Marvel Cinematic Universe special thread

Our berry Allan ndio tulimpenda,sasa kama wana badilisha itakua shida nyingine
 
Sasa nawaza kutakua na second season au walikua wanajifurahisha tu huko studio??

niliwaza nkasema ile itakuwa ni zile homework alizokuwa anaacha mwalim mjisahishie wenyewe😅
Season 2 ipo matayarishoni mzee. Kama season 2 ya what if..? Imeanza kuandaliwa 2019 kabla ya S1 kutoka muda huu wapo wanaandaa S3. Loki S2 wameanza kuindaa 2020
 
Nimemiss kujibu maswala.. Mwenye swali lolote la kuhus Marvel Universe aulize
I'm happy to comply ✌️
Kuna jambo linalonitatiza kuhusiana na Multiverse. Ukiwaangalia spiderman wa Universe nyingine ni tofauti kabisa ki sura na kiumbo na spiderman wetu.

Lakini sasa kwenye MOM wao wanafanana japo sio exactly.
Sasa swali langu Kwa nini kina spiderman wametofautiana sana?
 
Ok ishu ni ya Casting tu na hakuna utofauti wowote. Spider-man wwnatofautiana kwakua kulikuwepo actor waliowahi kuigiza kama spiderman lakini upande wa doctor strange muvi ya kwanza imeigizwa miaka ya 70s so kwasasa Nadhani kazeeka sana kama hajafariki.

So right kama kungekua hakuna watu waliowahi kuigiza muvi ya spiderman basi ingebidi Tom Holland aigize nafasi zote kama alivyofanya Doctor strange.

Lakini pia Kuwaleta wale spiderman wa mwanzo ilikua ni strategy ya kuwinBox office kwa kuwaHype watu (Nostalgia)
coz watu tuliwamiss kuwaona na tulipenda kuwaona pamoja. Strategy ilifanya kazi mpaka sasa NWH ni muvi ya sita iliyouza zaidi duniani.
Je nimeeleweka??

Doctor strange na Clea wa muvi ya 1978.
 
NWH ilikuwa ni fan service movie
 
Elezea The thunderbolts
Kwanza kabisa naomba nitumie post hii Kumtakio pumziko la milele bwana William Hurt. Natumaini mnafahamu william hurt kafariki mwaka huu kwa maradhi.

Mkuu Thunderbolt ina mlolongo mrefu sana ila Nitajitahidi kuwaeleza kadri ya ninavyofahamu. Kwanza kabisa hili ni kundi linaloundwa na Supervillain na Antiheroes Ambalo linakua linatumiawa na serikali katika shughuli mbalimbali ni kama vile kundi la Suicide Squad.
Kuna makundi mbalimbali ya Thunderbolt yaliyowahi kuanziswa na Baron Zemo, Luke Cage, Justine H.a.m.m.e.r, Winter Soldier, Punnisher na Red Hulk.

Kuna mkuu anaitwa General Thaddeus E Ross aka Thunderbolt huyu jamaa ni General wa jeshi la marekani ambae pia ni baba wa mkee wa Bruce Banner aitwae Betty Ross. Huyu ndie aliigizwa na Marehemu William Hart kwenye muvi za Incredible hulk, Captain america na Avangers.

Sasa kuna gereza linaitw The Raft tuliliona kwenye muvi ya Civil War, hili gereza hua wanafungiwa Superhero waliofanya makosa na Supervillain. Sasa General Thaddeus E Ross alikua anawachukua Supervillain na Antiheroes kwenda kufanya shughuli zile wanaita Black Operation

NB. Thaddeus Ross Ndio Red Hulk pia.
Mkuu imebidi nifupishe maana hapa ilitakiwa niongelee hasa Baron Zemo na kundi lake la Master of Evils pia ilitakiwa niongelee Dark avangers na vifo vya Avangers na Fantastic Four vilivyosababisha kundi la master of evil kujifanya Thunderbolt/Dark avangers

Lakini kama uliona mwisho wa series ya Falcon and Winter soldier Barob Zemo alipelekwa The Raft. Kuna maana kubwa sana hapo kuhusu muvi zijazo
 
Detail niliyoigundua leo nilipokuwa nairudia THE INCREDIBLE HULK 2008 kwenye final fight against Abomination. Kuna restaurant moja inaitwa ZANZIBAR 😁😁
 
Character wote waliokuwepo kwenye Muvi ya Captain Marvel ni young version za character waliopo leo. Ndio maana Ronan the Accuser alifariki kweye Guardian of the Galaxy 2014 ila kwenye Captain Marvel walikuwepo. Ndio maana Nick Fury anaonekana mdogo coz ile muvi imeisetiwa miaka ya 94
 
Hivi nitoe mfano ni nani mwenye nguvu kushinda wote pale Marvel!?
Kwa sasa unaweza kuona Scarlett Witch ndio mwenye nguvu zaidi. Lakini kuna mdaa anaitwa Jean Grey kutoka X-Men ni noma. Kuna Maria Rambou,Thor na Carol Denver they're so strong. Kuna mtu anaitwa Wonderman wako wanamtengenezea series yake ngoja utamuona he's so powerful balaa
Je mimi nikiwa na nguvu kama za superman naweza kurogwa na uchawi huu wetu nikarogeka au itashindikana😁
Inawezekana maana uchawi hua haungalii nguvu za mwili bali nguvu ya akili. Thor ana nguvu lakini aliweza kurogwa na Scarlett Witch kwenye age of ultron. Loki hawezi kurogeka coz ana Powerful mind. Kuna uzi wangu mmoja unasema Mental illusion Projection nimeeleza jinsi mchawi anavyoweza kukuroga.

NB. Hivi ubaposema kurogwa unamaanisha Kupogwa Juju,zongo,kipapai nk??? Maana huko sio kuroga kiuhalisia.
 
Ni kweli WB hawana mpango wa kumrudisha Henry Cavil wala Zack Snyder.
Kuanzia Zack,Henry,Ezra, Raymond Fisher,Ben Affleck hawa wote wanapigwa chini haijulikani watarudi au lah.
Wamebaki Gal Gadot na Jason Momoa
Zack hawez kuondoka Dc akiondoka na dc ndo imekufa ben affleck wanerb walitasema atakuwepo kwenye aquaman lost kingdom ya mwakan
 
Kwenye spider-man no way home kwa nini wale maadui walioneka wapo hai tena wakat walikufa kwenye movie zao
Mkuu kama nilivyosema mwanzo ukweli ni kwamba hakuna sababu za msingi zinazoelwza kwanini wamekua hai wakati walikufa kwenye muvi zao. Kwa kulijua hilo ndio maana wakaweka stori imekaa kwamba Walionekana kabla ya kutokea matukio ambao yalipelekea wao kufa ndio maana Peter 1 alikua anapambana awatibu kwanza kabla ya wao kurudi ili wasiende kufa kwenye universe yao.

Kwa ishu ya multiverse hiyo inawezekana lakini kama ingekua ni Tine Traveling basi kungetokea matatizo maana Peter 1 angekua ameharibu Time line.

Kwenye Theory of General Realativity ukifanya Time traveling kurudi Past huruhusiwi kubadiri chochote kile yaana hata kuhamisha kiti au glasi ya maji tayari unakua umeharibu Timeline/Mtiririko wa matukio katika muda husika.
 
Nimekuelewa Mkuu, kumbe movie ya kwanza ya Doctor Strange ilitoka kitambo namna hiyo.
 
Nimekuelewa Mkuu, kumbe movie ya kwanza ya Doctor Strange ilitoka kitambo namna hiyo.
Zipo nyingi za zamani mkuu kipindi hicho marvel ilikua haipendwi upande wa muvi kila muvi zao zilifanya vibaya. Ndio maana baadhi ya character waliuzwa kama Hulk,Xmen kwa Fox na Spiderman,Venom,Morbius kwa Sony.

Ilifika hatua wakataka kuuza character wote kwa Sony. Sony walikataa kuwanunua kwamba hawapendeki na hawana soko . Baadae miaka ya tisisni mwishonu ndio Marvel wakatoa muvi ya Blade. Hii muvi ndio ilingiza pesa kiasi zilizosaidia kuanzisha Marvel Studio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…