Masauni: Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi inaenda kuleta mabadiliko makubwa kwa Jeshi la Polisi

Masauni: Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi inaenda kuleta mabadiliko makubwa kwa Jeshi la Polisi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amezindua Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi huku akiipa majukumu bodi hiyo kulisimamia shirika ambalo linaenda kutekeleza miradi mbalimbali ambayo inaenda kuleta mabadiliko makubwa kwa Jeshi la Polisi katika kukabiliana na matukio ya kihalifu kwa kutumia dhana za teknolojia ya kisasa ili kuweza kustawisha amani na utulivu kwa Wananchi katika mikoa mbalimbali nchini.

Ameyasema hayo leo Septemba 13, 2024, wakati wa Uzinduzi wa Bodi hiyo yenye jumla ya wajumbe tisa ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Omar Issa ambae alikua Mjumbe wa Tume ya Haki Jinai iliyoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan kufuatilia Mfumo na Utendaji wa Taasisi za Haki Jinai likiwemo Jeshi la Polisi, Magereza, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Mamlaka ya Kudhibiti na Kuzuia Dawa za Kulevya.
d5be3ee0-e48f-459d-9ed8-76b84bf8f5a0.jpg
"Serikali imedhamiria kufanya mabadiliko makubwa katika Jeshi la Polisi sasa huwezi kuwa na Jeshi la Polisi la kisasa ambalo linafanya kazi kutumia mifumo ya zamani ndio maana tunazungumzia upelekaji wa jeshi kwenye ngazi za Kata na uwepo wa ofisi bora na za kisasa, tukiamini uhalifu unaanzia chini, wote tumeshuhudia changamoto kubwa sana ya uhalifu uliokithiri katika nchi hii ukihusisha viungo vya Watoto wadogo ili mtu apate utajiri vitu ambavyo vinaleta uhalifu katika jamii.

"Sasa katika kulipa uwezo Jeshi letu kupitia Shirika la Uzalishaji Mali katika kujenga vituo na kusimamia miradi mikubwa ikiwemo mradi wa miji salama tunaiomba Bodi sasa ilisimamie shirika ili lipate kutekeleza miradi hiyo kwa ufanisi mkubwa ili hatimaye tudhibiti masuala ya uhalifu kwa njia za kisasa," alisema Masauni.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ally Senga Gugu amesema wizara iko tayari kutoa ushirikiano kwa shirika na bodi pamoja na kusimamia mambo ya Kisera ili azma ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya Jeshi letu kuwa la Kisasa zaidi.
 
Hivi Tanzania kuwajibika huwa ni uhaini au

Ukitoa Mwinyi aliyejihudhuru kwa hiari yake

Yakamalizika kwa mzee Edo naye si kwa hiari Bali kelele zilipozidi

Ni lini tutakuwa na utamaduni wa kuwajibika ?
 
MABADILIKO JESHI LA POLISI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni amezindua Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi huku akiipa majukumu bodi hiyo kulisimamia shirika ambalo linaenda kutekeleza miradi mbalimbali ambayo inaenda kuleta mabadiliko makubwa kwa Jeshi la Polisi katika kukabiliana na matukio ya kihalifu kwa kutumia dhana za teknolojia ya kisasa ili kuweza kustawisha amani na utulivu kwa wananchi katika mikoa mbalimbali nchini.

Ameyasema hayo leo wakati wa Uzinduzi wa Bodi hiyo yenye jumla ya wajumbe tisa ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo,Omar Issa ambae alikua Mjumbe wa Tume ya Haki Jinai iliyoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan kufuatilia Mfumo na Utendaji wa Taasisi za Haki Jinai likiwemo Jeshi la Polisi,Magereza,Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU),Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Mamlaka ya Kudhibiti na Kuzuia Dawa za Kulevya.

‘Serikali imedhamiria kufanya mabadiliko makubwa katika Jeshi la Polisi sasa huwezi kuwa na Jeshi la Polisi la kisasa ambalo linafanya kazi kutumia mifumo ya zamani ndio maana tunazungumzia upelekaji wa jeshi kwenye ngazi za kata na uwepo wa ofisi bora na za kisasa tukiamini uhalifu unaanzia chini,wote tumeshuhudia changamoto kubwa sana ya uhalifu uliokithiri katika nchi hii ukihusisha viungo vya watoto wadogo ili mtu apate utajiri vitu ambavyo vinaleta uhalifu katika jamii sasa katika kulipa uwezo jeshi letu kupitia Shirika la Uzalishaji Mali katika kujenga vituo na kusimamia miradi mikubwa ikiwemo mradi wa miji salama tunaiomba bodi sasa ilisimamie shirika ili lipate kutekeleza miradi hiyo kwa ufanisi mkubwa ili hatimaye tudhibiti masuala ya uhalifu kwa njia za kisasa’alisema Masauni

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Ally Senga Gugu amesema wizara iko tayari kutoa ushirikiano kwa shirika na bodi pamoja na kusimamia mambo ya kisera ili azma ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya jeshi letu kuwa la kisasa zaidi.
 
Attachments

  • IMG-20240913-WA2527(1).jpg
    IMG-20240913-WA2527(1).jpg
    101.1 KB · Views: 4

Jeshi la polisi waachane na uzalishaji mali wajikite kwenye masuala ya usalama
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni amezindua Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi huku akiipa majukumu bodi hiyo kulisimamia shirika ambalo linaenda kutekeleza miradi mbalimbali ambayo inaenda kuleta mabadiliko makubwa kwa Jeshi la Polisi katika kukabiliana na matukio ya kihalifu kwa kutumia dhana za teknolojia ya kisasa ili kuweza kustawisha amani na utulivu kwa wananchi katika mikoa mbalimbali nchini.

Ameyasema hayo leo wakati wa Uzinduzi wa Bodi hiyo yenye jumla ya wajumbe tisa ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Omar Issa ambae alikua Mjumbe wa Tume ya Haki Jinai iliyoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kufuatilia Mfumo na Utendaji wa Taasisi za Haki Jinai likiwemo Jeshi la Polisi, Magereza, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Mamlaka ya Kudhibiti na Kuzuia Dawa za Kulevya.

‘Serikali imedhamiria kufanya mabadiliko makubwa katika Jeshi la Polisi sasa huwezi kuwa na Jeshi la Polisi la kisasa ambalo linafanya kazi kutumia mifumo ya zamani ndio maana tunazungumzia upelekaji wa jeshi kwenye ngazi za kata na uwepo wa ofisi bora na za kisasa tukiamini uhalifu unaanzia chini, wote tumeshuhudia changamoto kubwa sana ya uhalifu uliokithiri katika nchi hii ukihusisha viungo vya watoto wadogo ili mtu apate utajiri vitu ambavyo vinaleta uhalifu katika jamii sasa katika kulipa uwezo jeshi letu kupitia Shirika la Uzalishaji Mali katika kujenga vituo na kusimamia miradi mikubwa ikiwemo mradi wa miji salama tunaiomba bodi sasa ilisimamie shirika ili lipate kutekeleza miradi hiyo kwa ufanisi mkubwa ili hatimaye tudhibiti masuala ya uhalifu kwa njia za kisasa’alisema Masauni

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Ally Senga Gugu amesema wizara iko tayari kutoa ushirikiano kwa shirika na bodi pamoja na kusimamia mambo ya kisera ili azma ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya jeshi letu kuwa la kisasa zaidi.

IMG-20240913-WA0246(1).jpg
 
Back
Top Bottom