Masanja: Nimenunua BMW X6 kama mtu mwingine anavyonunua baiskeli

Masanja: Nimenunua BMW X6 kama mtu mwingine anavyonunua baiskeli

Mchekeshaji wa Orijino Komedi na mjasiriamali, Masanja Mkandamizaji amesema kila anachomiliki amekinunua kwa pesa yake halali huku akishangaa kwanini watu wameshtuka baada ya kuona anamiliki BMW yenye plate namba ya jina lake.

Akizungumza katika kipindi cha 360 cha Clouds TV Ijumaa hii, Masanja alisema anamiliki magari mengi huku akidai BMW X6 ameinunua kama mtu mwingine anavyonunua baiskeli.

“Mimi nina magari mengi sana na yote nayachukulia kama chombo cha usafiri cha kunitoa point moja kwenda nyingine,” alisema. “Sasa nashangaa watu wanaongea sana kuhusu mimi kwani gari kitu gani! Hiyo BMW X6 nimenunua kama watu wengine wanavyonunua baiskeli,” alijinadi.

Aliongeza, “Na hata hao TRA kama wananisikia waje hapa Clouds nimekuja nayo ipo hapo chini ili waangalie kama sijailipia.”

Masanja alisema anafanya biashara za aina mbalimbali hivyo kununua gari la thamani siku kitu cha ajabu kwakuwa anaweza kununua kupitia biashara yake moja tu.

View attachment 317030
Hii ndio faida ya kushabikia ccm, angeshabikia matapeli ukawa angetoka mikono mitupu, .

Kama mawakala wao (ukawa) waliokuwa bize kuzungusha mikono hawajalipwa mpaka Leo sembuse msanii
 
Kuna baadhi ya Watanzania kutwa kujionyesha wao eti hawana jelous. Wanajua kusifia sana waliofanikiwa na kuonyesha kua wanawajua wasanii na wafanya biashara kwa kina. Ukikosoa tu. watasema ohh Ana wivu.!
Ukifuatilia kwa kina mfumo wa nchi ulivyokua utakuja kukumbuka walikuwepo walioonekana wamefanikiwa kwa jasho lao mpaka pale walipokamatwa ughaibuni kwa kukutwa na sembe,(achilia waliochomolewa kwa kukwepa kodi bandarini hapa bongo) Wakachomolewa kwenye mikono ya sheria na mfumo wetu kiaina.
Lakini nyumbu Mtaani wanawaona mashujaa bado.sina haja ya kuwataja, manake wengine walijazana kwenye chama fulani kwenye kampeni ya urais.

Nimerusha Jiwe Gizani.... Si kila king'aacho ni dhahabu.
Yangu macho.
 
Last edited:
Biashara ya kuingia kwenye wallets za watu sio nzuri. Mie sioni tatizo kwa msanii kununua gari hilo tunaloliita kuwa ni la kifahari. Kweli ni la kifahari na expensive to run, but hatuwezi kusema bei yake inatofautiana na magari ya class yake. If talking of UK export, Land Cruiser na Range Rover zinaweza kuwa more exoensive hasa tukiangalia gari ya 2009 na specs for xDrive 3.0d SE Halafu kuna mtanzania gani asiyejisifu? Angalia wangapi hawana magari ila wanaingia madukani/makanisani wakizungusha funguo? Mtu amekula ugali maharage, akirudi ofisini anatafuna toothpick ati anatoa nyama kwenye meno.......
 
mwacheni ajivunie alichonacho! "a man brags about his own penis however it is tiny"by ngugi wa thiongo
 
Watu watamponda sana ila siku zote ukimshirikisha Mungu, ukiwa na nidhamu na ujafanya kazi kwa bidii mafanikio hayajifichi.
Namkumbuka Masanja wa miaka ile alipokuwa mambo hayo na akina Joti na Mpoki, leo tunaona mafanikio yao
Aisee uko unatudanganya mchana kweupe masanja umeshawahi kumuona anaigiza kwenye mambo hayo
 
Mjinga sana, maneno yanafaa kutamkwa na Dr. Mengi, Bkharessa na & Gwajima, profesa tibaijuka(BIBI wa pesa ya mboga), chenge,(babu wa vijisenti) na mzee wa msoga na watu wa kaliba hiyo....

Sio yeye. Masanja hana hela ya kununua BMW kama anavyonunua baskeli.

Gari zina charge nyingi sana. Baskeli na gari tofauti sana katika ununuzi, kuanzia kutoa hela benki nk na ikipata ajali anaweza kukesha miaka kuikarabati.

. You never know..Hope alikua anachekesha watu, manake ndo kazi ya ze komedian kama yeye.

Maskini akipata mata** ulia mbwata.

Kwanini JF haina entry exam kwa watu kama wewe! Kwanza unajua kipato cha Masanja. Unajua biashara zake. Yani unaamini wenye uwezo wa kununua x6 ni watu wanaosikika tu, kuna waTz wengi sana wenye huo uwezo FYI na wengine magari sio interest zao. Kama hujui kipato chake pole sana ndio tayari anamiliki x6 endelea kuamini katika bakhressa tu. Siamini uwepo wa uchawi ila waTz wengi ni wachawi kwa roho kama yako
 
ukifanya kazi na mama lwakatare, hizo mavitu ni takataka kwako. mama anajua kuunga. hero hero, hero sister. hongera mkandamizaji. nimeeleweka.
 
My dream car 😛😛
Gari niipendayo kuliko yote ulimwenguni.
 
Hivi ule ubunge alikotangazia nia alipta? No sitaki kuhusisha na haya coz mafanikio huwa uja bila taarifa panapo juhd. Mi nina ka vittara kangu 3doors mbona sihojiwi???
 
Mi hunifurahisha tu anavo wasimbulia watu waliojaa ukumbini kutizama kipindi chake pale kinapoisha! Anaanza Na mamkwe alitoka kijijini hataki kurudi, bekitatu, majirani, mdogo mtu anaelala ukumbini kwa shemeji yake! Ali muradi anawachamba mmoja baada ya mwengine! Kweli usanii ni kipaji kikubwa! I'm happy for his success! Mwacheni ajivune!
 
Akizungumza katika kipindi cha 360 cha Clouds TV Ijumaa hii, Masanja alisema anamiliki magari mengi huku akidai
BMW X6 ameinunua kama mtu mwingine anavyonunua baiskeli.
“Mimi nina magari mengi sana na yote nayachukulia kama chombo cha usafiri cha kunitoa point moja kwenda
nyingine,” alisema. “Sasa nashangaa watu wanaongea sana kuhusu mimi kwani gari kitu gani! Hiyo BMW X6
nimenunua kama watu wengine wanavyonunua baiskeli,” alijinadi.
Aliongeza, “Na hata hao TRA kama wananisikia waje hapa Clouds nimekuja nayo ipo hapo chini ili waangalie kama
sijailipia.”


source: http://www.bongo5.com/masanjaawaijiajuuwanaomshangaakumilikibmw012016/
 
Sawa hakuwepo
masanja alishawahi kuwepo mambo hayo mwishoni mwishoni akiwa pia na yule jamaa anayeigiza kikongo ITV kuna igizo moja wanaekti wametoka kijijini wanashangaa magorofa.
 
Hiyo gari na mimi nahitaji! Kwani shilingi ngapi?
 
Back
Top Bottom