Kwa kweli hawa wanakwaye na watumbuizaji wanajiharibia wenyewe. Kwa mtu yeyote aliyebahatika kununua VCD ya huyu jamaa ni mategemeo yangu haukujifunza ukitoa wimbo mmoja tu uliobeba jina jingine na zile nane zinazobakia zinaonyesha ni jinsi gani masabuli yametumika kufikiria. Jana nilinunua hiyo VCD orginal(Inauzwa sh 5000) ili nienjoy weekend hii, nilichokikuta sasa ndo hayo manyimbo ya mapambio ya live kanisani. Masanja umeniangusha sana na simshauli mtu anunue hiyo VCD kwa sababu inaonyesha jinsi gani haujatumia kipaji chako.