Martin Maranja Masese :Maridhiano bila ukweli na uwajibikaji ni usaliti

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Historia haina huruma kwa watawala katili. Historia inatunza kumbukumbu za sauti zilizopazwa mchana, lakini zikamezwa na giza totoro. Leo watawala wanazungumzia maridhiano, neno tamu vinywani, lakini lenye makovu makubwa moyoni

‪Mwanachama mwandamizi wa CCM, alisimama, akanyoosha kidole hadharani akasema: “Tupatane kwanza kabla ya uchaguzi” Akatekwa, akapotezwa. Alipotea kwa hiari au alipotezwa kwa lazima? Sauti yake ikawa kama mwangwi uliopotea bondeni

‪Jaji Joseph Sinde WARIOBA

‪Mzee wetu wa heshima, akapaza sauti: “Tusikimbilie sanduku la kura bila maridhiano.” Badala ya kumsikiliza, mawe yakawa majibu yake. Mzee wa heshima akazuiwa, akawa mfungwa wa mawazo yake mwenyewe ndani ya kuta za nyumbani kwake

‪Askofu Josephat GWAJIMA,

‪Mtumishi wa Mungu akajitokeza, akashauri CCM na watawala, nchi inahitaji uponyaji, majadiliano kabla ya kwenda katika uchaguzi. Akashauri, uchaguzi huru na haki ni tunda la amani. Hakusikilizwa. Akapuuzwa. Akatukanwa. Akashambuliwa

‪Fr. Dr. Charles Hugo KITIMA,
‪Mwanatheolojia, alipojaribu kutoa ushauri wake wa busara kuelekea uchaguzi mkuu akiwa salama ndani ya makazi ya Maaskofu, alivamiwa na maharamia. Alishambuliwa. Akaonewa sana. Akayaona mauti moja kwa moja usoni kwake. Mbaya sana

‪Captain John Charles TESHA?
‪Askari wa JWTZ, alisema mengi, akataka maridhiano ya dhati. Akasema mifumo imeharibika na inahitaji marekebisho. Leo, sauti yake imekuwa kama redio iliyozimwa ghafla katikati ya msiba mzito. Tesha na wengine, walioona mvua kabla ya mawingu

‪Tundu Antiphas Mughwai LISSU
‪Mwanasheria mashuhuri, Mwanasiasa nguli, na Mwenyekiti wa CHADEMA, alizunguka kuwaeleza wananchi kuhusu umuhimu wa ‘NO REFORMS, NO ELECTION”, hakuvumiliwa, akakamatwa akiwa katika ziara za CHADEMA, ameshtakiwa kwa UHAINI

‪Na wengine wengi, waliotekwa na kupotezwa.

‪CHADEMA hatuwezi kusahau. Chini ya jua kali na mvua za EL NIÑO, ngurumo na radi, tulipita katika matope tukidai kitu kimoja: Mageuzi ya msingi kabla ya Uchaguzi. Lakini majibu yalikuwa ni kutekwa, magereza na kuzuiliwa kufanya siasa

‪Shingo za watawala zilijawa na kiburi, mioyo ikawa migumu, mkiamini ushindi ni kuiba kura na si kuchaguliwa na wananchi. Hamkutaka kuchaguliwa. Mkajitangaza washindi kwa ushindi wa kishindo. Watu milioni 32 walishiriki uchaguzi wapi?

‪Vongozi wa kiroho hawakubaki kimya. Walionya na walisema maridhiano si chaguo, ni hitaji la lazima ili taifa lipumue. Lakini, shingo za watawala zilikuwa ngumu sana. Mkajiona miungu watu msiohitaji ushauri wa ardhi wala mbingu. Mkasonga tu

‪Mdude Nyagali alivamiwa usiku, akatekwa na kupotezwa. Deusdedith Soka alitekwa na kupotezwa. Dioniz Kipanya alitekwa na kupotezwa. Mamia ya vijana wa CHADEMA, watoto wazalendo wa Tanzania, walitekwa na kupotezwa. Hii ni tabia mbaya

‪Baada ya kuitimiza azma yenu na kuwapoteza watu wenye sauti na kuwapiga mawe watu wenye hekima; baada ya kuvuna mlichokusudia kwa nguvu. Mmefikia kile mlichokusudia. Mlichokikinga, mlichokilinda, mlichokitimiza kwa nguvu zote

‪Mnataka maridhiano ya aina gani?

‪Maridhiano ya kumsafisha mkosefu bila kutubu? Maridhiano ya kunyamazisha watu waliojeruhiwa kwa risasi za moto, ili msisikie sauti za maumivu yao? Maridhiano ya dhati yanayoanza na KUKIRI MAKOSA na KUWAJIBIKA? Sasa, tumekataa ulaghai

‪HAKI za watu wote waliouwawa, waliopotezwa, waliofungwa gerezani, na wote waliojeruhiwa. Maridhiano bila ya wahusika kukiri makosa yao ni kiini macho. CHADEMA hatuwezi kutumika katika safari ya wananchi kuelekea kusikojulikana

‪Maridhiano bila haki ni usaliti

‪Maridhiano ya kweli yanahitaji ujasiri kukiri makosa, si ujasiri wa kuficha yaliyopita. Yanahitaji haki, si hila. Yanahitaji sauti zisikike, si sauti za wapinzani kuzimwa ili zao pekee zisikike. Wapinzani waseme wapi panavuja. Watawala wakiri makosa

‪Kama mmetimiza mlichokusudia, angalau kuweni na ujasiri wa kusema: Tulikosea. Msione aibu. MLIUA.

‪MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila

Soma pia : Maridhiano bila maelewano 'a forced reconciliation', ni kosa kubwa kwa CHADEMA
 
 
Wote ulio wataja ni wa msalabani

Bila ya kujali umesemwa na nani, ukweli haubadiliki. Japo msemaji amesahau wengine wengi walioshauri, kama Shura ya maimamu, lakini ujumbe ulikiwa ni huo huo, kufnya mabadiliko muhimu kabla ya uchaguzi ili uchaguzi uwe halali, na Taifa lifanye uchaguzi halali likiwa na umoja, wtawala maharamia hawakupokea ushauri wowote, na kisha kuendelea na mipango ya kuwaua watakaofungua vinywa vyao kutaka uchaguzi uwe wa haki. Taifa lipo kwenye laana ya kutawaliwa na maharamia.
 
nonsense 🐒
 
Naunga mkono hoja. Mkaa waliouwasha kwa ajili ya kuchomea wengine utawachoma na wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…