Marupurupu ya Spika yanawavutia wengi kugombea

Marupurupu ya Spika yanawavutia wengi kugombea

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
Sifa kuwa Spika,

Ni uwe na sifa za kugombea ubunge tu. Wenzetu wanawapima elderly senior statesmen ambao wana track record nzuri kiutawala na kisiasa.

Hapa kwetu wagombea watauana, wengine wataenda hata kwa waganga wa kienyeji.

Yale marupurupu ya;
  • 80% mshahara wa Spika
  • Vieite (V8)mpyaa
  • Dereva wa serikali mpaka uchoke mwenyewe
  • Malipo bulungutu heavy
Na mengine mengi.
Ukiona hata mwanafunzi anataka kuwa Spika, basi vigezo vina matatizo.

CCM mmetufikisha kwenye huu upuuzi, mpaka jana jioni kokoro lilishavuta watu 66.
 
Kiukweli kinachowasukuma wengi kuitafuta hiyo nafasi ya uspika kipaumbele chao sio kuwatumikia wananchi; wala sio kulitumikia taifa; wala hawana nia kivile kuona taifa linasonga mbele; priority #1 kwao ni mshahara, posho, marupurupu na pensheni itokanayo na nafasi ya Spika pamoja na hadhi ya kutoshtakiwa popote.
 
Hata kama jamani, ndio hadi Mwijaku na Steve Nyerere? Kweli?
 
Tukiikomboa nchi haya yote yatakua reviewed pamoja na yake mahekalu wa ayojengeana.
... nchi itakombolewaje bila kifaa muhimu cha kazi ambacho ni Katiba ya Wananchi? Wanaofaidi keki hawaitaki; wako tayari kutumia mitutu kuhakikisha haipatikani.

Ni lini tutampata mzalendo wa ukweli hata kutoka huko huko CCM alikomboe taifa dhidi ya walafi? Tulitegemea mzalendo JPM angetuvusha angalau kwa kuweka mifumo badala ya personalities; matarajio yaliyeyuka ghafla kama theluji.
 
Wanasiasa hasa wabunge wamegoma kabisa kupunguza mishahara na marupurupu yao japo kila siku wanaimba watanzania wajiajiri, ndio maana sasa kila mmoja anataka kukimbilia huko.

Makamu wa Rais kawaambia waache kulogana lakini sidhani kama watamsikiliza kwa hali ilivyo, kila mmoja anataka kuhudumia tumbo lake na bungeni ndio sehemu sahihi yenye huduma muafaka, sio kutumikia watanzania uongo mtupu.
 
... kiukweli kinachowasukuma wengi kuitafuta hiyo nafasi ya uspika kipaumbele chao sio kuwatumikia wananchi; wala sio kulitumikia taifa; wala hawana nia kivile kuona taifa linasonga mbele; priority #1 kwao ni mshahara, posho, marupurupu na pensheni itokanayo na nafasi ya Spika pamoja na hadhi ya kutoshtakiwa popote.
Hilo limejionyesha fika.
CCM waanze kufikiria merits za utumishi wa hiyo nafasi, siyo kama ilivyo sasa.
 
Sawa hatukatai ,ila ndo mwijaku na steve nyerere wachukue fomu kweli.....!!!???.
Hao jamaa vilaza wawili, pamoja na msukuma kugombea uspika, inaonyesha just how low siasa za nchi hii zimefikia.

Kulundika mahela na kinga ya kutoshtakiwa, basi kila mjinga atakitaka hicho cheo.

Tatizo hata CCM hawajui wajibu wa Spika kwa Taifa, kisiasa.
 
Ukiwa speaker ni Bata na hata baada ya kua speaker bata linaendelea...
 
Back
Top Bottom