Masau Bwire tumechoka na Tambo zako zisizo na maana kila Timu yako ya Ruvu Shooting FC ikicheza na ama Yanga SC au Simba SC

Masau Bwire tumechoka na Tambo zako zisizo na maana kila Timu yako ya Ruvu Shooting FC ikicheza na ama Yanga SC au Simba SC

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Nakushauri tu Mwalimu Masau Bwire ( Msemaji wa Ruvu Shooting FC ) uwe unanyamaza tu kwani Tambo zako huwa haziendani na Ufanisi wa Timu yako Uwanjani pale ikikutana na Yanga SC au Simba SC sanasana huwa unaishia tu Kufungwa idadi Kubwa ya Magoli.

Tumekuchoka na Unatuboa sana Kaka!!
 
Amekusikia Sasa Hivi
Nasema Uongo Ndugu Zangu
 
Hakuna mapya kwa Masau Bwire maana matokeo ya mechi ni kama vile yanajulikana, Labda hamasa zake zinalenga mashabiki waende kwa wingi uwanjani ili wanufaike kwenye mapato

(Ruvu ya Kocha Mkwasa wanajiandaa kucheza na Yanga, hata kule kusini pia Namungo ya Kocha Julio nao wanajiandaa kukutana na Simba).
 
Nyie mafala kweli, kwa iyo mlitaka Bwire aseme tutafungwa tu na Yanga au Simba? Sasa si atakuwa ni msemaji wa hizo timu
 
Hakuna mapya kwa Masau Bwire maana matokeo ya mechi ni kama vile yanajulikana, Labda hamasa zake zinalenga mashabiki waende kwa wingi uwanjani ili wanufaike kwenye mapato

(Ruvu ya Kocha Mkwasa wanajiandaa kucheza na Yanga, hata kule kusini pia Namungo ya Kocha Julio nao wanajiandaa kukutana na Simba).
Mwenyeji ni Simba, Ruvu wananufaikaje na mapato?
 
Mwenyeji ni Simba, Ruvu wananufaikaje na mapato?
Huu uzi sio wa jana. Upo tangu Ruvu ikijiandaa kucheza na Yanga.

Comment yangu ilimlenga Masau na Tambo zake za kuifunga Yanga akiwa Kigoma (Mwenyeji alikuwa Ruvu)
 
Back
Top Bottom