Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu


Mkuu, labda nikuulize suali moja tu.

Je, ni kwanini askari mwingine alikuwa akihangaika kumtuliza yule askari ambae alifyatua risasi hewani?
 
Kumbe kapiga risasi ushabiki, kisa kaambiwa hana mamlaka... Dah, vijana wamekosa weledi wa kazi... Mtu kaweka mikono mfukoni kabisa wewe ka li 10Kg unajiona mwanaume....
Ni kosa usirudie kufanya utakuja kuvunjwa miguu au mikono kama sio kufa. Ukiona MTU ana silaha kesha koki toa mikono mfukoni ipandishe kichwani.
Ukiacha mikono mfukoni atajua unatoa cha moto.
Acha kabisa.
 
 

Attachments

Sasa si angemjaza tu risasi kwanini alikuwa anaongea tu?
We unaona mwisho wa siku nani kachukua credit pale?
Unafoka tu halafu unaondoka?
Yes leo kapata credit waziri... ila polisi angempa 5 za kichwa tungepata sababu ya kuitukana CCM ila jamaa angepata credit mbinguni. In my normal life siwezi kubishana na polisi. Most of them ni serial killers waliojificha huko ili waue kirahisi.
Kazi gani unajifunza kuua, kugombana, kukimbiza ... kesho tunataka wawe na busara
 
Yaweza kuwa akili yako ndio haipo vizur kwahyo kisa alikua kiongozi ndio avunje baadhi ya sheria za inchi du kweli wabongo wakati mwingne mantaka kuonewa kisa mtu alikua kiongozi nyie mwaona sawa tu
 
Ilianzia clouds,ikaja kwa nape na sasa malima twende tu
 
Ukisikia mwalimu anamfokea kwa nguvu mwanafunzi ati KWANINI HUNIHESHIMU,.....jua Mkuu wa shule aidha analewa gongo au ni swahiba wa mwanafunzi!!

"Kwanini hamuiheshimu seriikali??!!!.."...Hili ni swali la mtu aliyekata tamaa!!!

Mithali 27: 12 Jiwe ni zito na mchanga ni mzigo,
lakini kukasirishwa na mpumbavu ni kuzito
zaidi kuliko hivyo vyote viwili.
 
Hawa ni vijana waliopo chini ya wizara yako ndugu Mwigulu Nchemba

Nchi yetu haijafikia huko walikofika hawa walinzi wetu, kitendo hiki sio cha kiaskari!
Pengine yeye mwenye dhamana anafurahi,ila ipo siku wataumia hawa askari na ccm kwa ujumla.
 
Wewe unaonaje polisi wako katika majukumu yao wanaomba wapishwe ni sahihi au sio sahihi?
 
SERIKALI INATOKANA NA WANANCHI,IPO KWA AJILI YA WANANCHI,WENYE NAYO NI WANANCHI,WATUMISHI WA SERIKALI NI WATUMISHI WA WANANCHI HIVYO WANANCHI NDIO SERIKALI.
 
mwenzake alikuwa anatuliza jazba ila he had a reason ya kuwa na jazba kama husikilizwi unapotoa amri halali
Hata mimi siwapendi polisi ila kuna mahali siwapendi viongozi wanaojidhani ni above the law


Hii ndio society tuliyo ijenga, non-mannered. Wote wana makosa lkn polisi ana makosa zaidi, hutumii silaha namna hiyo hata siku moja.
 
Mh Mwigulu upo humu kama waziri. Tujiulize sie tulibarikiwa kwenda nchi za wenzetu police suala la kwanza anatakiwa akusaidie kama raia na sio kukihukumu.

Huyu askari anainesha ni muhuni anajibu majibu kana kwamba kazi ya upolisi alilazimishwa kwa njaa zake.

Hapo ni masaki IOM front kabisa ya Double tree kitovu cha wageni watalii na wawekezaji wanaokuja nchini mwetu hii inaleta picha gani kwa wageni. Mimi nilishawahi kupita kwenye nyekundu nchi za watu likuwa j2 na askari alinihoji na kujuà mgeni akaniambia usirudie hata kama hakuna mvukaji

Kwa kweli tunahitaji wasomi zaidi ambao wataleta civilisation kwenye jeshi letu la police
 
angewapisha tyu wapite maana km walikuwa wanawahi kuokoa mali au uhai wa watu?
 
Kila nikitazama ile clip, waswasi wangu ulikuwa kwenye ile AK47 recoil, yule askari ilimshinda kuishika kwa mkono mmoja, angeweza uwa watu pale, kweli akili ni nywele, yawezekana hawa ndiyo wale wenye vyeti bomu, sijaona sababu ya aina yoyote kupiga juu risasi, yale yale...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…