Mkurugenzi wa Kismaty Advert Media Company Ltd, Bi Mary Mollel, mfanyabiashara kutoka mkoa wa Arusha, amekimbilia Umoja wa Mataifa kuomba msaada kutokana na hofu ya usalama wake na wa familia yake. Bi Mollel anadai kuwa tangu mwaka 2022 amekuwa akipokea vitisho mbalimbali, hali iliyosababisha ndugu zake wawili kuuawa kikatili mwaka uliofuata, mara tu baada ya kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha.
Amesema kuwa licha ya kuomba msaada, bado hajakata tamaa, ingawa anaamini uongozi wa juu huenda haujui kuhusu hali yake kutokana na baadhi ya viongozi wanaodaiwa kuhusika katika uhalifu huo kuzuia upatikanaji wa msaada. Katika barua yake ya awali kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, Bi Mollel aliweza kufafanua chanzo cha matatizo yanayomfanya aishi kwa kujificha kwa zaidi ya miaka mitatu.
Aidha, kwenye barua hiyo, aliwataja baadhi ya viongozi pamoja na msanii Marioo na uongozi wake, ambao walifungua kesi ya madai dhidi yake, hali iliyomlazimu kuishi kwa tahadhari kubwa.