Fika hadi Ununio usawa wa mahaba beach kabla ya kufika lami ya Ghome sekondari hapa nyuma kuna kalami kanaingia kulia. Kwa kweli nilibaki na mshangao tu. Upande wa kulia wa lami ni bahari na upande wa kushoto ni ghorofa tupu kama wamechaguana kujenga yale maeneo tena sio ghorofa za wasiwasi mpaka unaenda kukuta nyumba za Lugumi zilizopigwa mnada, njia inatokea Jkt hadi chuo cha TISS. Kwa kweli kuna watu wamechuma hela ile masaki original sasa hivi imebaki historia with old version buildings. Kuna ghorofa moja juu kabisa ina picha ya jani la bangi hahaha. Bongo ni zaidi ya uijuavyo na tofauti ya walionacho na wasionacho ni kubwa mnooooo.