Martin Maranja: Najutia kumpa mtoto wangu jina la “Freeman”

Martin Maranja: Najutia kumpa mtoto wangu jina la “Freeman”

Kitendo cha kumuondoa uwenyekiti mbowe,kilikuwa kitendo cha kuiponya CHADEMA
Kama ni hivyo kwa nini mnakililia kirusi kilichosababisha ugonjwa wenu kiungane nanyi kwenye shughuli za chama chenu. Si mmpona! Pambaneni basi kwa nguvu mpaya maana mmepona maradhi yaliyokuwa yakiwasumbua. Acheni kirusi kibaki huko mlikokitupa.

Amandla...
 
Dogo baba yako. Wakati tunaanzisha hili jukwaa bado ulikuwa unavaa nepi wewe.
Fala wewe kama bado unaburuza na Martin ,watoto wa juzi ; mmeshazoea kuchunga mbuzi.

We mshamba kaishi porini ,huku mjini hatuwezi kumpa nchi Lissu wala kumsikiliza mchunga Mbuzi .
 
Mbowe alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chadema mwaka 2004. Wakati anachaguliwa Chadema ilikuwa na wabunge 5, Mbowe akiwa mmojawapo.

Katika uchaguzi wa 2015, Chadema ilitangazwa mshindi wa majimbo 34 ya uchaguzi, walipata pia viti maalum 36 vya wanawake. CUF ilipata viti 32 vyakuchaguliwa na 10 maalum. Act Wazalendo na NCCR mageuzi walitangazwa wabushindi katika jimbo moja moja. Umoja wa UKAWA ulikuwa na wabunge 112. Mwenyekiti wa Ukawa alikuwa Mbowe. Hivyo katika miaka 11 ya uongozi wake Chadema kiliongeza idadi ya wabunge kutoka watano hadi 70. Idadi hiyo ya wabunge ilikiwezesha chama cha Chadema kupata ruzuku kubwa ambayo ilichangia katika kukitangaza nchi nzims. Hili wanafik hawalioni, wanakazania tu kuwa Mbowe amewachelewesha.

Uamuzi wa kushirikiana na vyama vingine na kumkaribisha Lowassa ndio ulileta mafanikio hayo. Leo wapuuzi wanasema aliwachelewesha.

Lissu alishinda uchaguzi mwaka jana na sasa hivi Chadema haina mbunge hata mmoja.

Amandla....
 
Fala wewe kama bado unaburuza na Martin ,watoto wa juzi ; mmeshazoea kuchunga mbuzi.

We mshamba kaishi porini ,huku mjini hatuwezi kumpa nchi Lissu wala kumsikiliza mchunga Mbuzi .

Fala baba yako.
 
Mzee @freemanmbowetz

Wanyama wa porini huua/kupigana kwa sababu zinazohusiana na mahitaji ya kuishi: chakula, kujilinda, kulinda watoto au eneo. Simba anawinda kwa ajili ya chakula siyo mateso, chuki, kisasi

Binadamu ni viumbe katili zaidi ya wanyama. Binadamu anaweza kumdhuru mwingine kwa sababu ya chuki, ubaguzi, tamaa, kulipiza kisasi, madaraka au kwa sababu anaona mwingine hafai kuishi

Kutoka Mikocheni kwenda ilipo Mahakama Kuu ya Tanzania ni umbali usiozidi 5KM. Kutoka Mikocheni kwenda Rufiji ulipo mradi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) ni umbali wa 260KM

Unaweza kusafiri kwenda mkoa mwingine kwa zaidi ya saa tano kuhudhuria shughuli za Serikali katili ya CCM lakini huwezi kutumia dakika 10 kutoka kwako kwenda Mahakama Kuu katika kesi ya TAL?

Huwezi kwenda safari ya 5KM kumuona Mwenyekiti wako wa chama, aliyerithi kiti chako katika uchaguzi HURU na HAKI lakini unaweza kwenda 260KM kuungana na watesi wa Mwenyekiti wako?

Nini muhimu zaidi kwako? Ni wewe ulitueleza miradi ya maendeleo haiwezi kuwa mbadala wa haki za binadamu. Leo kuna watu wanatekwa na kupotezwa, wanashtakiwa kwa ugaidi na uhaini. Hujui?

Lakini umechagua nini? Nimekusikiliza ukisema “mradi wa JNHPP usichukuliwe kisiasa kwa kuwa ni mradi unaokwenda kusaidia uchumi”. Umesahau ulitueleza nini kuhusu miradi ya MAGUFULI?

Kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, Freeman Aikaeli Mbowe kwa sasa ni ‘mjumbe wa kudumu wa kamati kuu ya CHADEMA - ni kutokana na hiki kinachoitwa ‘ustaafu’ wa uenyekiti wa CHADEMA Taifa

Kwa maana kwamba, Freeman Mbowe yupo katika kundi sogozi la WhatsApp na mengine (kama yapo) ambayo wajumbe wa kamati kuu wanajadili kwa hisia zao tofauti masuala mbalimbali ya chama

Mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu CHADEMA huwezi kwenda Mahakamani katika kesi ya kiongozi wa chama, lakini unaweza kwenda katika shughuli zinazoongozwa na mwenyekiti wa CCM

Freeman Mbowe umesahau, wakati ukishtakiwa kwa makosa ya uongo ya UGAIDI, Tundu Lissu alikuwa Belgium akijiuguza majera ya risasi. Aliomba kukutana na Rais alipokuwa Brussels

Pamoja na mambo mengine waliyokubaliana, alisema Mwenyekiti Freeman Mbowe aachiwe ndiyo tufungue ukurasa mpya. Tundu Lissu alitujulisha mwenyewe hayo alipozungumza na umma.

Tundu Lissu akiwa na siku 500 gerezani. Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA, Freeman Mbowe hujawahi kukanyaga Mahakamani kuanzia Kisutu hadi Mahakama Kuu hata kwa bahati mbaya.

Saa 24 baada ya Mahakama Kuu kusema Tundu Lissu ana kesi ya kujibu katika mashtaka ya UHAINI ya uongo na uzandiki, Freeman Mbowe unaibuka katika shughuli za Serikali ukiwa na MAWAZIRI.

Mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu ya CHADEMA umekataa kabisa kuhudhuria shughuli zozote za CHADEMA lakini unaweza kuhudhuria shughuli unazoalikwa na WATAWALA KATILI wa CCM.

Unahudhuria shughuli za Serikali umeongozana na mawaziri wa Serikali katili ya CCM wakati ambao wanachama na wafuasi wa CHADEMA kwa mamia wamekamatwa na kushtakiwa kwa UGAIDI?

Mzee Freeman Mbowe umesahau haraka. Kuna watu walifungwa gerezani, wengine sasa ni walemavu, wengine sasa ni marehemu kwa sababu ya kupigania jina lako ukiwa kiongozi wa chama chetu.

Umesahau, wakati unakamatwa na Serikali katili ya CCM, 2021, wanachama wa CHADEMA walikwenda kuonyesha ‘solidarity’ na wewe pale KISUTU. Walikamatwa, wakashtakiwa, wakafungwa

Najutia zile siku nilisimama nawe, kukutetea na kunadi jina lako kwa nia njema kabisa nikifikiri unapambania uhuru, haki na mabadiliko ya kweli. Haikuwa hivyo. Ulitudanganya tukishindwa.

Nasema kwa kuwa kwa hiari yangu, niliamua kusimama nawe, kukunadi katika mazingira ambayo ilionekana ni kama kuuza kitimoto Mecca. Lakini sikutarajia tukishindwa, tuisaliti CHADEMA

Wengine sasa tumeelewa kwa kuchelewa sana. Hii chuki haiwezi kuwa ya kushindwa uchaguzi. Lazima kuna mafekeche mengine. Kuna kingine kimeujaza chuki moyo wako. Je, kuna mrija, umekatwa?

Najutia kumpa mtoto wangu jina lako, Freeman.

View attachment 3655185
Aende pia pale RITA akabadili jina la mwanae
 
Viongozi wengi wa siasa akiwemo Makamu Mwenyekiti wa Chadema wanakiri wazi mchango mkubwa wa Mbowe katika safari yao ya siasa. Sijasikia mpaka sasa hivi kiongozi yeyote wa kisiasa akisema kuwa Lissu alimjenga katika siasa. Hao nao watasema kuwa Mbowe aliwachelewesha?

Amandla...
 
So touching, hata sisi tusio wanasiasa tumeumia, sio sawa hata kidogo.
Huenda hata attempt ya assassination ya TAL ilikuwa plotted na huyu jamaa, who knows!
BTW, wachaga mbele ya pesa wanaweza kufanya lolote, the man's so selfish!!
Tulisema mbaya wa Lissu ni Mbowe,watu wakakomaa tu Magufuli,hata Sirro alimwambia Mbowe kama wewe ni mlokole kweli apa kwa biblia kuwa hujafanya,hii ilionyesha Sirro akiwa IGP alimjua Mbowe vizuri sana na akaiacha kesi ya Lissu maana alijua wanachezeana mchezo.
 
Kwa ulio wataja kamanda.. ni wangapi bado wapo huko .Alafu Prof.J sio kweli ndugu .Tuachane nayo,hivi makamanda mnafikiri ni sahihi Mbowe kutukanwa kila kukicha kwenye mitandao tangu Lissu awe mwenyekiti? Ninayo imani kua Lissu atakua huru lakini sio sawa kumtukana Mh.Mbowe
Kama anafanya mambo ya kishenzi atatukanwa sana na mimi nasema atukanwe tu! Maana huwezi ukawa mnafiki,ukaachwa eti kisa uliwahi kufanya mema, huo ni upuuzi sana,utakapo fanya mema utapongezwa na ukifanya upumbavu utasemwa kwa upumbavu wako! Huwezi kusema eti kwakuwa alifanya mema basi hata akifanya ushenzi tuufunike hapana haipo hivyo, ndio maana kiimani tunaamini kuwa Hata shetani kabla ya kuwa shetani alikuwa malaika mwema kabisa na alipendwa kwa kazi yake ya kumburudisha mungu wake, lakini alipo hasi alitupwa na sasa ni shetani na alilaaniwa hata kama alikuwa anamburudisha vizuri kabisa mungu na alimpenda sana.
 
Tulisema mbaya wa Lissu ni Mbowe,watu wakakomaa tu Magufuli,hata Sirro alimwambia Mbowe kama wewe ni mlokole kweli apa kwa biblia kuwa hujafanya,hii ilionyesha Sirro akiwa IGP alimjua Mbowe vizuri sana na akaiacha kesi ya Lissu maana alijua wanachezeana mchezo.
Usipotoshe magufuli hakumpenda lissu kwa sababu ya ukweli wa lissu dhidi ya maovu ya magufuli na ndio maana alisha panga kupoteza kabisa kwa kumtumia wauwaji wakamuue ,kwa hilo huwezi kumtetea huyo magufuli kwa hoja nyepesi kama hiyo
 
Back
Top Bottom