Uchaguzi 2020 Martin Munisi amfikisha Mbowe mbele ya Kamati ya Maadili

Uchaguzi 2020 Martin Munisi amfikisha Mbowe mbele ya Kamati ya Maadili

zanku

Member
Joined
Jun 9, 2020
Posts
70
Reaction score
152
Hai, Kilimanjaro

Mgombea udiwani Kata Ya Machame kupitia CCM Jimboni Hai, Ndugu Martin Munisi leo Mapema amefikisha Malalamiko yake kwa Msimamizi wa Uchaguzi dhidi ya Mgombea Ubunge kupitia Chadema Ndugu Freeman Mbowe

Malalamiko ya Martin Munisi ni kuwa Mgombea Wa Chadema Ndugu Freeman Mbowe mnamo Tarehe 07/09/2020 katika maeneo tofauti tofauti mfano kyeer na Nronga Jimboni Hai alimshutumu Diwani Martin Munisi kuongoza magenge ya wahalifu yanayoteka na kuumiza watu.

Munisi anadai alimpa Mbowe siku tatu za kumwomba Radhi au kudhibitisha lakini ameshindwa kufanya kufanya hivyo. Munisi amewasilisha Malalamiko yake kwa Msimamizi wa Uchaguzi Ndugu Yohana sintoo Ili Mbowe athibitishe tuhuma hizo au amwombe radhi hadharani kama alivyofanya otherwise achukuliwe hatua Kali za kimaadili ikiwemo kufungiwa kufanya kampeni ama kuondolewa kabisa kwenye kinyang'anyiro kwa ukosefu wa maadili.

IMG-20201016-WA0060.jpg
IMG-20201016-WA0059.jpg
IMG-20201016-WA0071.jpg

Hakuna kitu hapo mkuu, Mbowe aende nyumbani kwake kupiga Nyumba Mawe. Huyo hawezi kuthibitisha hiyo tuhuma ninachokiona hapo huenda ni ule usemi wa kesi ya Mbuzi anahukumu fisi basi lolote laweza kutokea.
 
Ha ha haaaa. Washajua hata mbwa akitupa karatasi linalomlalamikia mpinzani kwenye ofisi ya DED lazima afungiwe. Tuendelee kunakaribia kupambazuka maana giza linazidi.
 
Mmh! CCM wana hali mbaya sana huku mtaani. Wanyongeeee. Au washajua kwamba hawana chao uchguzi huu?
 
Mti wenye maembe ndiyo hupigwa mawe. Kila mleta pingamizi - CDM! Sijasikia chama kingine!
 
Sawa tumekusoma ndugu Martin Munisi.
 
Ukiwa na mtoto kila siku unakushitakia baba fulani kanipiga ujue umezaa boya na dhaifu
Ndo ccm kila sku kudeka deka tu
 
Uchaguzi huu CCM inakwenda kushinda kwa kishindo kwakua upinzani nidhaifu kuliko wakati wowote tangu kuanzishwa kwa vyama vingi.
 
Munisi Yuko sahihi .Jukwaani Mbowe alikuwa anatakiwa kunadi sera za za Chadema na atalifanyia Nini Jimbo Sio kumnadi negatively Munisi

Kamati ya Maadili imsikilize Munisi
 
Huyo Munisi ndio athibitishe kwamba hamiliki genge.
Hivi kwann wafaasi wa ccm wanafanya vitu vya ajabu na bado hawachuliwi hatua!!! ukiwa ccm unakuwa juu ya sheria eee!!?? watu wamerusha mawe kwa mgombea wa chadema, mbele ya askali, lakini askali anaangalia tu!! tunaenda wapi jamani??

Viongozi wa dini mko wapi jamani? pazeni sauti zenu!!

Wanasheria mko wapi jamani?? pazeni sauti zenu bhana!!

Wasomi mko wapi jamani?? bahati mbaya siku hizi hata mijadala iliyokuwa ikifanyika vyuoo vikuu haifanyiki tena!! Kina prof Shimji walikuwa wanaongoza mijadala moto moti! siku hizi kimiaaa! lakini naamini mpo pazeni sauti zenu bhana!!!

Wapenda haki mko wapi jamani?? pazeni sauti zenu bhana!! ccm wasituharibie
nchi!! nasema hivi ccm washambaaaaaaa!!
 
Kwani wasiojulikana si walikamatwa juzi wakakubali kuwa wao ni ccm ,na diwani ni mwanaccm hivyo akubali tuu kuwa na yeye ni walewale
 
Hivi kwann wafaasi wa ccm wanafanya vitu vya ajabu na bado hawachuliwi hatua!!! ukiwa ccm unakuwa juu ya sheria eee!!?? watu wamerusha mawe kwa mgombea wa chadema, mbele ya askali, lakini askali anaangalia tu!! tunaenda wapi jamani??

Viongozi wa dini mko wapi jamani? pazeni sauti zenu!!

Wanasheria mko wapi jamani?? pazeni sauti zenu bhana!!

Wasomi mko wapi jamani?? bahati mbaya siku hizi hata mijadala iliyokuwa ikifanyika vyuoo vikuu haifanyiki tena!! Kina prof Shimji walikuwa wanaongoza mijadala moto moti! siku hizi kimiaaa! lakini naamini mpo pazeni sauti zenu bhana!!!

Wapenda haki mko wapi jamani?? pazeni sauti zenu bhana!! ccm wasituharibie
nchi!! nasema hivi ccm washambaaaaaaa!!
Paza yako mkuu

Inatosha sana

Sent using Jamii Forums mobile app by My phone

Eti nabakia Africa.
 
Back
Top Bottom