Marufuku Mtanzania kujiunga Jeshi la nchi nyingine

Marufuku Mtanzania kujiunga Jeshi la nchi nyingine

NASIRIYA

Member
Joined
Dec 11, 2022
Posts
12
Reaction score
24
Tax apiga marufuku kwa watazania kujiunga na la Jeshi la nchi nyengine. Alisema kwa mujibu wa sheria zao Mtanzania yoyote haruhusiwi kujiunga na Jeshi la nchi yoyote isipokuwa Jeshi la Tanzaia tu na kufanya hivyo kuvunja sheria za nchi.

---

SERIKALI: ‘Fuateni sheria na taratibu mkiwa nje ya nchi’

Tax.jpg



Serikali imewataka Watanzania kuzingatia na kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi walizopo ili kulinda taswira nzuri ya nchi yao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Stergomena Tax kuhusu kifo cha Nemes Tarimo, Mtanzania aliyefariki dunia nchini Urusi, alisema:

“Nitoe rai kwa Watanzania kuhakikisha wanazingatia sheria kanuni na taratibu za nchi walizopo, na pia wawe mabalozi wazuri wa kulinda taswira ya Tanzania.

Ikumbukwe kwa mujibu wa sheria zetu, Mtanzania yeyote haruhusiwi kujiunga na jeshi la nchi yoyote isipokuwa Jeshi la Tanzania na kufanya hivyo ni kuvunja sheria,” amesema Waziri huyo.

Amesema Mtanzania huyo alikwenda nchini Urusi mwaka 2020 kwa lengo la kujiunga na Chuo Kikuu cha Moscow Technological University (MIREA) kwa masomo ya Shahada ya Uzamili katika fani ya Business Informatics.

Ameongeza kuwa Mwezi Machi 2022, Mtanzania huyo alitiwa hatiani kwa kuhusika na vitendo vya uhalifu na kwa mujibu wa sheria za Urusi alihukumiwa kifungo cha miaka saba jela.

Waziri Tax ameongeza kuwa Tarimo akiwa gerezani alijiunga na kikundi cha kijeshi cha Urusi cha Wagner kwa ahadi ya kulipwa fedha na kuachiwa huru, baada ya kumaliza muda wa kutumika vita na alifikwa na umauti akiwa nchini humo.

Waziri Tax amesema kuwa mwili wa marehemu umeondoka nchini Urusi leo Januari 24, 2023 na unatarajiwa kuwasili nchini muda wowote kuanzia sasa na kuongeza kuwa Serikali imekuwa ikiwasiliana na Serikali ya Urusi, ili kuhakikisha mwili wa marehemu Tarimo unarejeshwa nchini na kukabidhiwa kwa familia yake kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Waziri ametoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na Watanzania kwa msiba huo.

Waziri Tax amewauhakikishia umma na Diaspora wa Kitanzania wakiwemo wanafunzi walioko masomoni duniani kote kuwa serikali itaendelea kuwapa ushirikiano wakati
 
Tax apiga marufuku kwa watazania kujiunga na la jeshi la nchi nyengine. Alisema kwa mujibu wa sheria zao Mtanzania yoyote haruhusiwi kujiunga na jeshi la nchi yoyote isipokuwa jeshi la Tanzaia tu na kufanya hivyo kuvunja sheria za nchi.View attachment 2495160
CCM wanavunja sheria za nchi hii kila siku,mi nikipata nafasi najiunga na jeshi lolote hata kama ni somalia,!!
Yaani upate nafasi ya kujiunga na jeshi la Marekani,ukatae kisa uraia wa TZ!!!?aaaah wapi,hiyo passport yenu natupa,nachukua uraia mwingine
 
Back
Top Bottom