Marufuku Mtanzania kujiunga Jeshi la nchi nyingine

Marufuku Mtanzania kujiunga Jeshi la nchi nyingine

Tax apiga marufuku kwa watazania kujiunga na la Jeshi la nchi nyengine. Alisema kwa mujibu wa sheria zao Mtanzania yoyote haruhusiwi kujiunga na Jeshi la nchi yoyote isipokuwa Jeshi la Tanzaia tu na kufanya hivyo kuvunja sheria za nchi.

---

SERIKALI: ‘Fuateni sheria na taratibu mkiwa nje ya nchi’

View attachment 2495178


Serikali imewataka Watanzania kuzingatia na kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi walizopo ili kulinda taswira nzuri ya nchi yao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Stergomena Tax kuhusu kifo cha Nemes Tarimo, Mtanzania aliyefariki dunia nchini Urusi, alisema:

“Nitoe rai kwa Watanzania kuhakikisha wanazingatia sheria kanuni na taratibu za nchi walizopo, na pia wawe mabalozi wazuri wa kulinda taswira ya Tanzania.

Ikumbukwe kwa mujibu wa sheria zetu, Mtanzania yeyote haruhusiwi kujiunga na jeshi la nchi yoyote isipokuwa Jeshi la Tanzania na kufanya hivyo ni kuvunja sheria,” amesema Waziri huyo.

Amesema Mtanzania huyo alikwenda nchini Urusi mwaka 2020 kwa lengo la kujiunga na Chuo Kikuu cha Moscow Technological University (MIREA) kwa masomo ya Shahada ya Uzamili katika fani ya Business Informatics.

Ameongeza kuwa Mwezi Machi 2022, Mtanzania huyo alitiwa hatiani kwa kuhusika na vitendo vya uhalifu na kwa mujibu wa sheria za Urusi alihukumiwa kifungo cha miaka saba jela.

Waziri Tax ameongeza kuwa Tarimo akiwa gerezani alijiunga na kikundi cha kijeshi cha Urusi cha Wagner kwa ahadi ya kulipwa fedha na kuachiwa huru, baada ya kumaliza muda wa kutumika vita na alifikwa na umauti akiwa nchini humo.

Waziri Tax amesema kuwa mwili wa marehemu umeondoka nchini Urusi leo Januari 24, 2023 na unatarajiwa kuwasili nchini muda wowote kuanzia sasa na kuongeza kuwa Serikali imekuwa ikiwasiliana na Serikali ya Urusi, ili kuhakikisha mwili wa marehemu Tarimo unarejeshwa nchini na kukabidhiwa kwa familia yake kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Waziri ametoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na Watanzania kwa msiba huo.

Waziri Tax amewauhakikishia umma na Diaspora wa Kitanzania wakiwemo wanafunzi walioko masomoni duniani kote kuwa serikali itaendelea kuwapa ushirikiano wakati
matamko mengine ni kuonyesha tu wizara iko hai
 
Kwaiyo ajuhi au ndio kujizima data?

Wengi nawajua wapo US army
 
Kiongozi biti kama izo akawaambie wanawe hatusaidii kitu chochote katika maisha yetu.
 
Wajaribu pia black water mzee nao wanalipa vizuri [emoji1]
Una mafunzo kdg ya kijishi lakini

Ova

Unatafuta ulipo mgambo unapiga miezi mitatu , unapata cheti mengine utajifunzia huko huko lakini idea unakua nayo au unaenda jkt kwa mujibu baadae unajikataa ndio mbinu wengi hutumia kupata mbinu za awali
 
Mbona kibao tu wapo jeshi la Uingereza, USA, nk. Wao wameshindwa kuajiri vijana nchini wanavuka boda yeye atulie hayo ni maneno yake hayamzuii tembo kunywa maji.
Hakuna mtu wa kuacha fursa.
 
Unatafuta ulipo mgambo unapiga miezi mitatu , unapata cheti mengine utajifunzia huko huko lakini idea unakua nayo au unaenda jkt kwa mujibu baadae unajikataa ndio mbinu wengi hutumia kupata mbinu za awali
Hapo sawa

Ova
 
Nchi hii bhna jamaa, ni woga WA mmarekani kisa katia neni kifo cho Memes.

Hivi tutaishi kitumwa hivi mpaka lini!!
Vijana wengi hua na ndoto za kua wanajeshi na mbona hua hamuwapi izo ajira za jeshi alafu mnawazuia.

Na wengine kugikia kuandamana enzi za mwendazake wapewe ajira kama walivo ahidiwa nikiwemo🤔.

Ewe kijana ukiona nchii hii hujaona fursa inayokufaa na unauwezo wa kwenda nchi zingine kutafta na kukamilisha ndoto zako nenda.

Achana na Hawa wapuuzi na uwoga wao uje kukufanya uishi Nje ya future yako.

🖐🏿🖐🏿
 
Nchi hii bhna jamaa, ni woga WA mmarekani kisa katia neni kifo cho Memes.

Hivi tutaishi kitumwa hivi mpaka lini!!
Vijana wengi hua na ndoto za kua wanajeshi na mbona hua hamuwapi izo ajira za jeshi alafu mnawazuia.

Na wengine kugikia kuandamana enzi za mwendazake wapewe ajira kama walivo ahidiwa nikiwemo[emoji848].

Ewe kijana ukiona nchii hii hujaona fursa inayokufaa na unauwezo wa kwenda nchi zingine kutafta na kukamilisha ndoto zako nenda.

Achana na Hawa wapuuzi na uwoga wao uje kukufanya uishi Nje ya future yako.

[emoji1616][emoji1616]
Wanaogopa vijana wengi wakiwa na mentality na maamuzi kama ya nemes
Hawa jamaa zetu wanapenda vijana
Kuwaona wanajiingiza kwenyw mambo ya ubongo fleva na kukata mauno tu

Ova
 
Mbona inaeleweka Tanzania haina due nationality. Siyo majirani zetu leo anakuwa mkuu wa majeshi ya Congo kesho anahama timu anakuwa mkuu wa majeshi Rwanda.
Kwa kujiunga kwao Hawakani Uraia wa Nchi yetu.

Kile kikundi ni kama vile mfano wa Knight supports tu ile Kampuni ya Ulinzi.

Hivyo Wanaojiunga hawalazimiki Kuwa Raia wa Nchi Ya Urusi.
 
Back
Top Bottom