Martin Maranja: Najutia kumpa mtoto wangu jina la “Freeman”

Martin Maranja: Najutia kumpa mtoto wangu jina la “Freeman”

Mbowe sio fala kwamba Yuko hapo kuendeshwa Kwa emotions.

Pambanane na lipeni gharama za ujinga wenu,mstake wengine wawabebee.
Usemacho ni kweli, kila mwana siasa ana malengo yake katika siasa , kupata umaarufu na Pesa au kutaka kubadlisha maisha yako na watu unaowao waongoza. Mbowe Kawa muwazi kuonesha upande anaoupenda
 
Jina huwa halina tafsiri, vinginevyo Kumamoto lingekuwa ni tusi lakini si tusi bali ni jina la mji huko Japani.
Huyo ni mkurya na majina yetu ya kibantu yana maana. Mashili kwa kisukuma lina maana, Mabele lina maana, makubi, Masato, Lusato, Zengo nk
 
Chillah kwa kinyamwezi ni uke wa Malaya mzee ,so hili ndio jina lako
Mimi sio mnyamwezi hivyo wala sina shida na maana yenu wanyamwezi.

Ila huyo mkurya Maranja lina maana na Masese lina maana... ndio maana ameshindwa kuwapa watoto wake majina katika hayo.

Ni kama ilivyo kwa Mayala kuwa ni Njaa kwa wasukuma... kwa wakurya halina maana.
 
So touching, hata sisi tusio wanasiasa tumeumia, sio sawa hata kidogo.
Huenda hata attempt ya assassination ya TAL ilikuwa plotted na huyu jamaa, who knows!
BTW, wachaga mbele ya pesa wanaweza kufanya lolote, the man's so selfish!!
Self centered kuliko
 
Ina maana huyu martin miaka yote hiyo alikuwa hajui kama mbowe yupo kimaslahi zaidi?

Just imagine kuna watu walipigika, walipasuka kisa kauli za mbowe.
 
Mbowe na Jeriko Nyerere wa mbutu Wana hasira sana na Lissu na chadema, na hili tukalitizame.
 
MMM, kwa umri wako you should have known better.

Some of us learned this early, nadhani nilikuwa na miaka 22/23 wakati ZZK anajadiliwa na kamati kuu ya CDM, Joto la kufutwa uanachama likiwa juu, Usiku wake alikuwa na kikao private nyumbani kwa Mwigulu Uzunguni, imagine the naivity ya kuwa mdogo halafu unashuhudia mazingira ya usaliti kwa macho!!!

Next time likitokea jambo kama hili ni kujipiga kifua na kusonga mbele, wakati tukiweka kichwani kuwa yeyote muda wowote anaweza kuyaaga mashindano, it’s never easy kuwa mpinzani katika vyama ambavyo wakati vinaundwa serikali ilikuwa na mkono wake humo.

Que sera, sera.
 
Mimi tangia siku ile Mbowe anahojiwa na Clouds kabla ya uchaguzi wao nilimsikiliza kwa macho ya rohoni nikajua kabisa huyu mzee na Mrema mwisho wao utakuwa sawa
Round ya kwanza aliwapiga tukio mkanyamaza mnakumbuka alikutana na Chaumma-chadema kwenye msiba wa Muasisi wa Chadema tena walivalia sare za chaumma
Round ya pili kaenda kwenye shughuli ya Ccm
Round ya tatu hamtaamini macho yenu
zangu pop corn tuu
 
Pamoja na uhuru aliokuwa nao, bado anefanya kitendo cha hovyo sana. Na kama alifikiri kinamjenga kisiasa, amekosea sana. Kwa sababu anaingia rasmi kwenye kundi la akina Lipumba, Mrema, Cheyo, nk.
Huyu atakuwa comedian zaidi ya mrema we subiri
mpaka 2030 ifike tutamuona mbowe vizuri😂😂
atawapiga chadema paipu sana
 
Mzee @freemanmbowetz

Wanyama wa porini huua/kupigana kwa sababu zinazohusiana na mahitaji ya kuishi: chakula, kujilinda, kulinda watoto au eneo. Simba anawinda kwa ajili ya chakula siyo mateso, chuki, kisasi

Binadamu ni viumbe katili zaidi ya wanyama. Binadamu anaweza kumdhuru mwingine kwa sababu ya chuki, ubaguzi, tamaa, kulipiza kisasi, madaraka au kwa sababu anaona mwingine hafai kuishi

Kutoka Mikocheni kwenda ilipo Mahakama Kuu ya Tanzania ni umbali usiozidi 5KM. Kutoka Mikocheni kwenda Rufiji ulipo mradi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) ni umbali wa 260KM

Unaweza kusafiri kwenda mkoa mwingine kwa zaidi ya saa tano kuhudhuria shughuli za Serikali katili ya CCM lakini huwezi kutumia dakika 10 kutoka kwako kwenda Mahakama Kuu katika kesi ya TAL?

Huwezi kwenda safari ya 5KM kumuona Mwenyekiti wako wa chama, aliyerithi kiti chako katika uchaguzi HURU na HAKI lakini unaweza kwenda 260KM kuungana na watesi wa Mwenyekiti wako?

Nini muhimu zaidi kwako? Ni wewe ulitueleza miradi ya maendeleo haiwezi kuwa mbadala wa haki za binadamu. Leo kuna watu wanatekwa na kupotezwa, wanashtakiwa kwa ugaidi na uhaini. Hujui?

Lakini umechagua nini? Nimekusikiliza ukisema “mradi wa JNHPP usichukuliwe kisiasa kwa kuwa ni mradi unaokwenda kusaidia uchumi”. Umesahau ulitueleza nini kuhusu miradi ya MAGUFULI?

Kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, Freeman Aikaeli Mbowe kwa sasa ni ‘mjumbe wa kudumu wa kamati kuu ya CHADEMA - ni kutokana na hiki kinachoitwa ‘ustaafu’ wa uenyekiti wa CHADEMA Taifa

Kwa maana kwamba, Freeman Mbowe yupo katika kundi sogozi la WhatsApp na mengine (kama yapo) ambayo wajumbe wa kamati kuu wanajadili kwa hisia zao tofauti masuala mbalimbali ya chama

Mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu CHADEMA huwezi kwenda Mahakamani katika kesi ya kiongozi wa chama, lakini unaweza kwenda katika shughuli zinazoongozwa na mwenyekiti wa CCM

Freeman Mbowe umesahau, wakati ukishtakiwa kwa makosa ya uongo ya UGAIDI, Tundu Lissu alikuwa Belgium akijiuguza majera ya risasi. Aliomba kukutana na Rais alipokuwa Brussels

Pamoja na mambo mengine waliyokubaliana, alisema Mwenyekiti Freeman Mbowe aachiwe ndiyo tufungue ukurasa mpya. Tundu Lissu alitujulisha mwenyewe hayo alipozungumza na umma.

Tundu Lissu akiwa na siku 500 gerezani. Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA, Freeman Mbowe hujawahi kukanyaga Mahakamani kuanzia Kisutu hadi Mahakama Kuu hata kwa bahati mbaya.

Saa 24 baada ya Mahakama Kuu kusema Tundu Lissu ana kesi ya kujibu katika mashtaka ya UHAINI ya uongo na uzandiki, Freeman Mbowe unaibuka katika shughuli za Serikali ukiwa na MAWAZIRI.

Mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu ya CHADEMA umekataa kabisa kuhudhuria shughuli zozote za CHADEMA lakini unaweza kuhudhuria shughuli unazoalikwa na WATAWALA KATILI wa CCM.

Unahudhuria shughuli za Serikali umeongozana na mawaziri wa Serikali katili ya CCM wakati ambao wanachama na wafuasi wa CHADEMA kwa mamia wamekamatwa na kushtakiwa kwa UGAIDI?

Mzee Freeman Mbowe umesahau haraka. Kuna watu walifungwa gerezani, wengine sasa ni walemavu, wengine sasa ni marehemu kwa sababu ya kupigania jina lako ukiwa kiongozi wa chama chetu.

Umesahau, wakati unakamatwa na Serikali katili ya CCM, 2021, wanachama wa CHADEMA walikwenda kuonyesha ‘solidarity’ na wewe pale KISUTU. Walikamatwa, wakashtakiwa, wakafungwa

Najutia zile siku nilisimama nawe, kukutetea na kunadi jina lako kwa nia njema kabisa nikifikiri unapambania uhuru, haki na mabadiliko ya kweli. Haikuwa hivyo. Ulitudanganya tukishindwa.

Nasema kwa kuwa kwa hiari yangu, niliamua kusimama nawe, kukunadi katika mazingira ambayo ilionekana ni kama kuuza kitimoto Mecca. Lakini sikutarajia tukishindwa, tuisaliti CHADEMA

Wengine sasa tumeelewa kwa kuchelewa sana. Hii chuki haiwezi kuwa ya kushindwa uchaguzi. Lazima kuna mafekeche mengine. Kuna kingine kimeujaza chuki moyo wako. Je, kuna mrija, umekatwa?

Najutia kumpa mtoto wangu jina lako, Freeman.

View attachment 3655185
Uko sahihi japo sijasoma gazeti lote
 
Nimemwangalia yale majasho usoni wakati anahojiwa nikasema utakufa vibaya sana weee mnafiki FM.
 
Wafuasi wa CHADEMA hawana tofauti na wafuasi wa Mwamposa. Wanaabudu watu. Badala ya kupambania sera za chama chao wanapambania mtu. MMM ni mfano hai wa watu waliokabidhi akili zao kwa viongozi badala kufuata katiba na misimamo ya chama. Siku Lissu akihamia CCM utaona watakavyomtukana balaa.
 
Back
Top Bottom