Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu

Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu

Kwa kweli askari wengine wanahabisha jeshi letu pendwa kiasi cha kuonekana halina nidhamu kabisakufikia kiasi cha kutumia silaha ovyo ovyo tu.
IGP please chukua hatua maana inaoneka makamanda wako akina Mkuu Silo hilo la nidhamu ya watu wao linakuwa gumu kweli na mtihani kweli kweli!!!!!!!!!!
 
Watanzania tumezoea kuongea kwa fashion ya upepo wa kisiasa.

Kwa mtazamo wa haraka haraka wananchi walipomzingira mtu walijua ni mwizi na wangeweza kumuua sasa polisi kupiga risasi juu ni kwa nia ya kutawanyisha watu ili kuepusha kifo cha jamaa.
Fashion zingine zinatuvua nguo ni vema tukaachana nazo.

Tazama heading ya hii habari, risasi zarindima! Katika maelezo risasi moja ndiyo imepigwa hewani sasa risasi zirizolindima ni ngapi na ziko wapi katika maelezo?

Mwanzoni mwa habari, mleta mada anasema kumekuwepo na majibizano ya risasi, mwishoni anasema risasi moja ndiyo imefyatuliwa hewani, sasa hayo majibizano ya risasi ni baina ya polisi na nani? ikiwa mmiliki wa gari hakua na silaha na wananchi hawakua na silaha!
Nimesema wapi ni risasi moja, hapo zimefyatuliwa kama nne hivi au tano hata kuskiliza milio ya risasi huwezi pia
 
Ukiwa hapa jf kila kazi unaweza kusema unaiweza.
Nakushauri nenda ukawe polisi maana hata wewe ni mtanzania ili uwafundishe huo weledi wako
Huwezi jua kazi ya kila mtu hapa jf, siwezi kufanya ujinga kama huo wa kufyatua risasi hovyo bila sababu ya msingi halafu kwanini upaniki bila sababu za msingi, Huyo askari ni mjinga sana hajaiva kiuaskari au anasumbuliwa na utoto na huenda na wewe ukawa mmoja wao.
 
Sasa kwa nini na yeye anapack sehemu isiyoruhusiwa ? Akisababisha ajali je ? Tatizo hawa wazito wanawadharau sana askari polisi
Haku park sehemu isiyoruhusiwa, gari lilikuwa limeegeshwa na dereva akiwemo ndani, na liliegeshwa upande wenye maduka ambao unaruhusiwa, ila mara nyingi huwa wanapenda kusumbua na hata kusababisha wenye maduka kukosa wateja kwa kuogopa kukamatwa na hao majembe
 
Huwezi jua kazi ya kila mtu hapa jf, siwezi kufanya ujinga kama huo wa kufyatua risasi hovyo bila sababu ya msingi halafu kwanini upaniki bila sababu za msingi, Huyo askari ni mjinga sana hajaiva kiuaskari au anasumbuliwa na utoto na huenda na wewe ukawa mmoja wao.
Ni rahisi kuandika hapa jf.
Mtanzania anajua kila kitu lakini cha ajabu nchi yetu bado haisongi mbele.
 
Haya baadhi ya maneno... "mimi nina mkanda wenye Bendera...... Nimeapa...."
Kwa wale wajuvi wa sheria za kapa Tanzania... Kuhusu ufyetuaji wa risasi mbele ya raia... Aliyesimama... Sasa jamaa kaanza kukoki mtutu, raia wakamwambia huna mamlaka, kawaoneshea kwa kufyetua risasi... Raia wapo tu hata hawajakimbia...

Halafu polisi kajaa jazba hatari, je kama angekuwa anamkamata na aka resist arrest si angepigwa hata ya kichwa...
 
Fafanua mkuu
Ishu ni hv, huyu ndugu malima jr alienda IOM akamuacha dereva wake kwenye gari, dereva akaegesha gari upande ambao kuna maduka na migahawa na ni upande ambao huwa hawakamati labda wakubabatishe mjinga mjinga, sasa mabwana wakubwa (Majembe) wakaja akawa anataka kukamata gari, dereva anamuuliza kitambulisho jamaa akagoma, sasa dereva akaanza kumfokea ndo wananchi wakajaa kwenye tukio, walipomuomba tena atoe kitambulisho akagoma ndo wakataka kumpiga, bahati walikuja na polisi ambao walikuwa kwenye gari, baada ya kelele polisi wakatoka kutuliza presha za wananchi. Mwenye gari (Malima) alipokuja akauliza kwa nn wanataka kukamata gari na kwa nn hawataki kutoa vitambulisho majibu hayakupatikana, Polisi wakapanda kwenye gari wakawa wanaondoka, sasa cha ajabu baanda ya mwendo waa sekunde 30 wakapaki gari pembeni wakaanza kujibizana upya ndo hapo dereva akapaniki na askari akapaniki jamaa akaamua kufyatua risasi juu watu hawakukimbia. Ikabidi Polisi wamchukue Malima Jr waende nae Kituoni.
 
Haya baadhi ya maneno... "mimi nina mkanda wenye Bendera...... Nimeapa...."
Kwa wale wajuvi wa sheria za kapa Tanzania... Kuhusu ufyetuaji wa risasi mbele ya raia... Aliyesimama... Sasa jamaa kaanza kukoki mtutu, raia wakamwambia huna mamlaka, kawaoneshea kwa kufyetua risasi... Raia wapo tu hata hawajakimbia...

Halafu polisi kajaa jazba hatari, je kama angekuwa anamkamata na aka resist arrest si angepigwa hata ya kichwa...
Mkuu we acha tu. Kuna mambo ukiyafikiri kwa kina wazimu utaambatana na wewe
 
Back
Top Bottom