Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu

Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu

HAO SIO MAJEMBE NI KAMPUNI YA PRE SCAN AUCTION MATT NDO WAKALA WA KUTOKA MANISPAA YA KINONDONI NA KAMPUNI NYINGINE INAITWA HEPAUTWA INV.
HAO MAJEMBE WAO NI ILALA PAMOJA NA TAMBAZA.
 
Inasikitisha kuona risasi ambazo serikali inagharamia pesa nyingi zinatumika visivyo kwa kutishia raia daah bongo kweli tunaenda mbali
 
Kwa maelezo haya, polisi hajafanya kosa kabisa kufyatua risasi hewani.

Kwa sababu, naona maelezo hapo yanasema wananchi walikuwa Karibu kujichukulia sheria mikononi.

Hivyo, polisi kuokoa maisha ya aliyedhaniwa ni jambazi ili asitolewe roho.

Au mi nimeelewa tofauti!?
Alitakiwa aonyeshe kitambulisho but why alikataa?na kama yuko kazini kwa shughuli hiyo kitambulisho muhimu.maono yangu
 
Pole yake Malima.
Hii inaweza kumpelekea akashtakiwa kwa kuwazuia askari kufanya kazi yao.
 
Umenikumbusha mbali sana, mwaka 1992 yalipotoka matokeo yetu ya O-Level kuna jamaa yangu alikua amepata Division Four basi mzee wake kwa hasira akasema "hata sitaki kusikia mambo ya ku re-sit naliacha liende Polisi ili likajiendeleze lenyewe mbele ya Safari kama linadhani kulipa ada ni lelemama"
Na usikute hadi wa leo hajajiendeleza
 
Wamejifunza kutoka kwa Harmorapa...

hamorapa alitoka mbio! ila qadri siku zinavozidi kusonga waTanzania wanatiwa usugu na watendaji wa Rais wa kutoogopa bunduki, nasema hili halipendezi na ni ishara mbaya sana! Enzi zetu sisi ukisikia bunduki inapigwa nje unaingia uvunguni mwa kitanda kwa kuogopa! Dah sasa hivi watu ndio kwanza wanashabikia utadhani kuna movie unarecordiwa!

pale utadhani yule askari rambo anafyatua risasi! all in all si jambo zuri kabisa askari kufanya yale! nashauri wote wahojiwe na mkosa atiwe hatiani!
 


Mchana huu pamesikika milio ya risasi maeneo ya Masaki karibu na Double tree Hotel.

Yalikuwa ni majibizano kati ya PRE SCAN AUCTION MATT waliokuwa wameambatana na Polisi walipojaribu kukamata gari lilokuwa limeegeshwa pembeni ya barabara hali ya kuwa Dereva yupo ndani.

Inasemekana gari lilikuwa la Mwanae Kighoma Malima aliyeenda IOM kufatilia ishu zake.

Mtu wa Majembe akavamia gari hilo na alipodaiwa kuonyesha vitambulisho aligoma kutoa ndio wananchi walipolizingira gari wakitaka kumpiga wakijua ni jambazi.

Polisi aliingilia kati na katika majibizano akafyatua risasi juu kumtishia ndugu Malima aliyekuwa hana hata silaha wala hakukuwa na mwananchi aliyekuwa na silaha.

Adam Kighoma Malima alikuwa mbunge wa jimbo la Mkuranga na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, enzi za Kikwete. Anatokea katika chama cha CCM.[/QUOTE]

  • Vitendo kama hivi vya polisi kutumia bunduki hadharani kama Jeshi lisilokuwa na nidhabu ni aibu kubwa kwa Tanzania na itawaogooesha wawekezaji. Polisi wajifunze kuongea na watu bila ya kutumia bunduki na vitisho bila ya sababu Hii ni aibu kwa taifa na haioneshi kuwa Tanzania ni nchi yenye amani
GullamJF-Expert Member
#37
Today at 8:34 AM

Joined: Dec 1, 2013
Messages: 1,759

Likes Received: 568

Trophy Points: 280
 
Litapita tu kama upepo ila angekuwa ndo Tundulisu au kiongozi wa chadema ,yaani ingekuwa patashika ...mkuu wa polisi nchini angetoa tamko, kamanda wa ilala sijui kinondoni angetoa tamko. Waziri mwigulu angetoa tamko, mkuu wa mkoa, wilaya ,uvccm ...woote wangemlaani huyo mpinxani kumtishia polisi na kushindwa kufanya kazi yake..
Wakati huo huyo mpinzani yupo Segerea na kanyimwa dhamana.

Hizi double standard ndo zinawafanya wananchi kufurahi watu fulani wakimfuata JKN
 
Ningekuwa mkulu kiukweli ningehakikisha askari huyu anapanda cheo haiwezekani wajinga wachache wachukulie nchi kama yao kisa viongozi
Viva askari
 
Back
Top Bottom