Marufuku Mtanzania kujiunga Jeshi la nchi nyingine

Marufuku Mtanzania kujiunga Jeshi la nchi nyingine

Mshahara kiasi gani kwani. Mfano mtanzania kajiunga jeshi la Russia anapata faida zipi?

R.I.P soldier
 
Nmesema toka mwnzo kijana kama una mawazo ya kujiunga na jeahi fanya hvo.
Hakuna Sheria inayozui Hilo.
 
Mbona kibao tu wapo jeshi la Uingereza, USA, nk. Wao wameshindwa kuajiri vijana nchini wanavuka boda yeye atulie hayo ni maneno yake hayamzuii tembo kunywa maji.
Hakuna mtu wa kuacha fursa.

Wapo huko bado wakiwa ni raia wa tz au wakiwa wamesha chukua uraia wa nchi husika?
 
Kuna jamaa mmoja yupo marekani na yupo jeshini wamchukulie hatua ndo tuone wapo werious au wanasubiri na yy apelekwe kyiv wakamlenkichwa waje kusema tena hapa
 
Mbona katika maelezo uliyoyatoa mama ni kama bwana Tarimo alilazimishwa kuwa 'mercenary' na wala haikuwa hiyari yake?

Iweje hamtoi tamko la kuwalaani hao waliomlazimisha?
 
Hivi kiukweli kijana anawekwa jela huku na kuambiwa tunakuachia lakini ukapigane kwenye vita atachagua lipi? Na inawezekana kalazimishwa. Badala ya kufanya kazi viongozi wetu wanaweka lawama kwa vijana ambao hata hatujui wameingiaje jela huko Russia
Exactly!

Hajui ameingiaje jela

Hajui ameingiaje jeshini

Hajui kama aliomba Uraia wa Russia

Hajui kama alipewa haki zake kisheria

Mwili bado haujafika ushaanza kumchana kavunja sheria! Sheria gani ?

Watanzania hatunaga mtetezi.

Vienna Convention iliwataka polisi wa Russia wampe simu apige ubalozi siku amekamatwa na viji bangi. Ubalozi walijua amekamatwa ? Walipigiwa simu ? Kwa nini hawakupigiwa? Alipewa haki zake ? Au alishinikizwa ? Walimsaidia kisheria ?

Au Waziri nae kashinikizwa kutoa cockamamie statement kama hii ?

Au kalewa madaraka kwa kupata mavyeo ghafla ghafla au hajui kazi yake kama mtetezi wa Watanzania mbele ya dunia ?

Maana haiwezekani hajui hizi protocols. Alikuwa executive wa SADC, akawa mbunge ghafla, akawa Waziri Ulinzi, akawa Waziri Foreign..... Hajajifunza funza protocols za kazi kama hizi ???

Mbona mimi muuza nyama Tandale najua diplomat hupaswi kuwachana raia wako mbele ya dunia ????????

Huyo hakujiunga kwa hiyari yake bali kwa kulazimishwa, Serikali ilitakiwa kutoa tamko kuilaani Urusi kwa inachokifanya hasa kwa wageni maana ni kinyume na haki za binadamu.
Kwani wale Wagner ni jeshi la nchi nyingine au ni “mercenaries”?!

atueleze balozi zetu zinafanya Nini pale watanzania wanapopata matatizo wakiwa nje ya nchi.
Wanahakikisha wanapata mawakili pia wanapata muda wa kuwatembelea ni wazi Kuna uzembe kwenye wizara yake.
Good observation , Kama waziri ingekuwa vyema angetaja kabisa hiyo Sheria na kifungu husika.
Mimi mwenyewe ndio mara ya kwanza
 
Sasa yule mangi si alikuwa mfungwa kule russia. Akalazimishwa kwenda vitani ili apunguziwe adhabu
 
Yani nikiomba kujiunga na jeshi la hapa nakosa nafasi alafu inakuja nafasi ya kujiunga na jeshi huko nchi za mbali eti nikose kwenda eti kisa nitavunja Sheria za nchi?, na iwe hivyo tuu sitokua wa kwanza Wala wa mwisho kuvunja hizo Sheria, tena na uraia naukana hadharani kabisaaaaa hauna dili lolote mjini
Aisee!
"Uraia wa Tz hauna dili lolote mjini"
wabongo noma
 
Shida nyumbani kuingia jeshi ni ngumu kweli, sasa huko nje ka rahisi na mkwanja mrefu hapo ndio kipengele!
 
Back
Top Bottom