Marvel Cinematic Universe special thread

Dah Ndio maana story naona siipati kabisa kwenye.
Nimeangalia zote Black Widow, Shang Chi R, Eternals ,Spider-Man: No Way Home , Doctor Strange in the Multiverse of Madness ,Thor Love and Thunder ,Black Panther Wakanda Forever, Ant-Man and the Wasp Quantumania ila naona hazina link up ngoja nianze kucheki hizo series ulizorecommend taratibu.

Kilichonifanya niamue kuangalia movie tu za marvel bila series ni sababu i grew up watching Star war Universe na Star trek Universe na nikawa Marvel nnaangalia movie moja moja last year ndo nikaanza kuangalia kwa mfuatano kufuata release date.

Tatizo linakuja Star War Universe na Star trek Universe wana a lot of movies and series having interconnected storyline with a vast timeline wanatoa almost series 4 kila mwaka. Itabidi nijibalance niangalie taratibu MCU.
 
Kwenye hii multiverse saga series ya muhimu mpaka Sasa NI Loki na what if ,sema uzuri wanajua Sio watuwengi wanachecki series ko matukio huwa wanaya refer ,ila ukitaka unaweza cheki recap yt
 

itabidi nikucheki kwa maelezo ya MCU[emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119]
 
Wakuu naomba msome hii comment nikitulia kuna kitu nitakuja kuelezea. Nahisi GOTG itakua connected na muvi ya The Marvels.
Nitakuja kueleza how...

 
GALACTIC RECORD!

'Guardians Of The Galaxy Vol 3' enters the Guinness Book of Records as the film that most makeup prosthetics used, being over 22,500..

 
Sure mkuu haya mambo yao ya Multiversal yanachanganya sana basi tu
 
Mkuu Da'Vinci hebu nipe full details za iron man kama atakuwepo tena kwenye movies yaani yaliyopita,yaliyopo na yajayo kumhusu yeye na uigizaji wake.
Ninamkubali sana mwamba.


Nitashukuru sana.
 
Mkuu Da'Vinci hebu nipe full details za iron man kama atakuwepo tena kwenye movies yaani yaliyopita,yaliyopo na yajayo kumhusu yeye na uigizaji wake.
Ninamkubali sana mwamba.


Nitashukuru sana.
Swali lako umeliweka katika aina mbili. Nikupe details za mwigizaji Robert Dwayne Jr pia nikupe details za character Iron Man.
Kevin Feige alisema kwamba phase 5 haiatahusu maswala yaliyotokea kwenye phase 3 (endgame). Kwamba wana move on.
So habari za fallen heroes zitabaki huko. But tupo kwenye Multiverse saga, kila kitu kinaweza kutokea kwenye multiverse usishangae kumuona Nicholas Cage kama John Blaze/Ghost Rider 2008
So usishangae kumuona tena Iron man As alternate character of earth 616
 
Ok finally nimepata wasaa wa kuelezea
Kama mmeona Post credit scene ya GOT imeonyesha kundi jipya la GOTG likiwa na Rocket, Groot, Cosmo, Kraglin, Adam, Phyla.

Si mnakumbuka niliongelea kuhusu mtu mmoja anaitwa Mar-veill kwenye muvi ya captain marvel 2019 alitumia jina la Dr.Wendy Lawson. Huyu Marvel ana watoto wawili wanaitwa Genis-Veill na Phyla-veil. Huyu phyala ndio kaonekana kwenye muvi ya GOTG. Kwenye comics phyala ni member wa Guardians, hivyo basi naamini hajaonekana kwa bahati mbaya kwenye hii muvi inawezekana atakuwepo kwenye The Marvel 2023 au GOTG itakua inahusiana na The Marvels .
Ngoja tusubiri November
Wakuu naomba msome hii comment nikitulia kuna kitu nitakuja kuelezea. Nahisi GOTG itakua connected na muvi ya The Marvels.
Nitakuja kueleza how...
 
Oooi! ila bado kwenye tasnia ya uigizaji yumo kwenye siku za usoni maana uhusika wake naupenda sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…