Marvel Cinematic Universe special thread


acting anaweza sana ndg yake Casey performance ya ile Manchester by the sea ilikuwa outstanding, ndio maana alipata oscar I think
 
Sasa hivi mrvel tupo phase ya multverse mimi nahisi wale waliofariki kama iron man na black widow watakuja wenzao ambao wanao fanana nao kutoka earth nyinginekama tumeona dr strange antokea mtu alifanana nae au spiderman tumeona wametoke watatu mimi nadhani watakuja nao
 
Namimi nawaona watu wapuuzi sana wanaopenda bia na Mpira. Unapataje kiu ya pombe au mpira???
Muvi tunapata vingi vya kujifunza
Hapo kwenye Mpira sasa ndo penyewe Jamaa kashindwa kabisa kuvumilia sii akaushie kama tunavyo kausha kwenye Uzi wa rikiboy..... Kila mtu ana starehe zake Bhana.
 
Hebu twende mbele turudi nyuma. Nini maoni yako kwenye movie ya Eternals. Naona inafanya si vizuri sana kama ilivyotegemewa. Nini shida ??
 
Hawa jamaa wanafikilia mbele sana utashangaa uko mbele utaipenda kama mm nilikua simuelewagi dokta strange ila sasa hivi naanza kutafuta movie zake
 
Nionavyo mimi, hii ingefaa sana kama ingekuwa series.

Kweli huwez ku introduce characters wote wale kwa masaa mawili na uwafanyie character development actions ziwemo pia.. ni kitu kigumu

Wangeweka series halafu episodes ziwe chapters za kumuelezea mmoja baada ya mwingine ingekuwa interesting
 
Hawa jamaa wanafikilia mbele sana utashangaa uko mbele utaipenda kama mm nilikua simuelewagi dokta strange ila sasa hivi naanza kutafuta movie zake
Hawa jamaa ni noma ndio utaona wazungu sio wenzetu kabisa. Mfumo wao ni kwamba hua creative team wakiwemo Trinh Tran, Nate Moore, Jonathan Schwartz, Brad Winderbaum, Stephen Broussard, Eric Carroll Na Ryan Meinerding wakiongozwa na Kevin Feige, Victoria alonso na Lois de'Espocito hua wanakaa wanajadili labda Phase 4 iwe na characters fulani na ihusu masuala fulani kisha wanaajiri developer/Creator sasa kila mmoja anapewa characters wa kuwafanyia kazi.

Mfano Sean gunn yupo na GoG, Taika waititi yupo na thor, Nia Dacosta yupo na Capt Marve nk. Sasa wanatunga story kila mmoja kivyake ila katika hizo story wanaangalia jinsi ya kuzihusianisha na muvi zingine ndio maana unakuta Characters kutoka muvi zingine wanakua kwenye muvi fulani. Mtengenezaji wa WandaVision Jac Scheifer alikua anafaya kazi pamoja na mtengenezaji wa Doctor Strange Michael Waldron
 
Hebu twende mbele turudi nyuma. Nini maoni yako kwenye movie ya Eternals. Naona inafanya si vizuri sana kama ilivyotegemewa. Nini shida ??
Nimepata uvivu kuiangalia kwa jinsi ilivyopondwa. Labda tupate maoni ya walioiona hapa.
 
Asee ebu mnieleweshe hapa kwa Spider Man no way home, wale jamaa waliokuja kutoka sijui wapi si katika movie wamekufa mfano yule mwenye machuma ya miguu alifia kwenye maji, na huyu mwenye kigari kinachopaa aligongwa na hicho kigari kilikuwa na mikuki sijui, sasa humu wazima imekuwaje
 
Hebu twende mbele turudi nyuma. Nini maoni yako kwenye movie ya Eternals. Naona inafanya si vizuri sana kama ilivyotegemewa. Nini shida ??

Nimepata uvivu kuiangalia kwa jinsi ilivyopondwa. Labda tupate maoni ya walioiona hapa.
Nimeitazama jana hii muvi kiukweli haina mvuto kiivyo na story yake hovyo. Fight scene zilizonivutia ni Makkari kaupiga mwingi sana humo kuliko wengine. Anyway labda tungoje mwendelezo unaweza kua bora maana hata Thor Dark world na Iron man 2 zilikua hovyo
 

asaidiwe huyu mtu mm sion hata pa kuanzia... msipite tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…