Masauni: Hakuna sababu viongozi wa CHADEMA kutorejea nchini. Asema Tanzania ni salama

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema Tanzania ni salama na haina tishio lolote la usalama, pia Masauni amesema hakuna sababu ya Mtanzania yeyote ikiwemo viongozi wa CHADEMA waliopo nje ya nchi kutorudi Nchini ili waje kutumia fursa zilizopo za maendeleo pia kushiriki kutoa mchango wa kwa maendeleo kwani Tanzania ni nyumbani kwao.

Masauni alikuwa akijibu swali la nyongeza kutoka kwa Grace Tendega aliyeuliza kuhusu wanasiasa walioenda nje ya nchi ilhali Rais Samia ameshayaweka makundi tofauti pamoja hivyo kutaka kauli ya Serikali kuwataka Watanzania waliopo nje ya nchi kurudi nchini.

Pia Masauni ametumia fursa hiyo kusema Serikali ya awamu ya sita itaendelea kusimamia vyombo vyake vya usalama kutekeleza majukumu yake kwa misingi ya kisheria ili haki isitendeke bali ionekane kwamba imetendeka.
 
Atoe wito rasmi na kuwahakikishia usalama wao
 
Masauni;"Tanzania ni salama na haina tishio lolote la usalama"

Huyu nae anajiongelea tu kama kasuku,

Yule mfanyabiashara aliyeuawa mtwara mikononi mwa polisi ndio usalama huo?

Juzi kuna mfanyabiashara Arusha kauawa mikononi mwa polisi ni usalama huo?

Wale wafanyabiashara wa Kariakoo waliotekwa mchana na polisi mpaka leo hawajulikani wako wapi ndio usalama huo?

Kama huna majibu wakati mwingine ni vizuri kukaa kimya kuliko kuzungumzia usalama wakati unafuga wahalifu ndani.

Haya atuambie uchunguzi wa kushambuliwa Lissu umefikia wapi mpaka sasa?
 
Tuna subiri Siro astaafu ili tuki rudi tuna panda nae mahakamani kama Sabaya.
 
Atoe wito rasmi na kuwahakikishia usalama wao
hapo ndiyo huwa mnakosea ahakikishiwe usalama mara ngapi wakati polisi wapo kulinda raia wote na mali zao au mnataka wawekewe mabodyguard wao pekeyao
 
Penyewe kijana anaongea hivi taifa limekosa hazina naibu kabisa ....hakumbuki hata kipindi Cha magufuli aliwahi semahaya
 
Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema Tanzania ni salama na haina tishio lolote la usalama, pia Masauni amesema hakuna sababu ya Mtanzania yeyote ikiwemo viongozi wa CHADEMA waliopo nje ya nchi kutorudi Nchini ili waje kutumia fursa zilizopo za maendeleo pia kushiriki kutoa mchango wa kwa maendeleo kwani Tanzania ni nyumbani kwao.

Masauni alikuwa akijibu swali la nyongeza kutoka kwa Grace Tendega aliyeuliza kuhusu wanasiasa walioenda nje ya nchi ilhali Rais Samia ameshayaweka makundi tofauti pamoja hivyo kutaka kauli ya Serikali kuwataka Watanzania waliopo nje ya nchi kurudi nchini.

Pia Masauni ametumia fursa hiyo kusema Serikali ya awamu ya sita itaendelea kusimamia vyombo vyake vya usalama kutekeleza majukumu yake kwa misingi ya kisheria ili haki isitendeke bali ionekane kwamba imetendeka.
Tunataka kauli ya Samia, atamke hadharani ili akiri kwamba kulikuwa na tishio dhidi ya maisha ya watanzania wenzetu kutoka serikali ya nduli Mwendazake!
 
Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema Tanzania ni salama na haina tishio lolote la usalama, pia Masauni amesema hakuna sababu ya Mtanzania yeyote ikiwemo viongozi wa CHADEMA waliopo nje ya nchi kutorudi Nchini ili waje kutumia fursa zilizopo za maendeleo pia kushiriki kutoa mchango wa kwa maendeleo kwani Tanzania ni nyumbani kwao.

Masauni alikuwa akijibu swali la nyongeza kutoka kwa Grace Tendega aliyeuliza kuhusu wanasiasa walioenda nje ya nchi ilhali Rais Samia ameshayaweka makundi tofauti pamoja hivyo kutaka kauli ya Serikali kuwataka Watanzania waliopo nje ya nchi kurudi nchini.

Pia Masauni ametumia fursa hiyo kusema Serikali ya awamu ya sita itaendelea kusimamia vyombo vyake vya usalama kutekeleza majukumu yake kwa misingi ya kisheria ili haki isitendeke bali ionekane kwamba imetendeka.
Huyo mbunge aliyetoa hoja hiyo anatoka Chama gani ?
 
hapo ndiyo huwa mnakosea ahakikishiwe usalama mara ngapi wakati polisi wapo kulinda raia wote na mali zao au mnataka wawekewe mabodyguard wao pekeyao
Kwani wakati anashambuliwa na risasi mchana kweupe tena eneo la makazi ya viongozi Polisi hawakuwepo?
 
Masauni;"Tanzania ni salama na haina tishio lolote la usalama"

Huyu nae anajiongelea tu kama kasuku,

Yule mfanyabiashara aliyeuawa mtwara mikononi mwa polisi ndio usalama huo?

Juzi kuna mfanyabiashara Arusha kauawa mikononi mwa polisi ni usalama huo?

Wale wafanyabiashara wa Kariakoo waliotekwa mchana na polisi mpaka leo hawajulikani wako wapi ndio usalama huo?

Kama huna majibu wakati mwingine ni vizuri kukaa kimya kuliko kuzungumzia usalama wakati unafuga wahalifu ndani.

Haya atuambie uchunguzi wa kushambuliwa Lissu umefikia wapi mpaka sasa?
Kuna muuza matunda pale kariakoo karibu na msikiti flani hivi leo ni mwezi wa pili tangu alipochukuliwa na hajulikani alipo
 
Ndio maana nasema huyu hajielewi asifikiri Lissu kutaka guarantee ya usalama ni mjinga,mtu anachukuliwa mchana kweupe baada ya hapo hapatikani tena halafu unasema usalama upo
 
Back
Top Bottom