Marufuku ya kusafirisha abiria usiku yapingwa vikali

Marufuku ya kusafirisha abiria usiku yapingwa vikali

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mwenyekiti wa Chama cha Wenye Matatu. Dickson Mbugua aikejeli NTSA kupiga marufuku safari za usiku.

Akizungumza na waandishi wa habari, Bw, Mbugua amesema marufuku hiyo ni kinyume na azma ya serikali kuweka miundombinu ya uchumi wa saa 24.

Aitaka NTSA kuondoa marufuku hiyo mara moja!
MATATU.jpg
 
Usafiri wa usiku ambao ni salama kwa halaiki ni usafiri wa treni, meli na ndege.. Huu wa mabasi, hapana.
Mimi huwa nasafiri masafa marefu usiku ila huwa naona jinsi kulivyo na hatari nyingi.
Usafiri wa mabasi usiku, si salama kwa halaiki.
 
haya Kenya tunawasikiliza, sisi faida na madhara ya kuTotembea usiku na Mabadi tunayaona, ajali zinapungua, lkn kazi ya siku moja hufanya siku 3, kuna kulsla guest, njiani tochi kibao, zebra na matuta, hebu gangamaleni tupo nyuma yenu
 
Huyu waziri wa usafiri angepiga marufuku usafiri wa usiku kwa mabasi mwezi wa Desemba tungemuelewa. Sasa hivi ni too late na hii sasa ni hujuma tu kwa wanabiashara. Hao Matatu owners Association naamini watafika mahakamani ili waanze shughuli ya kutupilia mbali agizo hilo la waziri Macharia.
 
Huyu waziri wa usafiri angepiga marufuku usafiri wa usiku kwa mabasi mwezi huu wa Desemba tungemuelewa. Sasa hivi ni too late na hii hujuma tu kwa biashara. Hao Matatu owners Association naamini watafika mahakamani kutupilia mbali agizo la waziri Macharia.
Kaka japo ajali zinaongezeka mwishoni mwa mwaka, lakini hata miezi mingine pia zinatokea, kumbuka hata wakifa watu watano ni hasara kubwa, chukulia ni mkeo au mzazi wako, kutembea usiku kunawapa uhakika wa kutokutana na polisi wa barabarani, hivyo kuendesha apendavyo, pigeni marufuku mtaona ajali zitakavyopungua, kwa mfano huku Tanzania kipindi hiki cha mwisho wa mwaka, ni ajali moja tu ya bus iliyotokea na kupoteza maisha ya watu saba, ukilinganisha na huko Kenya, zaidi ya watu 300 wamekufa ndani ya siku 40
 
Marufuku ya safari za usiku sijaona impact yake kubwa ukichukulia mfano way Tz ambao tumekuwa tukisafiri mchana kwa zaidi ya miaka 20 sasa.

Iwapo serikali ina mpango wa kuimarisha miundo mbinu na kuwa ya kufanya kazi kwa saa 24, marufuku hiyo haina faida yoyote kwa sasa.

Zaidi waangalie mambo mengine kadhaa ambayo uchangia kuwepo kwa ajali ambayo yanaweza kurekebishika pasipo marufuku hiyo.
 
Kaka japo ajali zinaongezeka mwishoni mwa mwaka, lakini hata miezi mingine pia zinatokea, kumbuka hata wakifa watu watano ni hasara kubwa, chukulia ni mkeo au mzazi wako, kutembea usiku kunawapa uhakika wa kutokutana na polisi wa barabarani, hivyo kuendesha apendavyo, pigeni marufuku mtaona ajali zitakavyopungua, kwa mfano huku Tanzania kipindi hiki cha mwisho wa mwaka, ni ajali moja tu ya bus iliyotokea na kupoteza maisha ya watu saba, ukilinganisha
Msimu huu wa krisimasi ajali huwa nyingi sana Kenya ukilinganisha na miezi mingine. Kaunti tafuti zinajaribu ziwezavyo kua na uchumi wa 24/7. Hili agizo la waziri Macharia ni la muda tu.
 
Hamna namna, zipigwe marufuku tu na poleni kwa wanabiashara, hivi vifo vya halaiki vimetuchosha. Usafiri wa mabasi hata mchana huwa hatari sana, sipendi kabisa na huwa nasafiri pale ikitokea sina namna. Nakumbuka kipindi nasafiri kutokea Dodoma hadi Tabora mida ya mchana, nikasinzia halafu ghafla nikakurupushwa na mayowe ya kina mama maana basi liliyumba na nusra ligongane na lori kichwa kwa kichwa, yaani hiyo siku nilikwepa kifo kama nakiona mubashara.

Naomba serikali iharakishe SGR safu ya Naivasha na Kisumu ili tuondokane na haya mabasi, madereva wenyewe huwa kama vichaa fulani.
 
Msimu huu wa krisimasi ajali huwa nyingi sana Kenya ukilinganisha na miezi mingine. Kaunti tafuti zinajaribu ziwezavyo kua na uchumi wa 24/7. Hili agizo la waziri Macharia ni la muda tu.
Hivi unadhani kwanini tuliamua kupiga marifuku safari za usiku?, sababu ni hiyo hiyo ya ajali kuwa nyingi, haina uhusiano wowote wa uchumi wa 24/7, kaka kama wewe ni dereva utakubaliana na ukweli kwamba usiku ni ngumu sana kwa sababu vision na taa zinazokuja opposite zinakuchanganya, malori yanayoharibika njiani bila kuwekwa alama.

Acheni kuthamini uchumi kwanza, miwe mnajali maisha ya watu wanaoteketea, sikitegemea kama kingekuwa na mkenya anayepinga hatua za kuokoa maisha ya watu kwa kisingizioa cha uchumi wa 24/7, hasa kipindi hiki ambacho ndani ya mwezi mmoja wamekufa wananchi wengi kuliko au sawa na miaka yote ya KDF kuwepo Somalia, ni vizuri mkajifunza kwa waliofanikiwa.
 
Kwa miundo mbinu yetu ya barabara ni risk sana kusafiri usiku, na hata ukifika salama ni kwa Kudra za mwenyezi Mungu tu lkn si kwa barabara hizi,.
 
Back
Top Bottom