Unajisikiaje unapotangaza Uongo ulio dhahiri dhidi ya jirani wako? Una uhakika ktk Tz kuna jamii hata kihistoria iliowahi kutumia nyama ya binadamu kama kitoweo hata ktk ushirikina? Mi Nadhani kama jambo hulijui ni busara kuuliza.
Kihistoria kuna jamii moja ya wakenya, walitumia nyama ya binadamu (wareno) kama kitoweo, kwa Tz ulishawshi kusikia hayo?
Kuna imani za kishirikina huku, kwa baadhi ya jamii, nazo ni ngeni toka Congo na Zambia, ambazo huamini viungo vya albino huweza kutumika ktk kufanikisha mambo yao kishirikina, kama utajiri, kipato nknk, si chakula.
Kihistoria, duniani kote na ktk jamii zote, kulikuwepo na kwa baadhi ya jamii bado hadi sasa, imani inayoamini mtu kuwa albino ni mkosi, najisi hivyo hapaswi kuishi, hilo lipo Afrika yetu yote, tukubalii uwepo wa tatizo ndio tufanikiwe kulikabili, sio kulificha. Swala la imani hizi lipo ktk jamii nyingi za kiafrika, tulishawahi kuuliza humu kama kuna mtu alishawahi kumuona albino Mmasai.