Masanja na Uropokaji kwa Wazee!

Masanja na Uropokaji kwa Wazee!

Jana kama kuna mtu alipata kutazama kipindi cha Orijino Komedi, basi lazima angepatwa na jazba nyingi, hasa katika sehemu ya umalizaji wake.
Masanja katika hali ya kuonyesha kukerwa na kuanza kwa kipindi-pinzani cha EATV cha kusaka wachekeshaji, basi alitoa kauli 2 chafu zote zikimlenga R.MENGI, kama hivi:
i-Mtu anajifanya tajiri na ana hela, sijui kwanini anachanganyikiwa na mambo madogo kama haya!

ii-Nilitegemea UMRI wake (Mengi) ungeendana na mambo yake, lakini kumbe wapi, ndo hivyo tena!

Binafsi niliboreka sana na maneno hayo, si kwamba nampenda sana Reginald, lakini kumkashifu mtu kama yule aliyemzidi umri mno ni kinyume cha maadili kabisa!
Hana adabu kabisa Masanja, *+$%%*inkoskaz huyu!😡....
Ulijuaje anamsema MZEE MENGI???
 
1st Lady,

Kuna siku nilikuwa mtaani nikaona jarida fulani likiwa na picha unayotumia kama avatar yako.(kama nakumbuka vizuri tittle inasema "usilie kwa ajili yangu")
Siku nyigine nikaona kuna mtu kavaa T-shirt imeandikwa "NIKO KIZAZI" kama sijakosea.
Kwakweli nilivutiwa na hivyo vitu viwili nikasema siku moja nikiwa jamvini nitakuuliza.
Ninachotaka kujua ni je? , kuna uhusiano wowote kati ya wewe na hivyo vitu?
Kama jibu ni ndiyo basi HONGERA SANA.

Heshima mbele.

hahaha Nitakujibu PM
asante
 
Nilitazama hicho kipindi tangu mwanzo hadi mwisho sikusikia jina la Mengi likitajwa.

Mimi niliangalia kipindi kile, ijapokuwa nilikuwa na hama hama kati ya TBC1 na EATV, pale mwishoni alipokuwa anafunga kipindi Masanja alitoa maneno yaliyokuwa yanaonyesha hasira yake juu ya EATV na R. Mengi.

Ingawa hakutaja jina, lakini sentensi kama hii ahihitaji mtu kujua sayansi ya kurusha roketi kujua alimaanisha nini, alisema...."watu wana hela lakini wana roho mbaya (huku akionesha ishara ya kukunja kidole) wana hela nyingi lakini hawatosheki......na je kwa nini wameweka muda huu huu......si wangetafuta muda mwingine?" Alafu akaendelea..."najua sasa hivi watazamaji mnaenda kwa jirani ku angalia....lakini sisi ndo wenye vipaji vya ukweli...hatuna hela lakini tuna vipaji...."

Ni wazi alikuwa akiwasema EATV na kipindi chao kipya cha Ze Comedy....ambacho kinarushwa muda sawa sawa na kipindi cha Orijino Komedi cha kina Masanja!!!

Masanja anasahau kwamba EATV walikuwa wanarusha hicho kipindi muda huo huo hapo mwanzo....na ni TBC1 na kina Masanja unaweza ukasema ndo waliiga muda (ambapo kwangu naona sio issue).

Nakumbuka hata kipindi kile Futuhi wa Star TV na Vimbwanga time wa Channel 10 wanaanza, kina Masanja waliwapiga madongo sanaaaa!!

Ninachokiona hapa ni kwamba kina Masanja, Joti na Seki hawajui maana ya soko huria ambapo kila mtu ana uhuru wa kuingina sokoni na kuuza bidhaa au huduma anayoitaka. Katika mfumo huu ni soko tu ndilo litakalomfanya mtu aitoe bidhaa yake sokoni, kwa mfano Vimbwanga time cha Channel 10 walivyoacha kurusha kipindi hicho.

Masanja et al acheni kutukana watu........TV station zenyewe ziko 3 tu hapa nchini sijui mtakimbilia wapi mkitemwa TBC1. Kila mtu atakayetaka kufanya kazi na nyie ataogopa kudhalilishwa siku mtakapo vunja mkataba!!

Naona upeo wenu wa kufikiria ni mdogo sana, nawashauri acheni majungu na visilani.......pigeni kazi, kipindi bora ndicho kitakachoangaliwa na watamaji na si vinginevyo!!

Ni hayo tu!
 
Halafu utakuta mzee wa watu hata hahusiki na upangaji wa vipindi au ubunifu wa vipindi.Pengine hata hajui nini kinaendelea.Jamani hawa akina Masanja sijui wataerevuka lini jamani.
 
Mimi niliangalia kipindi kile, ijapokuwa nilikuwa na hama hama kati ya TBC1 na EATV, pale mwishoni alipokuwa anafunga kipindi Masanja alitoa maneno yaliyokuwa yanaonyesha hasira yake juu ya EATV na R. Mengi.

Sasa wabishi waliocoment huko juu wanabisha wakati hawajui wasemalo, they just copy each other's univestigated sentence!...shame!
Thanx that wewe mkuu uliona na kusikia mwenyewe kwa macho na masikio yako...may be they will be careful before answering the posts!
 
Hiyo kwenye mabano aliiweka Masanja au ya kwako?. Kama Masanja hakutaja jina la mtu basi sioni ubaya upo wapi. Maana Mtu si Mengi pekee, sisi sote ni watu.

Tusimuwekee masanja maneno mdomoni mwake. Cha kufanya mtafute umuulize alikuwa anamuongelea mtu yupi?. Then lete jibu tulijadili.
Hofstede umeonyesha upeo mkubwa sana. Kweli kama Masanja hataja jina la Mtu, kwa nini wao wanataja jina la Mengi?.

Siwatetei akina Masanja, lakini nasi tutafakari kabla ya kutuhumu mtu. Tufanye research kidogo ili tuwe na proof kabla ya kusema!
 
Hawa wanaojiita Orijino Comedy sasa naona wamefulia to the last drop!
 
Mimi mnanichosha! Eti Masanja hakutaja jina jamani hata kuread/listen between lines nako kunakuwaga kugumu kwetu?
 
Mimi mnanichosha! Eti Masanja hakutaja jina jamani hata kuread/listen between lines nako kunakuwaga kugumu kwetu?

Hivi pale masanja anapomcopy Pinda huwa anamtaja jina?
Vuipi Mpoki na J Komba-huwa anamtaja jina?

sasa iweje akimtaja Mengi watu wankuwa wakali?
 
Hivi pale masanja anapomcopy Pinda huwa anamtaja jina?
Vuipi Mpoki na J Komba-huwa anamtaja jina?

sasa iweje akimtaja Mengi watu wankuwa wakali?
Hueleweki, na hauko kwenye hoja!

Ishu ni kwamba ni tabia gani hii ya kumsema mtu aliyemzidi sana umri kama mtoto mdogo, na kwa kejeli zisizokuwa na msingi?..
AWaache wenye mali wasemane bana, yeye NI KAPUKU TU, inamhusu nini wakati hana kitu zaidi ya makalio😡
 
Mi nadhani mdau hapo juu yuko right... je ni kweli masanja alitamka jina la MENGI?
TAFAKARI KABLA HUJATENDA/KUSEMA/NENA!
Tusiwawekee watu maneno midomoni..
 
Ukinona mtu aliemuacha mke wake anazua ugomvi akimuona mtalaka wake na bwana mwingine ujue bado anampenda mke huyo. Masanja na crew yake waliondoka kwa Mengi wakiwa bado wanapapenda ndio maana analia wivu! we ukiona cha nini wenzio wasema watakipata lini! Komedi orijino msimlaumu mwamuzi, mkubali tu matokeo!
 
PJ naona uache tu kuwaelewesha watu kila mtu na uelewa wake ..du du ebwanaeee
 
Ukinona mtu aliemuacha mke wake anazua ugomvi akimuona mtalaka wake na bwana mwingine ujue bado anampenda mke huyo. Masanja na crew yake waliondoka kwa Mengi wakiwa bado wanapapenda ndio maana analia wivu! we ukiona cha nini wenzio wasema watakipata lini! Komedi orijino msimlaumu mwamuzi, mkubali tu matokeo!

We umenena vyema sana
Thanxs yangu haijaenda bure!
 
Kwa kweli vijembe vilikuwepo kama mutakubali au la.

Jengine linalonikera mimi ni yale maneno yao ya kejeli kejeli na hata ukisema "ukipenda angalia usipopenda ....."

Wajue kwamba wanaoangalia ndio wafalme na sio wao, bila ya waangaliaji kipindi kitafutwa kwa muda mfupi tu.
 
hodi wenyeji, hodi tena!
Naomba kukaribia kwenye jamvi na kamchango kadogo Huyu mshkaji masanja hakumtaja jina mtu. Mchangiaji kwa fikra zake amemrenga R. Mengi. Ni sawa na maneno ya kwenye khanga mwingine anaweza soma akasema amenivalia mimi je mtengenezaji alijua wewe na huyo mna bifu? ACHA KUJISHUKU NGOMA HUJAPIGIWA WEWE, UNACHEZA.
 
Ukiona ngoma inavuma sana ujue karibu inapasuka, ujue hawa vijana wana kumbukumbu fupi kwani wameshasahau kabisa walikotoka. Mtoto hakui kwa mzazi
 
hodi wenyeji, hodi tena!
Naomba kukaribia kwenye jamvi na kamchango kadogo Huyu mshkaji masanja hakumtaja jina mtu. Mchangiaji kwa fikra zake amemrenga R. Mengi. Ni sawa na maneno ya kwenye khanga mwingine anaweza soma akasema amenivalia mimi je mtengenezaji alijua wewe na huyo mna bifu? ACHA KUJISHUKU NGOMA HUJAPIGIWA WEWE, UNACHEZA.

Nina shaka na upeo wako Banda! Kwa taarifa yako Orijino Komedi wanafanya maigizo ambayo kila igizo huwa anajulikana nani mlengwa kama unafuatilia vizuri. Mfano kina masanja walipoigiza Mheshimiwa kutaka kuingizwa mjini kwa kukabidhi gari la mgonjwa kwa halmashauri isiyohusika...je ulikuwa hujui nani anaigizwa kwa sababu hakutajwa jina???

Bisha palipo na mantiki na hoja ndugu, vinginevyo tutatilia shaka ufikirivu wako!!
 
hodi wenyeji, hodi tena!
Naomba kukaribia kwenye jamvi na kamchango kadogo Huyu mshkaji masanja hakumtaja jina mtu. Mchangiaji kwa fikra zake amemrenga R. Mengi. Ni sawa na maneno ya kwenye khanga mwingine anaweza soma akasema amenivalia mimi je mtengenezaji alijua wewe na huyo mna bifu? ACHA KUJISHUKU NGOMA HUJAPIGIWA WEWE, UNACHEZA.

Nenda kwenye jukwaa la utambulisho kwanza ujitambulishe huko, ndo uanze kuflow
 
Back
Top Bottom