Martin: Mwigulu tueleza ongezeko la Sh 1.85 Trilioni kwenye Mkataba wa Ujenzi wa SGR Tabora hadi Kigoma kabla ya kuomba fedha China na Benki ya Dunia

Martin: Mwigulu tueleza ongezeko la Sh 1.85 Trilioni kwenye Mkataba wa Ujenzi wa SGR Tabora hadi Kigoma kabla ya kuomba fedha China na Benki ya Dunia

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wakuu nimekutana na huu mjadala kuhusu zabuni ya ujenzi wa reli ya SGR kutoka Tabora hadi Kigoma ambao umeibua maswali muhimu kuhusu mchakato wa manunuzi na ufadhili wa mradi huo.

Ingawa TRC ilitangaza makubaliano ya ujenzi na kampuni ya CCECC Desemba 2022, kuna maswali juu ya tofauti ya bei iliyotangazwa na ile iliyoidhinishwa. Pia, kumekuwa na mjadala kuhusu kwa nini serikali inaomba fedha za ziada kwa ajili ya Lot 5 na 6 ilihali mkopo wa USD 3.5 bilioni kutoka AfDB tayari ulikuwa umekubaliwa.
5821318915911959835.jpg
Mchakato wa 'single sourcing' wa CCECC pia umesababisha mjadala zaidi, huku ishu ya kuhusu uwazi na utaratibu wa zabuni ikishika kasi.

Ishu iko hivi

Dec 20, 2022 serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania (Tanzania Railway Corporation) ilisaini mkataba wa ujenzi wa Standard Gauge Railway (SGR) kutoka Tabora hadi Kigoma (TBR-KGM) kwa urefu wa 506km.

Gharama za ujenzi ulitajwa kugharimu $2.7bn (Sh6.34 trilioni) na ujenzi utachukua miezi 48. Kusaini kipande hiki, Serikali iliwekeza $10.04bn (Sh23.3 trilioni) kwa awamu ya DSM-Mwanza na Tabora-Kigoma.

Waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba, akisoma hotuba ya bajeti 2022/23, uk.44, alisema serikali imeanza mchakato kutafuta mkandarasi ujenzi SGR (Tabora-Kigoma) 514km kwa $2.1 bilioni (Sh4.89T).

Kabla ya mkataba, walikuwa wamewapa kandarasi China Civil Engineering construction corporation (CCECC) kwa utaratibu wa manunuzi wa zabuni usio na ushindani (single source) tangu mwezi June 2022.

Pia, Soma: Zaidi ya Tsh. Trilioni 1 zimepigwa kwenye ujenzi wa Reli ya SGR

Mwigulu alisema ni 514km, (TRC) walisaini mkataba kujenga 506km. Kuna pungufu ya 8km. Mwigulu alisema ujenzi utagharimu Sh4.89 trilioni lakini mkataba umesainiwa Sh6.34 trilioni. Ongezeko Sh1.45 trilioni.

Masanja Kadogosa alisema mikataba haitakuwa na mabadiliko ya bei, ikijumuisha vitu vya ujenzi, ongezeko $1.304bn (30.3%, thamani ya fedha) HALIPO. Ongezeko la bajeti ya serikali na mkataba imetoka wapi?

Katika mfumo wa TANePS, ilionekana CCECC walipewa zabuni kwa Sh6.69 trilioni. Tofauti ya bajeti ya Mwigulu na TANePS ni Sh1.85 trilioni. Tofauti ya bajeti ya Mwigulu na mkataba (TRC na CCECC) Sh1.45 trilioni.

Mwigulu akisoma bajeti kuu ya serikali 2022/2023 alisema “serikali imeanza mchakato” wakati ukweli ni kwamba CCECC alikuwa tayari amepewa zabuni tangu April 04, 2022 kwa utaratibu wa ‘single source’.

(CCECC) alipewa zabuni hiyo bila ushindani (single source) ambayo ilidumu TANePS kwa dakika 30, yenye BID ID 421346 ambayo ipo secured. Opening na Closing date yake ni 10:00 hadi 10:30, 04/04/2022

Hii ndiyo zabuni (CCECC) ilivyoonekana TANePS. Mwigulu, Bajeti ya serikali ilisema ni $2.1bn (Sh4.90 trillioni) kwa 516km. Mkataba wa ujenzi uliosainiwa TRC na CCECC ni $2.7bn (Sh6.34 trilioni) 506km

CCECC alipewa zabuni hiyo bila kushindana ana zaidi ya 38% ya kiasi ambacho Mwigulu (waziri wa fedha) amekitaja katika hotuba yake ya bajeti. Gharama za ujenzi ni US$4.8M (Sh11.19bn) kwa kila kilometa 1

Hii tofauti ni ziada Sh1.45/1.85 trilioni, hatupewi ufafanuzi. Ghafla, Serikali inaomba pesa CHINA za ujenzi wa SGR lot Na. 5 na 6 na wanakwenda kuomba pesa Benki ya Dunia (WB) kufadhili vipande vilivyosalia.

Soma: China kutoa uamuzi wa kufadhili ujenzi wa SGR baada ya tathmini kukamilika hivi karibuni

CCECC alipewa lot Na. 5, Isaka–Mwanza (249km). Miezi 16 alijenga 4.4% na HAKUNA kipande kimoja cha reli aliweka katika miezi 17. Mwigulu akaenda bungeni kusema haukuwepo ufadhili wa kifedha.

RICHMOND; ilipewa zabuni ya kuzalisha umeme ikiwa haina fedha, wataalam na ofisi. Hii iliondoka na Edward Lowassa. (CCECC) wamepewa zabuni katika mazingira hayo. Mwigulu anakiri hawakuwa na fedha.

CCECC alipewa ujenzi wa lot Na. 6 Tabora - Kigoma (506km). Ujenzi wa 506km mkandarasi angetumia $2.7 bilioni (Sh6.34 trillioni). Alipewa zabuni bila ushindani; TANePS ilionyesha ni Sh6.69 trilioni.

Phase 1; DSM–Morogoro (300km) kandarasi Yapi Merkezi na Mota Engil Africa. Phase 2; Morogoro -Makutupora (422km) kandarasi Yapi Merkezi. Phase 3; Makutupora–Tabora (294km) kandarasi Yapi Merkezi.

Kumbuka, ujenzi wa phase 3 umetajwa kugharimu $1.9 billion (Sh4.43 trillioni). Phase 3 ni kutoka Makutupora –Tabora (294km) haijakamilika na kutumika hadi sasa. Kandarasi hii walipewa Yapi Merkezi.

Mwigulu na TRC, (CCECC), alikidhi wapi vigezo kupewa kandarasi yenye thamani ya $2.7 bilioni (Sh6.34 trillioni) wakati kwa miezi 17 alifanikiwa kujenga lot Na.5 kwa 4.4% pekee? Hapa kuna mzaha mkubwa.

(CCECC) kipande cha Tabora-Kigoma (514km) anachukua Sh6.34 trilioni. Nusu ya fedha zote ambazo zilitengwa kwa ujenzi wa DSM-Mwanza. Sh14.9 trillion (US$6.4 billion). Hapa kuna mashaka makubwa.

Athari za kutumia mzabuni mmoja kwa utaratibu wa manunuzi wa zabuni zisizoshindanishwa (single source) ni kiini kikubwa cha rushwa, uzembe, upendeleo, pamoja na uwezo mdogo wa mzabuni.
Lipo ongezeko kubwa (TZS 1.85 trilioni) la fedha kati ya TRC na CCECC (nje ya bajeti) fedha za walipa kodi. Hivyo ni LAZIMA tuelezwe, tupate ufafanuzi. Biashara imegubikwa na mashaka makubwa. Ndiyo.
Screenshot 2024-10-23 115449.png
Mwigulu, kabla ya kuomba fedha China na (WB) za ujenzi wa lot Na 5 na 6 mtueleze, zipo wapi Sh1.85 trilioni ambazo ni ongezeko katika fedha ambazo zipo kati ya bajeti ya Serikali na Mkataba wa Ujenzi.

Ujenzi wa lot Na. 6 kutoka Tabora - Kigoma (506km) uliombewa mkopo wa fedha unaosubiri kuidhinishwa African Development Bank (AfDB) wa $3.5 bilioni (Sh9.53 bilioni). Pesa zinakwenda wapi?

Ziada hii ipo wapi? Ujenzi kutoka Tabora—Kigoma ni 506km za kwenye mkataba wa ujenzi kati ya TRC na CCECC au 514km katika hotuba ya bajeti ya Kuu ya Serikali ya Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba?

Uwazi na uwajibikaji katika ujenzi wa miradi ya kimkakati ni muhimu. Tunapata wasi wasi na mashaka makubwa na hapa tunakumbuka Open Government Partnership (OGP) ambayo Serikali ilijiondoa.

MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.
 
Back
Top Bottom