Martin Maranja: Najutia kumpa mtoto wangu jina la “Freeman”

MAWAZO YA UWANDISHI WAKO BADO NI MGANDO - Huwezi kuandika hoja nzito kama hii bila kupangilia hoja zako kwa mantiki ya msingi kama msomi mzuri - Unakuwa kama hujataka kuandika andiko kama msomi huru nadhani ujitafakari mwandishi kwa hilo maana upo very poor kabisa katika andiko lako unakuwa kama sio msomi au mtu umeenda shule kabisa .....​

Kaachwa nae huyu maana si kwa kilio hicho.
Unaendaje kumpa mwanao majina usiyoelewa badae unaanza kulaumu mwenyewe na unatuambia sisi ili iweje?
Manyumbu yameza uboho kichwani.
 
Mzee @freemanmbowetz

Wanyama wa porini huua/kupigana kwa sababu zinazohusiana na mahitaji ya kuishi: chakula, kujilinda, kulinda watoto au eneo. Simba anawinda kwa ajili ya chakula siyo mateso, chuki, kisasi

Binadamu ni viumbe katili zaidi ya wanyama. Binadamu anaweza kumdhuru mwingine kwa sababu ya chuki, ubaguzi, tamaa, kulipiza kisasi, madaraka au kwa sababu anaona mwingine hafai kuishi

Kutoka Mikocheni kwenda ilipo Mahakama Kuu ya Tanzania ni umbali usiozidi 5KM. Kutoka Mikocheni kwenda Rufiji ulipo mradi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) ni umbali wa 260KM

Unaweza kusafiri kwenda mkoa mwingine kwa zaidi ya saa tano kuhudhuria shughuli za Serikali katili ya CCM lakini huwezi kutumia dakika 10 kutoka kwako kwenda Mahakama Kuu katika kesi ya TAL?

Huwezi kwenda safari ya 5KM kumuona Mwenyekiti wako wa chama, aliyerithi kiti chako katika uchaguzi HURU na HAKI lakini unaweza kwenda 260KM kuungana na watesi wa Mwenyekiti wako?

Nini muhimu zaidi kwako? Ni wewe ulitueleza miradi ya maendeleo haiwezi kuwa mbadala wa haki za binadamu. Leo kuna watu wanatekwa na kupotezwa, wanashtakiwa kwa ugaidi na uhaini. Hujui?

Lakini umechagua nini? Nimekusikiliza ukisema “mradi wa JNHPP usichukuliwe kisiasa kwa kuwa ni mradi unaokwenda kusaidia uchumi”. Umesahau ulitueleza nini kuhusu miradi ya MAGUFULI?

Kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, Freeman Aikaeli Mbowe kwa sasa ni ‘mjumbe wa kudumu wa kamati kuu ya CHADEMA - ni kutokana na hiki kinachoitwa ‘ustaafu’ wa uenyekiti wa CHADEMA Taifa

Kwa maana kwamba, Freeman Mbowe yupo katika kundi sogozi la WhatsApp na mengine (kama yapo) ambayo wajumbe wa kamati kuu wanajadili kwa hisia zao tofauti masuala mbalimbali ya chama

Mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu CHADEMA huwezi kwenda Mahakamani katika kesi ya kiongozi wa chama, lakini unaweza kwenda katika shughuli zinazoongozwa na mwenyekiti wa CCM

Freeman Mbowe umesahau, wakati ukishtakiwa kwa makosa ya uongo ya UGAIDI, Tundu Lissu alikuwa Belgium akijiuguza majera ya risasi. Aliomba kukutana na Rais alipokuwa Brussels

Pamoja na mambo mengine waliyokubaliana, alisema Mwenyekiti Freeman Mbowe aachiwe ndiyo tufungue ukurasa mpya. Tundu Lissu alitujulisha mwenyewe hayo alipozungumza na umma.

Tundu Lissu akiwa na siku 500 gerezani. Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA, Freeman Mbowe hujawahi kukanyaga Mahakamani kuanzia Kisutu hadi Mahakama Kuu hata kwa bahati mbaya.

Saa 24 baada ya Mahakama Kuu kusema Tundu Lissu ana kesi ya kujibu katika mashtaka ya UHAINI ya uongo na uzandiki, Freeman Mbowe unaibuka katika shughuli za Serikali ukiwa na MAWAZIRI.

Mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu ya CHADEMA umekataa kabisa kuhudhuria shughuli zozote za CHADEMA lakini unaweza kuhudhuria shughuli unazoalikwa na WATAWALA KATILI wa CCM.

Unahudhuria shughuli za Serikali umeongozana na mawaziri wa Serikali katili ya CCM wakati ambao wanachama na wafuasi wa CHADEMA kwa mamia wamekamatwa na kushtakiwa kwa UGAIDI?

Mzee Freeman Mbowe umesahau haraka. Kuna watu walifungwa gerezani, wengine sasa ni walemavu, wengine sasa ni marehemu kwa sababu ya kupigania jina lako ukiwa kiongozi wa chama chetu.

Umesahau, wakati unakamatwa na Serikali katili ya CCM, 2021, wanachama wa CHADEMA walikwenda kuonyesha ‘solidarity’ na wewe pale KISUTU. Walikamatwa, wakashtakiwa, wakafungwa

Najutia zile siku nilisimama nawe, kukutetea na kunadi jina lako kwa nia njema kabisa nikifikiri unapambania uhuru, haki na mabadiliko ya kweli. Haikuwa hivyo. Ulitudanganya tukishindwa.

Nasema kwa kuwa kwa hiari yangu, niliamua kusimama nawe, kukunadi katika mazingira ambayo ilionekana ni kama kuuza kitimoto Mecca. Lakini sikutarajia tukishindwa, tuisaliti CHADEMA

Wengine sasa tumeelewa kwa kuchelewa sana. Hii chuki haiwezi kuwa ya kushindwa uchaguzi. Lazima kuna mafekeche mengine. Kuna kingine kimeujaza chuki moyo wako. Je, kuna mrija, umekatwa?

Najutia kumpa mtoto wangu jina lako, Freeman.

View attachment 3655185
Limfikie barabara hili andiko! Mungu amlaani yeye na kizazi chake! Amina
 
Huyo mtoto wako atakuwa na akili kuliko wewe.

Yaani mtu ukahudhurie kesi ya mtu asiyechana nywele na kuhamasisha wenzake wasichane na kuzungusha mikono tu juu.

Usiende kwenye uzinduzi wa kutuo cha kutoa umeme utaokuwa chachu ya maendeleo ya Taifa??

Mbowe yupo sawa kabisa, ukiwa mpinzani sio lazima kupinga kila kitu.

Yale mambo kazungumza pale, ndio inavyotakiwa sasa.

Sio kuhamasishana kutochana nywele na kuzungusha mikono juu.
 
Ila ukiwa mpinzani inatakiwa upinge nini?
 
Mlichelewa kumfahamu Mbowe, Mbowe ni Mnafiki na Mtu hatari sana, haifai kumwamini hata kidogo
 
So touching, hata sisi tusio wanasiasa tumeumia, sio sawa hata kidogo.
Huenda hata attempt ya assassination ya TAL ilikuwa plotted na huyu jamaa, who knows!
BTW, wachaga mbele ya pesa wanaweza kufanya lolote, the man's so selfish!!
Apo mwisho kwenye wachaga na pesa hii nadharia wailoianzisha walituweza mnoo. Siku hizi dunia imefungua taarifa unazipata kila kona sasa fanya tafiti zako kuhusu hizi nadharia zinazohusu makabila jee ziko sawa

Au kama kuna watu wanasimama na uyo mzee wa mafekechee kisa ukabila wataje
 
Ni kupitia mtandao wa X ambapo Martin Maranja Masese ameandika makala ndefu akisikitishwa na ushiriki wa Mbowe kwenye huo uzinduzi.

Kwakweli ameandika kwa uchungu mkubwa na mwishoe kasema anajuta kumpa mwanae jina la Freeman.

It is very bad!
Abadilishe tuu
 
Mzee @freemanmbowetz

Wanyama wa porini huua/kupigana kwa sababu zinazohusiana na mahitaji ya kuishi: chakula, kujilinda, kulinda watoto au eneo. Simba anawinda kwa ajili ya chakula siyo mateso, chuki, kisasi

Binadamu ni viumbe katili zaidi ya wanyama. Binadamu anaweza kumdhuru mwingine kwa sababu ya chuki, ubaguzi, tamaa, kulipiza kisasi, madaraka au kwa sababu anaona mwingine hafai kuishi

Kutoka Mikocheni kwenda ilipo Mahakama Kuu ya Tanzania ni umbali usiozidi 5KM. Kutoka Mikocheni kwenda Rufiji ulipo mradi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) ni umbali wa 260KM

Unaweza kusafiri kwenda mkoa mwingine kwa zaidi ya saa tano kuhudhuria shughuli za Serikali katili ya CCM lakini huwezi kutumia dakika 10 kutoka kwako kwenda Mahakama Kuu katika kesi ya TAL?

Huwezi kwenda safari ya 5KM kumuona Mwenyekiti wako wa chama, aliyerithi kiti chako katika uchaguzi HURU na HAKI lakini unaweza kwenda 260KM kuungana na watesi wa Mwenyekiti wako?

Nini muhimu zaidi kwako? Ni wewe ulitueleza miradi ya maendeleo haiwezi kuwa mbadala wa haki za binadamu. Leo kuna watu wanatekwa na kupotezwa, wanashtakiwa kwa ugaidi na uhaini. Hujui?

Lakini umechagua nini? Nimekusikiliza ukisema “mradi wa JNHPP usichukuliwe kisiasa kwa kuwa ni mradi unaokwenda kusaidia uchumi”. Umesahau ulitueleza nini kuhusu miradi ya MAGUFULI?

Kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, Freeman Aikaeli Mbowe kwa sasa ni ‘mjumbe wa kudumu wa kamati kuu ya CHADEMA - ni kutokana na hiki kinachoitwa ‘ustaafu’ wa uenyekiti wa CHADEMA Taifa

Kwa maana kwamba, Freeman Mbowe yupo katika kundi sogozi la WhatsApp na mengine (kama yapo) ambayo wajumbe wa kamati kuu wanajadili kwa hisia zao tofauti masuala mbalimbali ya chama

Mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu CHADEMA huwezi kwenda Mahakamani katika kesi ya kiongozi wa chama, lakini unaweza kwenda katika shughuli zinazoongozwa na mwenyekiti wa CCM

Freeman Mbowe umesahau, wakati ukishtakiwa kwa makosa ya uongo ya UGAIDI, Tundu Lissu alikuwa Belgium akijiuguza majera ya risasi. Aliomba kukutana na Rais alipokuwa Brussels

Pamoja na mambo mengine waliyokubaliana, alisema Mwenyekiti Freeman Mbowe aachiwe ndiyo tufungue ukurasa mpya. Tundu Lissu alitujulisha mwenyewe hayo alipozungumza na umma.

Tundu Lissu akiwa na siku 500 gerezani. Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA, Freeman Mbowe hujawahi kukanyaga Mahakamani kuanzia Kisutu hadi Mahakama Kuu hata kwa bahati mbaya.

Saa 24 baada ya Mahakama Kuu kusema Tundu Lissu ana kesi ya kujibu katika mashtaka ya UHAINI ya uongo na uzandiki, Freeman Mbowe unaibuka katika shughuli za Serikali ukiwa na MAWAZIRI.

Mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu ya CHADEMA umekataa kabisa kuhudhuria shughuli zozote za CHADEMA lakini unaweza kuhudhuria shughuli unazoalikwa na WATAWALA KATILI wa CCM.

Unahudhuria shughuli za Serikali umeongozana na mawaziri wa Serikali katili ya CCM wakati ambao wanachama na wafuasi wa CHADEMA kwa mamia wamekamatwa na kushtakiwa kwa UGAIDI?

Mzee Freeman Mbowe umesahau haraka. Kuna watu walifungwa gerezani, wengine sasa ni walemavu, wengine sasa ni marehemu kwa sababu ya kupigania jina lako ukiwa kiongozi wa chama chetu.

Umesahau, wakati unakamatwa na Serikali katili ya CCM, 2021, wanachama wa CHADEMA walikwenda kuonyesha ‘solidarity’ na wewe pale KISUTU. Walikamatwa, wakashtakiwa, wakafungwa

Najutia zile siku nilisimama nawe, kukutetea na kunadi jina lako kwa nia njema kabisa nikifikiri unapambania uhuru, haki na mabadiliko ya kweli. Haikuwa hivyo. Ulitudanganya tukishindwa.

Nasema kwa kuwa kwa hiari yangu, niliamua kusimama nawe, kukunadi katika mazingira ambayo ilionekana ni kama kuuza kitimoto Mecca. Lakini sikutarajia tukishindwa, tuisaliti CHADEMA

Wengine sasa tumeelewa kwa kuchelewa sana. Hii chuki haiwezi kuwa ya kushindwa uchaguzi. Lazima kuna mafekeche mengine. Kuna kingine kimeujaza chuki moyo wako. Je, kuna mrija, umekatwa?

Najutia kumpa mtoto wangu jina lako, Freeman.

View attachment 3655185
Alizingua sana kumpa hilo jina mtoto wake,ni bora angelimuita Masese.
 
1. Lissu alipopigwa risasi, Mbowe alisimama kidete kuzuia asipelekwe Muhimbili. Mbowe alihusika kikamilifu kuhakikisha kuwa anapata tiba stahiki Nairobi.
2.Lissu alipopigwa na kukamatwa Mbeya, Mbowe alipanda ndege mara moja kwenda kuungana nae.
3. Lissu na wenzake kuruhusiwa kurudi Tanzania na kuhakikishiwa usalama wake lilikuwa mojawapo ya masharti ya Chadema ya Mbowe kuingia katika mazungumzo kuelekea kwenye maridhiano.

Matokeo yake ni Mbowe kuitwa msaliti, aliyelamba asali. Lissu aliangalia tu na kuchochea moto.

Lissu alikataa hadharani wito wa Mwenyekiti wake kuhudhuria kikao cha Kamati Kuu cha chama chake akisema ana mambo muhimu zaidi ya kufanya.

Lissu alikataa kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa ambao chama chake kilishiriki.

Lissu aliwahi kusema kuwa chanzo cha fedha za Mbowe hakijulikani! Si alitaka tuelewe kuwa ama Mbowe anahongwa au ana biashara haramu.

Baada ya uchaguzi Lissu na chama chake hakikuwahi kumuomba radhi aliyekuwa Mwenyekiti wao kwa matusi na kejeli zilizoelekezwa dhidi yake.

Humu ndani kuna mabandiko kibao ya kutaka Chadema imzuie Mbowe kumuona Lissu kwa sababu anaweza kumdhuru.

Siwezi kujua kwa nini Mbowe hajaenda Ukonga au Mahakamani. Lakini sishangai maana bila shaka aliumizwa sana na kukaa kimya kwa Lissu alipokuwa anatukanwa wakati yeye alisimama nae wakati anapitia wakati mgumu.

Huyu Martin ambae ana hint kuwa Mbowe kama mjumbe wa Kamati Kuu ya CDM anaweza kuwa anatumika na CCM, anamkumbatia Msigwa ambae alisimama kwenye majukwaa na CCM kuinanga Chadema! Pure hypocrisy.

Mbowe hakumuomba amuite mtoto wake jina la Freeman. Anaweza kulibadili akitaka. Aanze kwa kuwakataza watu kumuita mtoto wake Freeman na afanye taratibu za kulibadilisha rasmi.

Unafik mtupu. Mbowe amealikwa kwenye shughuli ya kitaifa na ameenda bila kujificha. Hakwenda kama muwakilishi wa Chadema. Kama wameumizwa kiasi hicho, waanze taratibu za kumtimua kwenye chama. Ama sivyo, wamuache aendelee na maisha yake.

Amandla...
 
Ama kweli mjinga mjinga tuuu leo mwana lumumba buku7fc unamtetea mjumbe wa kamati kuu chadema pia kub msitafu na mbunge wa hai mala 3 mstafu kweli nyinyi chawa
Mjinga ni wewe na huyo anaejiliza kama fala akitegemea huruma za mwanaume mwenzie kwenye harakati zake.

Mbowe ni mtu ambae mnaweza kufanya mazungumzo akaelewa sio radical kama hao wengine wanaoendeshwa Kwa emotions.

Ndio maana CCM wanamuona wa maana ,ni moderate.

Kwa akili Yako ya hovyo unadhani kati ya J.Mnyika na Heche/Lisu ni yupi CCM waaweza kaa nae mezani?
 
Bwana Masese kasahau kanuni moja kwamba, "usiishi ukimtegemea mwanadamu"...
 
Kitendo cha kumuondoa uwenyekiti mbowe,kilikuwa kitendo cha kuiponya CHADEMA
 
Back
Top Bottom