mwenyewe. Kuna siku Nathan alimnyoishea bastola kwa muda wa dakika tano akimtishia asimuache kwenda kwa huyo mchumba wake mpya.

Rose Muhando ndiye aliyekuwa akimhudumia mchumba huyu mpya kwani alikuwa na hali duni kifedha. Rose alifikia hatua ya kumjengea nyumba kwao kwa wazazi wa mchumba wake huyu mchumba wake. Kama wahenga wasemavyo bora umfadhili mbuzi utakula mchuzi Rose alimfumania mchumba huyu mpya na mwanafunzi wa shule laivu bila chenga.

Rose Muhando alichanyikiwa na akajikuta amerudi tena na kuangukia kwenye penzi la meneja wake Nathan ambaye ni mme wa mtu.

Martha anasema Rose Muhando alitumikishwa kwa show zisizokoma na ilifika hatua anachoka anaishiwa nguvu anaanguka jukwaani anatolea mfano alivyoanguka madhabahuni kwa Rwakatale. Martha Mwaipaja anasema Rose Muhando alikuwa si mtu wa furaha muda mwingi alikuwa akilia awapo peke yake. Martha Mwaipaja anasema Rose Muhando alimwambia kwa uchungu kuwa anafanya kazi ngumu lakini anawafanyia watu wengine.

Ili kuondoa uchovu na stress kutokana na wingi wa matamasha ambayo Nathan alikuwa ameshakula pesa, Nathan alimlazimisha Rose kunywa vilevi ili akaperform bila kuchoka haraka, Martha Mwaipaja anasema alishuhudia hili kwa macho yake kwenye show ya mwanza.

Ilifika hatua pombe zikawa hazifui dafu ikawa zamu sasa ya madawa ya kulevya, ikafika hatua haimbi tena amekuwa teja na ndiyo hali Rose Muhando aliyonayo sasa.

Martha Mwaipaja anaeleza kuwa Rose Muhando alipoamua kujinasua kwa meneja wake huyo alipata vitisho vikali kutoka kwa Nathan na Msama wa msama promotion waliomtisha kuwa kama ataachana na huyo meneja atapoteana kimuziki.

Martha Mwaipaja anasema tumuombee Rose Muhando badala ya kumhukumu. Waimbaji wa nyimbo za injili wamechukua nafasi ya shetani, shetani ndiye alikuwa kiongozi wa sifa kabla ya kutupwa kuzimu. Hivyo shetani anawawinda sana kwani wamechukua nafasi yake.
 
Aiseee... Ukiweza kuepuka mbakutona/uzinzi/uasherati na Tamaa ya pesa PEPO hii hapa wallah.
 
dah niliwah kufikiri pengine alipita hiyo njia. Kweli tumuombee
 
No matter what happens she will always be the Queen of Gospel music....

GOD blessed her with a second to non talent, her first album might be the best selling album of all times(Tz)..

Its not easy to be a Queen, ill always love you Rose.

Sent from my SM-J700F using JamiiForums mobile app

Binafsi siwaamini wauza muziki wa injili. Wengi sio mfano bora kwa jamii. Wana majivuno, wazinzi, wanafiki, wasengenyaji, matapeli na wako after money zaidi kama wanamuziki wa "muziki wa dunia"
Wale wa kike, wengi ni tongozable!!
 
Na ifahamike leo
Yeremia 17 inasema hivi:

5 Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana.

6 Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.

7 Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake.

8 Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda.



Tumuombee rehema dada Rose, kwani inaonekana roho ilko radhi lakini mwili ni dhaifu. Amen
 
Huyu tumekula nae bangi hapa Dom toka yuko hiyo timtim unafikiri ile mizuka alikuwa anatoa wapi
 
Tumuulize yule kijana Amani aliyemtaja kuwa Rose ni mama yake wa hiari akaishia kusemwa. Anaweza kujua siri nzito behind the seen.

Pili tusichanganye dini na siasa kwenye kueneza neno. Huyu Rose alidhulumu watu pesa kisa anakwenda chato kwenye kampeini mara akaanza kuonekana majukwaa ya ccm. Swali ina maana Bashite alipotaja wabwia unga hakujua Rose anabwia au labda .......
 
Tatizo la dalali kugeuka kuwa promota, unatarajia nini zaidi ya kukuletea njaa zake?!

Sheria ichukue mkondo wake! Tamwa kesi hii ni yenu. Shangazi wa taifa msaidieni huyu mama, hasa kitendo cha kutishiwa bastola na ubakaji.

Pia huyo promota afataliwe kama alikuwa analipa kodi kisawasawa!

Vitu vingine hata kama ni ujinga wa Mtu(Rose) . kufanya mikataba ya kinyonyaji si sawa na inakuondokea credibility mhusika.

Basata kama mnavyo kataa nyimbo chafu ni wakati kuwe na kitengo/utaratibu cha kupitia mikataba ya wasanii hata kwa kulipia gharama.
 
Nimesoma haya maelezo kuna nusu ya ukweli na Nusu ya chumvi.!
Binafsi ni muandaaji wa Matamasha haya ya muziki wa injili. Nimeanza kufanya kazi na Rose mwaka 2007.
Akiwa chini ya Nathan, na bila shaka Nathan ndio meneja pekee Rose aliyewahi kuwa naye.!
Nathan alimuwezesha Rose kuwa na maendeleo kadhaa, Nathan aliweza kumsaidia Rose kumiliki magari kadhaa ikiwemo Rav 4 ya blue gari yake ya kwanza kisha baadae prado .alimuwezesha kuwa na makazi yake pale ipagala.!
Rose alipoamua kuachana na Nathan kwa sabbu anazozijua yeye aliangukia kwenye mikono ya watu kadhaa, mbona haujaeleza habari za yule meneje mchungaji Fake aliye mnyang'anya passport na gari zake?
Wakati akienda marekani?
Rose kaanza kupotea hewani baada ya kuondoka kwenye mikono ya Nathan hakujua tena upepo wa umaarufu wake unampeleka wapi. Hakuwa na Nguzo imara tena kwa kazi zake.!
Baada ya kuachwa huru na Nathani kila mtu alikuwa anajipigia je amekueleza kuhusu wale vijana aliokuwa anaambatana nao pale Dodoma?

Mimi binafsi Rose Muhando keshakula pesa yangu nyingi tu, na wala sio Nathan, kuna watu amewaumiza zaidi ya unavyoweza kuleta hayo maelezo ya Martna. Isingekuwa muziki wa Injili natumai angekuwa amefanyiwa kitu kibaya sana!
Mara ya mwisho nimemtafuta Rose mwezi huu tarehe 13 . Kupitia kwa Producer wangu na akatoa maelezo kuwa kazi yoyote atakayopaswa kuifanya ipitie kwa Meneja wake Nathan.

Hii ikiwa kabla ya video ya Nairobi haijaanza kusambaa mitandaoni.

Mwisho. Rose Mhando bado ana nafasi ya kufanya vizuri zaidi kama atampata mtu sahihi wa kumsimamia Kiafya, na kazi zake kwa ujumla.
Usione vinaelea vimeundwa bila Nathani usingemfahamu Rose mhando.
Kwa maelezo yako haya unamaanisha huyo Nathani alikuwa na uhalali wa kumfanya Rose nyumba ndogo yake kisa kamuwezesha kununua gari na kujenga nyumba? Hizo gari na Nyumba hela ilitoa nathan au ilikuwa ni ya rose mwenyewe, naona unatetea ujinga, yawezekana ni kweli rose ana mapungufu yake lakini nathan na msama wamechangia kumporomosha rose
 
Hawa watu wanaoishi maisha ya kilokole, sometime ukiingia kwenye maisha yao unaweza ukajiona ww bonge la mtakatifu, kwani wengi wao ni wanafiki.

Ndio maana usishangae amber rutty akaiona pepo na mlokole akaingia motoni, pole Rose kwani huu ni wakati wa kumtafuta Mungu na uishi yale unayo yaimba.
Yaan kiukweli wanaojiita walokole ni wanafki kupitiliza, katika kumi ukipata mmoja ni katika wale mafukara haswa tofauti na hapo hakuna.
 
Natumai utakuwa umeshamaliza povu lako,!
Kama una hakika na unachokisema kuwa wamehusika kumporomosha si angeinuka basi mwingine ambaye hawezi kumporomosha? Mbona mnakuwa wepesi wa lawama zaidi ya kufuatilia ukweli?
Nimesema pale juu, sehemu ya shughuli zangu imehusika na hawa watu hivyo imenipa nafasi kuwafahamu zaidi ya watu wengine.!!
Nawewe je umefanya nao kazi hivyo unafahamu lolote zaidi yangu?
Je unafahamu waimbaji wangapi wa gospel. Wa kike wanaotamani kujulikana leo.? Na huko chini wanafanya ama kufanyishwa nini?

Kama una Uchungu sana leta namna unayoiona kuwa bora ya wazo lako tuweze msaidia Rose sio unakuja na povu kujifanya wewe ndiye mwenye akili zaidi.
Kwa maelezo yako haya unamaanisha huyo Nathani alikuwa na uhalali wa kumfanya Rose nyumba ndogo yake kisa kamuwezesha kununua gari na kujenga nyumba? Hizo gari na Nyumba hela ilitoa nathan au ilikuwa ni ya rose mwenyewe, naona unatetea ujinga, yawezekana ni kweli rose ana mapungufu yake lakini nathan na msama wamechangia kumporomosha rose
 
Back
Top Bottom