Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu

Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu

Kwa maelezo haya, polisi hajafanya kosa kabisa kufyatua risasi hewani.

Kwa sababu, naona maelezo hapo yanasema wananchi walikuwa Karibu kujichukulia sheria mikononi.

Hivyo, polisi kuokoa maisha ya aliyedhaniwa ni jambazi ili asitolewe roho.

Au mi nimeelewa tofauti!?

Achana na maelezi, je kwa ulichokiona unadhani kulikua na ulazima gani wa kupiga risasi?
 
Hujui kitu usifikiri hiyo silaha amebeba kama manati ya ndege. Huyu ana busara sana kupiga juu kutawanya watu. Malima kama wazirj mstaafu alitakiwa kuwa na busara kuliko kubeza Askari yeye akipata shida anakimbilia kuomba msaada huko huko Polisi
siwezi kubishana na wewe ambaye hata hujui ni wakati gani hasa unatakiwa utumie silaha ya moto,,, ilitakiwa kwanza amri kama kulikuwa na tishio lolote lile. Malima alitishia nini, je aliamriwa kukamatwa yeye akakimbia?
 
Nimeangalia clip,Askari Polisi wa namna hawatakiwi kufanya kazi za operations kama hizo,anaonekana anafaa sana kuwa ktk kikosi cha kufuatilia wahalifu au majambazi wanaotumia silaha hukooo field ata enjoy sana kazi yake ya Polisi.
Apelekwe mkuranga..!
 
Tufanye uko sawa,kutumia smg kupiga risasi hewani kwa mkono mmoja? duuh!! Halafu rapid umeiona ile recoil kidogo ajipige mwenyewe au raia..hii inaonyesha uzembe! uzembe! ukosefu weledi yeye ni askari amepanic mwenzake yuko well trained and displined anamuamua mwenzake hii inaleta taswira za ajabu good cop and bad cop.
Hiyo clip ikifika Ikulu aliyekua anamzuia mwenzaje ni lazima awajibishwe kwa kitwndo cha yeye kama afisa wa serikali kumpinga afisa mwenzake hadharani badala ya kuonyesha uwajibikaji wa pamoja na Hugo aliyekua amepanic na kupiga risasi hovyo, IGP ataagizwa ampandishe cheo.
 
Siyo waziri lakini viashiria vya kujiona kuwa yeye ni kiongozi mkubwa asiyetakiwa kuguswa kwa kitu chochote bado anavyo.
Mbona haya mambo ya viongozi kushikiwa bastola na bunduki yameibuka awamu hii?mbona awamu zilizopita hatukuona haya?tatizo ni nini?
 
Sitagusia sababu za kilicho sababisha gari ya Mtoto wa Malima kukamatwa. Ntajikita kwenye matumizi sahihi ya silaha ya moto.

Askari ambaye hajawiva kimafunzo hasa kwenye "use of force and fire army" anaweza kufanya ujinga waajabu kwenye matumizi ya silaha ya moto.

Silaha ya moto ina miiko yake mikuu minne. Wanaofahamu wamenielewa, sio kitu unachoweza kukitumia hovyo hovyo upojisikia ikiwa zile 5 circumstances hazijatimia au sio justifiable, necessary and proportionate.

Askari yule akiulizwa atoe maelezo kulikuwa na ulazima gani wa yeye kufyatua risasi? Je kulikuwa na kitisho cha maisha yake au wenzake aliokusudiwa kuwalinda? Je aliyemsababisha (subject) huyo private officer kufyatua risasi ya moto alikuwa na silaha zinazolingana nguvu na silaha yake? Kwenye discharge form atajaza nini? Kuhalalisha matumizi ya risasi alizopoteza? Haya ndio matumizi mabovu ya vifaa vya jeshi!

Askari unafanya "warning shot" alichofanya huyo askari ikiwa unaondoa kitisho cha maisha yako au kutawanya mkusanyiko hatarishi kwenye maisha yenu. Kitu ambacho hakikuwepo!

Askari amejitia hasira mwenyewe, anashuka kwenye gari then anafoka na kufyatua risasi angani bila kuangalia iendako.

What if kungekuwa na jengo refu? What if kungewa na ndege inapita angani usawa huo? What if ingepiga nyaya za umeme? What if Malima angeonyesha aggressiveness behaviour toward him?

Askari lazima uwe na uwezo wa ku control short temper, askari huyo binafsi angekuwa rumande na nisingeruhusu apewe silaha ya moto mpaka arudi darasani.

Kama issue ilikuwa ni maneno ya kukarahisha mbona mwenzie hakufyatua wala kuonyesha nia ya kutumia silaha yake na badala yake akamsihi mwenzie kwa kumuita "port" na kumrudisha kwenye gari.

Itoshe kusema somo la use of force and fire army lizingatiwe sana. Deal with difficult people and confrontation nalo lizingatiwe.

Nawakilisha!
 
Apelekwe mkuranga..!
Huyo Polisi amekosa maadili kabisa ya kiaskari amefanya jambo la kihuni kabisa akiwa na sare za Janhuri huku akitumia silaha ndiyo sivyo hafai ktk usalama wa raia na Mali zake.

Hicho kiapo anachopiga kelele ameapa ni kiapo gani hivyo.IGP Mangu hawa ndiyo vijana tunaowategemea ktk ulinzi wa RAIA wa Tanzania na Mali zao.

I think you have to think twice on the ethics as well as standard operating procedures on guns kwa ujumla kuhusu matumizi ya silaha kwa RAIA asiye kuwa na silaha.

Otherwise huyo kijana aliyefanya hili tukio la kutumia silaha ovyo achukuliwe hatua za kinidhani kijeshi.
 
Kama mpaka tunappandika hapa huyo askari hajavuliwa uaskari ntashangaa sana.unapiga risasi hewani kutishia raia?wakati unalipwa mshahara kwa kodi zetu kulinda raia na mali zao.tunaomba fagio la vyeti feki lipite polisi na jeshini.na kuanzia sasa hivi polisi waajiriwe wenye diploma na degree
Nilishawahi kuandika humu, hao hata wasome mpaka level ya PhD, wakiisha vaa hizo nguo zao tu na hiyo mikanda ya bendera uwezo wa kufikiri unakuwa wa kindergarten.

"ALIYEPUNGUKIWA NA AKILI UWAONEA WATU"
 
Kutoa bunduki kwa mtu ambaye ana ata kiwembe in bonge la usengerema.Kuna kila haja ya kupitia upya mitahara, age na qualification za vijana wetu Wa jeshi la Polisi.
Ukiangalia kwa makini yule ni kijana chini ya 22 yrs na ni in take ya miaka 2 au 3 iliyopita.
 
Back
Top Bottom