Poise
JF-Expert Member
- May 31, 2016
- 7,633
- 7,912
Usiwe narrow minded nimekupa mfano, kimsingi unapoonesha dharau tegemea feedback mbaya kutoka kwa yule uliyemdharau.
Yule jamaa anataka kuonesha jeuri ya pesa, kuna mambo kama mtu mwenye akili timamu unapaswa kutambua, heshimu askari maana wao ndio walinzi tuliowapa dhamana ya kutulinda, hata rais na viongozi wengine tunalazimika kuwaheshimu maana wana dhamana, umaarufu na utajiri wetu sio jambo la msingi sana linapokuja suala la ulinzi na usalama, ndio maana tunahitaji kuilinda amani tuliyonayo kwa nguvu zote maana hiyo amani ikipotea hata pesa zako hazina thamani tena, utatumia wapi?
Tuheshimu serikali, tuheshimu askari suala la mapungufu kila mtu analo hata wewe lazima una mapungufu yako.
Cha kujua ni kwamba askari hapendwi kirahisi kama wengi wenu mnavyodhani
Ndiyo hili ambalo, watanzania wengi wanakuwa wanafiki.
Hata pale aliyepaki gari angeachiwa bila kukamatwa bado wangesema kwa unafiki kwa mfano, majembe na polisi bila kumkamata na kumpeleka huyo jamaa kituoni bado huu uzi ungekuwa na lawama kwa polisi na majembe kuwa hawawakamati vigogo na wenye hela.
Ila polisi wasilaumiwe tu bila, watu /wananchi kuangalia nini kilichopelekea hali hiyo ikatokea wao wanakaa kuangalia kama dosari .