Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu


Hii ndiyo ingekuwa post yako/bandiko lako namba moja wala kusingekuwa
na maswali mengi kutoka kwa wachangiaji.
 
kuna jambo ni nilisha wahi ku post jf.ukijua sheria kwa tanzania polisi huwa mbaya kwake na kuweza kukufanyia baya kwa makusudi.sasa huyu ni mtu mkubwa je sisi makapuku
 
Askari muoga huyo anakimbilia kufyatua risasi ovyo akidhani ataogopwa
SI VEMA KABISA KUCHUKUA SILAHA YA ULINZI WA RAIA UNAPOKUWA CHINI YA INFLUENCE A MADAWA YA KULEVYA AU UTINDIO WA DHAMIRA CHANYA KWA JAMII!
 
SI VEMA KABISA KUCHUKUA SILAHA YA ULINZI WA RAIA UNAPOKUWA CHINI YA INFLUENCE A MADAWA YA KULEVYA AU UTINDIO WA DHAMIRA CHANYA KWA JAMII!
Mkuu nimemshangaa pia sana huyu jamaa ila mungu mkubwa bwana
 
Malima naye ni mjinga aweziona mtu kashapandisha jazba kupitiliza pale angeweza pigwa risasi akafa kwa jambo ambalo angeweza epusha .police yule amepitiliza kiwango cha ujinga na nilishaona mauti kwa Malima yalishanikia siku nyingine asibishane na askari mwenye jazba hivyo ni hatari kwake
 
Nimeona umuhim wa askari polisi, Kuwa na Elim walau ya chuo ,kikukuu au diploma, tu, itawasaidia ktk reasoning,
 
Kwahiyo angefanyaje anageingia kwenye gari apelekwe kusikojulikana?
 
vipi wamefikia wapi kwenye hili sakata baada ya malima kwenda kituoni?
 
*SHERIA YA JESHI LA POLISI NA HUDUMA SAIDIZI (SHERIA KUU SURA YA 322)*

29. (1) Afisa polisi yeyote anaweza kutumia silaha dhidi ya:–
(a) mtu yeyote aliyefungwa kisheria kwa kutuhumiwa au kuhukumiwa kwa
kosa pale ambapo mtu huyo anatoroka au anajaribu kutoroka na pale
ambapo afisa polisi huyo ana sababu ya kutosha kuamini kwamba
hataweza vinginevyo kuzuia utoro huo na amempa onyo mtu huyo
kwamba angetumia silaha hizo dhidi yake na onyo hilo halikusikilizwa;
(b) mtu yeyote ambaye:–
(i) kwa kutumia nguvu, anaokoa au anajaribu
kumuokoa mtu mwingine yoyote kutoka katika kifungo; au
(ii) kwa kutumia nguvu, anazuia au kujaribu kuzuia
kukamatwa kwa mtu mwingine yeyote,
pale ambapo afisa polisi huyo ana sababu ya kutosha kuamini kwamba yeye au mtu
mwingine yeyote yuko katika hatari ya kuumizwa na hataweza vinginevyo kukamata
au kuzuia uokoaji huo
(2) Mamlaka aliyopewa afisa polisi chini ya kifungu hiki yatakuwa ni
nyongeza na sio pungufu ya mamlaka yoyote aliyopewa afisa polisi huyo na sheria
nyingine yoyote.
 
Mim binafs huwa siwez kubinashana na watu wenye I.Q ndogo kama po.....li.....ci. eti mkanda unabendera ya taifa so then....!!!!! Kwani kama umeapa hutakufa???. Idiot
 
Watu wenye pesa yao wanadharau sana polisi.

Nimeshuhudia sana hasa katika majiji kama dar au Arsha yaani maskini polisi wanadharaulika sana .

Watu wanalala kwenye mbu kwa ajili ya Usalama wetu lakini mijitu bado haitambui ina leta dharau.

Inakera Sana mtu kukuletea dharau kwa sababu eti anapesa.
 
Safi sana Askari angempiga na mtama, wanasiasa washenzi sana, wanajiona wanahodhi kila kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…