Voice of Tanzania
JF-Expert Member
- Sep 23, 2018
- 2,036
- 3,107
Ujinga huo nife njaa. Niache fursa nchi nyingine mtuajiri sasa kama mna uwezo lakini sio kututishia nyau
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Marekani Wana uraia pacha mambo ya kuukana uraia ni huku kwetuUnaowaona insta wameukana uraia wa tz kabla ya kujiunga kwao. Maana jeshi la marekani lenyewe linalazimu uchukue uraia wa nchi hiyo kwanza
Naunga mkono hoja.Ccm wanavunja sheria za nchi hii kila siku,mi nikipata nafasi najiunga na jeshi lolote hata kama ni somalia,!!
Yaani upate nafasi ya kujiunga na jeshi la Marekani,ukatae kisa uraia wa TZ!!!?aaaah wapi,hiyo passport yenu natupa,nachukua uraia mwingine
Kabla ya kukemea muangalie nafasi ya vijana nchi mwao kwenye majeshi yetu haya.Tax apiga marufuku kwa watazania kujiunga na la jeshi la nchi nyengine. Alisema kwa mujibu wa sheria zao Mtanzania yoyote haruhusiwi kujiunga na jeshi la nchi yoyote isipokuwa jeshi la Tanzaia tu na kufanya hivyo kuvunja sheria za nchi.
---
SERIKALI: ‘Fuateni sheria na taratibu mkiwa nje ya nchi’
View attachment 2495178
Serikali imewataka Watanzania kuzingatia na kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi walizopo ili kulinda taswira nzuri ya nchi yao.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Stergomena Tax kuhusu kifo cha Nemes Tarimo, Mtanzania aliyefariki dunia nchini Urusi, alisema:
“Nitoe rai kwa Watanzania kuhakikisha wanazingatia sheria kanuni na taratibu za nchi walizopo, na pia wawe mabalozi wazuri wa kulinda taswira ya Tanzania.
“Ikumbukwe kwa mujibu wa sheria zetu, Mtanzania yeyote haruhusiwi kujiunga na jeshi la nchi yoyote isipokuwa Jeshi la Tanzania na kufanya hivyo ni kuvunja sheria,” amesema Waziri huyo.
Amesema Mtanzania huyo alikwenda nchini Urusi mwaka 2020 kwa lengo la kujiunga na Chuo Kikuu cha Moscow Technological University (MIREA) kwa masomo ya Shahada ya Uzamili katika fani ya Business Informatics.
Ameongeza kuwa Mwezi Machi 2022, Mtanzania huyo alitiwa hatiani kwa kuhusika na vitendo vya uhalifu na kwa mujibu wa sheria za Urusi alihukumiwa kifungo cha miaka saba jela.
Waziri Tax ameongeza kuwa Tarimo akiwa gerezani alijiunga na kikundi cha kijeshi cha Urusi cha Wagner kwa ahadi ya kulipwa fedha na kuachiwa huru, baada ya kumaliza muda wa kutumika vita na alifikwa na umauti akiwa nchini humo.
Waziri Tax amesema kuwa mwili wa marehemu umeondoka nchini Urusi leo Januari 24, 2023 na unatarajiwa kuwasili nchini muda wowote kuanzia sasa na kuongeza kuwa Serikali imekuwa ikiwasiliana na Serikali ya Urusi, ili kuhakikisha mwili wa marehemu Tarimo unarejeshwa nchini na kukabidhiwa kwa familia yake kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Waziri ametoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na Watanzania kwa msiba huo.
Waziri Tax amewauhakikishia umma na Diaspora wa Kitanzania wakiwemo wanafunzi walioko masomoni duniani kote kuwa serikali itaendelea kuwapa ushirikiano wakati
Sasa hao tayari ni raia wa marekaniKuna watanzania wengi nawafahamu ni wanajeshi wa marekani lakini badala ya kutoa kauli kali atueleze balozi zetu zinafanya Nini pale watanzania wanapopata matatizo wakiwa nje ya nchi.
Wanahakikisha wanapata mawakili pia wanapata muda wa kuwatembelea ni wazi Kuna uzembe kwenye wizara yake.
Na lazima atakuwa raia wa marekani
yeah amechukua uraia kabisa alienda somea engineering akaunga jeshi mazimaNa lazima atakuwa raia wa marekani
Tayari huyo
Ova
Weka details zake mkuuUnatamani umgoo
Nini tafsiri ya kushabikia,na ni ipi tafsiri ya kutoa maoni?
Good observation , Kama waziri ingekuwa vyema angetaja kabisa hiyo Sheria na kifungu husika.Sheria gani imevunjwa nikijiunga na jeshi la nchi nyingine.
Ya uhamiaji na makazi. Kama uko interested na majeshi ya nchi zingine, ukane uraia wa tz kisheria then chukua uraia wa nchi husika ambapo utataka kujiunga na jeshi hilo
Kuna watanzania wengi nawafahamu ni wanajeshi wa marekani lakini badala ya kutoa kauli kali atueleze balozi zetu zinafanya Nini pale watanzania wanapopata matatizo wakiwa nje ya nchi.
Wanahakikisha wanapata mawakili pia wanapata muda wa kuwatembelea ni wazi Kuna uzembe kwenye wizara yake.
Sawa tu, maana utakuwa sio mtzUkijiunga ukahama na uraia?
Siku Estonia wakipigana na tz utakaa upande ganiNo mie nipo Estonia nafanya mambo yangu
Upande wa Estonia mkuuSiku Estonia wakipigana na tz utakaa upande gani
Unamaanisha yule mfungwa?Huyo hakujiunga kwa hiyari yake Bali kwa kulazimishwa serikali ilitakiwa kutoa tamko kuilaan Urusi kwa inachokifanya hasa kwa wageni maana ni kinyume na haki za binadamu