BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Masanja Mkandamizaji ameulizwa anahisi kwa nini watu wengi hawamuelewi kwa namna yake ya mahubiri amesema kuwa sababu kubwa ni kuwa kuna watu wengi wanatamani awe kama Mtumishi wao yaani afanane nao mpaka mavazi.
Amesema “Msinifananishe na mtumishi wenu bali mwambieni mtumishi wenu afanane na mimi kwa sabanu yeye ni mtumishi wa kisasa zaidi.”
Ameeleza hayo Jijini Dar es Salaam wakati anaongea na waandishi kuhusu kampeni za kudumisha Uzalendo kwa Watanzania ili kuyasifia na kuyatangaza mambo mazuri ya taifa la Tanzania.
Mbali na hilo kampeni hii inahusu kuhamasisha zoezi la Sensa ya watu na makazi ambayo itafanyika tarehe 23-8-2022.
Chanzo: Bongo5