Watu Wengi humu JF, wanawalaumu polisi ila ukiwa pale Benki unaambiwa egesha au ondoa gari eneo hili au lile mbona huwa hamji humu kusema polisi wabaya!?
Mbona tukiwa tunachukua hela kiasi kikubwa tunawalilia polisi watufanyie escort ili pesa zetu ziwe salama!?
Majambazi, wakikuvamia mbona kilio cha kwanza huwa ni kutoa taarifa polisi na kuomba msaada wao!?
Hebu jiulize, kama gari lilokuwa limeegeshwa kisha aliyeegesha akatenda uhalifu!?
Sasa hivi, ingekuwa tofauti kabisa humu JF , kuwa polisi inawaachia watu wanapaki ovyo na kusababisisha waharifu kutekeleza azima zao.
Angalia, lugha iliyotumiwa na hao waliopaki gari , kweli mtu mwenye sitaha na kujiheshimu na kuheshimu watu wengine anaweza kujibu vile!? Mbaya zaidi eti amekuwa hadi naibu waziri!?
Jiulize, ni mara ngapi watu wanapaki mahala siyo sahihi ila wanatumia lugha ya staha ao hao watendaji wanawaacha na kuondoa magari kwa ustarabu!?
Vyeo, nafasi fedha isiwe chanzo baadhi kuwadharau na kuona kazi za wengine hazifai.
Kutii, sheria na amri ndiyo suruhisho tu kwa mambo kama haya ili yasijitokeze.