Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama utajari naomba link ya hayo matangazo mkuuMbona sijawahi kuona wakikataza au kukemea yale matangazo ya barozi ya marekani wanatoaga kukaribisha vijana wanaotaka kujiunga na jeshi la Marekani kwa mkataba?
Shukrani sanaHata ufaransa wana French legion
Vijana changamkieni fursa
Utakuwa sio raia wa Tz so automatically utaruhusiwaUkijiunga ukahama na uraia?
Bora wangekaa kimya tu yaani kwa press hii ni kama wamewatangaza hao wagner, jamaa wakija bongo kuchukua vijana watawapata wengi sana. Vijana tulivyopigika mtaani alafu tukatae fursa because of the so called kuvunja sheria.! as if hao wanaotupika mkwala mbuzi izo sheria wao wanazifata.Wazalisje ajira za ndani, nipo kwenye mchakato wa kujiunga Wagner PMC
Kuliko ya boss wake?Mama ana macho mazuri[emoji39]
Knight support na hao warusi ni vitu viwili tofauti.Knight support hawavuki mipaka kupigana vita kwa niaba ya Nchi yoyote.Kwa kujiunga kwao Hawakani Uraia wa Nchi yetu.
Kile kikundi ni kama vile mfano wa Knight supports tu ile Kampuni ya Ulinzi.
Hivyo Wanaojiunga hawalazimiki Kuwa Raia wa Nchi Ya Urusi.
Naomba anuani yao mkuuWajaribu pia black water mzee nao wanalipa vizuri [emoji1]
Una mafunzo kdg ya kijishi lakini
Ova
Wagner Group ni jeshi la nchi gani?Ya uhamiaji na makazi. Kama uko interested na majeshi ya nchi zingine, ukane uraia wa tz kisheria then chukua uraia wa nchi husika ambapo utataka kujiunga na jeshi hilo
Dogo utapata laaaaana.Mama ana macho mazuri[emoji39]
Jeshi la Marekani lina Watanzania kibao ambao pia wamepigana vita nje ya Marekani.Tax apiga marufuku kwa watazania kujiunga na la Jeshi la nchi nyengine. Alisema kwa mujibu wa sheria zao Mtanzania yoyote haruhusiwi kujiunga na Jeshi la nchi yoyote isipokuwa Jeshi la Tanzaia tu na kufanya hivyo kuvunja sheria za nchi.
---
SERIKALI: ‘Fuateni sheria na taratibu mkiwa nje ya nchi’
View attachment 2495178
Serikali imewataka Watanzania kuzingatia na kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi walizopo ili kulinda taswira nzuri ya nchi yao.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Stergomena Tax kuhusu kifo cha Nemes Tarimo, Mtanzania aliyefariki dunia nchini Urusi, alisema:
“Nitoe rai kwa Watanzania kuhakikisha wanazingatia sheria kanuni na taratibu za nchi walizopo, na pia wawe mabalozi wazuri wa kulinda taswira ya Tanzania.
“Ikumbukwe kwa mujibu wa sheria zetu, Mtanzania yeyote haruhusiwi kujiunga na jeshi la nchi yoyote isipokuwa Jeshi la Tanzania na kufanya hivyo ni kuvunja sheria,” amesema Waziri huyo.
Amesema Mtanzania huyo alikwenda nchini Urusi mwaka 2020 kwa lengo la kujiunga na Chuo Kikuu cha Moscow Technological University (MIREA) kwa masomo ya Shahada ya Uzamili katika fani ya Business Informatics.
Ameongeza kuwa Mwezi Machi 2022, Mtanzania huyo alitiwa hatiani kwa kuhusika na vitendo vya uhalifu na kwa mujibu wa sheria za Urusi alihukumiwa kifungo cha miaka saba jela.
Waziri Tax ameongeza kuwa Tarimo akiwa gerezani alijiunga na kikundi cha kijeshi cha Urusi cha Wagner kwa ahadi ya kulipwa fedha na kuachiwa huru, baada ya kumaliza muda wa kutumika vita na alifikwa na umauti akiwa nchini humo.
Waziri Tax amesema kuwa mwili wa marehemu umeondoka nchini Urusi leo Januari 24, 2023 na unatarajiwa kuwasili nchini muda wowote kuanzia sasa na kuongeza kuwa Serikali imekuwa ikiwasiliana na Serikali ya Urusi, ili kuhakikisha mwili wa marehemu Tarimo unarejeshwa nchini na kukabidhiwa kwa familia yake kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Waziri ametoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na Watanzania kwa msiba huo.
Waziri Tax amewauhakikishia umma na Diaspora wa Kitanzania wakiwemo wanafunzi walioko masomoni duniani kote kuwa serikali itaendelea kuwapa ushirikiano wakati
Ya uhamiaji na makazi. Kama uko interested na majeshi ya nchi zingine, ukane uraia wa tz kisheria then chukua uraia wa nchi husika ambapo utataka kujiunga na jeshi hilo
Hapana ,Marekani kama una visa ya ukazi wa kudumu au permanent residency status inaingia jeshini na kuwa mwanajeshi na vita unapigana kama active combat soldier , si lazima ibadilishwe uraia ,watu wengi hawajui hiliNa lazima atakuwa raia wa marekani
Tayari huyo
Ova
Hivi kiukweli kijana anawekwa jela huku na kuambiwa tunakuachia lakini ukapigane kwenye vita atachagua lipi? Na inawezekana kalazimishwa. Badala ya kufanya kazi viongozi wetu wanaweka lawama kwa vijana ambao hata hatujui wameingiaje jela huko RussiaTax apiga marufuku kwa watazania kujiunga na la Jeshi la nchi nyengine. Alisema kwa mujibu wa sheria zao Mtanzania yoyote haruhusiwi kujiunga na Jeshi la nchi yoyote isipokuwa Jeshi la Tanzaia tu na kufanya hivyo kuvunja sheria za nchi...
Yeah ! hata France pia Wana kikosi cha kijeshi cha wapiganaji kinachojumuisha wapiganaji raia toka nchi nyingine ,na masharti ni rahisi ni wewe kuingia tu pale France na kuingia headquarters kuenlist then unaingia kufanya test , au mtihani wa kupima utimamu wa mwili then mnaingia bootcamp ,Ila bootcamp lake si la kitoto ,kama wewe ni mlenda mlenda au urojo lazima uikimbie au wakuteme ,so hiyo kuingia jeshini na uraia wa nchi nyingine kwa wenzetu ni kawaida kabisaMi namjua mmoja yupo France legion
Huyu Mama nadhani kakurupuka
Ni vitu viwili tofauti lakini ni Muktadha Sawa kwamba yote ni kama makampuni ya Ulinzi ila Moja inashiriki Vita Kwa ajili ya Nchi yake.Knight support na hao warusi ni vitu viwili tofauti.Knight support hawavuki mipaka kupigana vita kwa niaba ya Nchi yoyote.