Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Ni wazi kauli ya mbowe inayosubiriwa kwa hamu na gamu kubwa sana na wana chadema na taifa kwa ujumla, atakayoitoa mbele ya waandishi wa habari, ndani ya masaa 48 yajayo, itaamua mustakabali, uelekeo na myukano wa kisiasa wa aina ya kitofauti mno ndani ya chadema kuelekea uchaguzi wa ndani ya chama hicho cha siasa ngazi ya taifa.
Kauli hiyo,
inatarajiwa kurejesha ari mpya kwa wanachadema na kuleta pumzi mpya, kuimarisha umoja ndani ya chadema, kuamsha matumaini mapya na ya uhakika dhidi ya uhai, afya, ustawi na uimara wa chadema kitaifa, kama chama madhubuti cha upinzani chenye malengo ya kitaifa na kimataifa.
Kauli ya Mbowe inatarajiwa kua mwibwa kwa wenye mitazamo tofauti na dhamira yake ya kugombea uenyekiti wa chadema taifa, na kwa kiasi kikubwa inaweza kuzidisha mbinyo kwa baadhi ya wagombea hususani kwa nafasi ya uenyekiti Taifa, kujiondoa mapema kabla ya siku ya uchaguzi huo muhimu, kwa vizingizio mbalimbali.
Hali hiyo inatazamiwa pia,
kurahisisha upatikanaji wa mgombea urais wa chama hicho uchaguzi mkuu mkuu ujao oct.2025, bila kua na makundi wala migawanyiko isiyo kua na lazima, kwasababu, huenda watu wa makelele na midomo watakua wameshatulia na kupoteza uelekeo kabisa kwenye medani za siasa Tanzania.
Unadhani ni viongozi gani chadema wanaweza kusukumwa nje ya ulingo wa mapambano ya kuendelea kua wagombea uongozi na kauli ya Mbowe ndani ya masaa48 yajayo?
Mungu Ibariki Tanzania