Masanja: Nimevuna mpunga ekari 15 Mbarali Estate - Mbeya

Masanja: Nimevuna mpunga ekari 15 Mbarali Estate - Mbeya

Mchekeshaji maarufu kupitia kipindi cha Ze Orijino Comedy, Emmanuel Mgaya maarufu kama Masanja Mkandamizaji amesema kuwa vijana wanapaswa kufikiria namna ya kuwekeza mashambani kwenye fursa za kutosha kuliko kuendekeza majivuno yasiyo na msingi.

Akizungumza na Starehe Masanja alisema anafurahi kwani mwaka huu amefanikiwa kuvuna tani kadhaa za zao la mpunga katika shamba lake lililopo Mbarali Estate.

"Nimelimia Mbarali Estate namshkuru Mungu kwa kufanikiwa kuvuna mpunga wangu baada ya kuwekeza shamba lenye ukubwa wa ekari 15, huu ni uwekezaji mzuri unaotoa matunda kwa muda mfupi iwapo utahudumia shamba lako ipasavyo."

"Vijana wengi wana nguvu na uwezo wa kuingia mashambani ila wanaendekeza ‘usharobaro' kitu ambacho hakina mavuno kwao," alisema Masanja aliyetumia mashine ya kisasa katika zoezi hilo.

Masanja ambaye pia ni mwimbaji wa kwaya ya New Jerusalem alisema: "Mimi ni mchungaji mtarajiwa lakini huduma yangu ya uchungaji nimeanzia kwenye kundi langu hili la Ze Komedy, kupitia hilo nina washirika wangu ambao natamani wawe kama mimi mchungaji wao wafuate nyayo zangu, naomba maombi ya watumishi wengine wamuombee Joti," alisisitiza!

Kwa sasa, Masanja anahudhuria ibada katika kanisa la EAGT, Mito ya Baraka pia amefanikiwa kutoa nyimbo 10 za Injili na tayari album yake ya ‘Hakuna Jipya' iko mitaani.


Masanja : Nimevuna mpunga ekari 15 Mbarali Estate Mbeya - Makala - mwananchi.co.tz

 
So uyo ni mchungaji au mkulima?

Mkuu, mpongeze mwenzako anapoachieve...

The boy has done justice to his potentials, wewe zako ziko wapi??? mtaishia kuua humu kwenye mitandao na kulalama maisha yanawapiga wakati domo na typing ndio vimekua silaha za kujikosha na majukumu na other popportunities

Silly
 
Big up massanja.wewe jembe kila kona.mastaa wachache sana wenye plan za kuwekeza ktk kilimo.
 
Masanja mjanja sana kasoma mchezo kaona biashara ya Injili inalipa, katumia umaarufu wake wa zamani kama mchekeshaji, sasa anataka kuwa mchungaji avune pesa za wadanganyika..

Soon tutasikia watu wakikimbizana kwenda kwenye kanisa la Masanja..
 
Big up masanja unatisha umeanzisha watafata umetoa elimu ambayo hatufundishwi darasani unaonyesha njia kupitia sanaa.
 
Hongera masanja ni mwanzo mzuri...ila huo uchungaji nenda hatua kwa hatua uive vizuri!
 
Hivi JOTI dini yake ni ipi maana anakoelekea siko, mimi binafsi sitamani hata kumwangalia kwenye kipindi chao, hasa anapoanza mambo yake ya makavu laivu
 
wewe bila shaka hujui lolote juu ya kilimo hasa hicho cha mpunga yaani unabeza Masanja kulima hekta 15?

Unless alikua analima for funny kama ni kibiashara naamini kabisa Masanja ana mtaji wa kutosha kabisa kulima 100+ acres by the way sijambeza
 
Me kiukweli nampongeza masanja kama kijana mchekeshaji na pia alieamua kuwekeza kwenye kilimo,kwa roho safi nakupongeza.Kuhusu uchungaji najua watu wanapima nje na sio ndani,hizi ndio kazi za wanadamu,big up masanja fanya uchungaji kwa mapenzi ya Mungu yeye ndie anaejua unafanya nini.. Mungu akubariki,utuombe na sisi.
 
Unless alikua analima for funny kama ni kibiashara naamini kabisa Masanja ana mtaji wa kutosha kabisa kulima 100+ acres by the way sijambeza
Hata alipoanzia ni kipimo tosha cha uwekezaji,kipimo hichi ndio kitakachompa furusa ya kuwekeza zaidi
 
Back
Top Bottom