Masanja Mkandamizaji: Watu ooh! Mama anasafiri sana. Ulitaka asafiri babaako?

Masanja Mkandamizaji: Watu ooh! Mama anasafiri sana. Ulitaka asafiri babaako?

Kigodoro

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2014
Posts
1,660
Reaction score
1,679

Kauli hii ya kifedhuli ameitoa Masanja Mkandamizaji alipopewa nafasi ya kuburudisha leo hii mbele ya mamilioni ya Watanzania na wana-Afirika Mashariki kwa ujumla, waliokuwa wanafuatilia sherehe za Uhuru wa Tanganyika kupitia runinga.

Kauli hii inawabeza Watanzania wenye moyo wa kuipenda nchi yao wanaohoji kwanini Rais Samia anafanya sana safari za nje?

Hii dharau kwa umma wa Watanzania haikubaliki na haivumiliki.
 
Siku hizi wamerahisisha kila kitu, teuzi wanapewa vichaa bila kufanyiwa vetting yoyote, sishangai hata huyo nabii uchwara nae wamemuokota jalalani wakampeleka akatoe speech tena ametamka huo upuuzi mbele ya wageni waalikwa, sijui tunaonekana taifa la aina gani mbele za waliostaarabika.
 
Kauli hii ya kifedhuli ameitoa Masanja Mkandamizaji alipopewa nafasi ya kuburudisha leo hii mbele ya mamilioni ya watanzania na wana-Afirika Mashariki kwa ujumla, waliokuwa wanafuatilia sherehe za Uhuru wa Tanganyika kupitia runinga.

Kauli hii inawabeza watanzania wenye moyo wa kuipenda nchi yao wanaohoji kwanini Rais Samia anafanya sana safari za nje?.

Hii dharau kwa umma wa watanzania haikubaliki na haivumiliki.
Ndio wapiga debe wa CCM hao. Hata mwenda kuzimu alipo zuia safari za nje walimpigia makofi na kumpongeza. Mama kawa Vasco da Gama wana msifu. Ccm hawajulikani kama ni popo au ndege!!
 
Huyo ndo mchungaji eti, why lakini? Kwann watu wanaichukulia kazi ya uchungaji poa namna hii?

Na tena ajabu unakuta mtu anawafuasi lukuki kanisani, hivi huwa anawapumbuza na nini!!

Achaneni na hawa watu, nendeni kwa watu wanaomuabudu Mungu katika kweli yote!!
 
Wajinga ndio waliwao.
 
Back
Top Bottom